Hifadhi ya barabara ya Morogoro ni mita ngapi?

Mutensa

JF-Expert Member
Feb 20, 2009
421
90
Wakubwa, nalileta hili ktk sehemu hii maana linagusa uchumi kwa maana ya miundombinu, pamoja na mali za watu na mashirika. Eneo la hifadhi ya barabara, ni mira ngapi kutokea katikati ya bara bara? Nimeona bomoa bomoa imeanza mkrogoro road, wadau wenye uelewa naomba watuelekeze.
 
Ina upana wa mita 60 toka katikati ya barabara kwenda kila upande. Kwa maana hiyo ina upana wa mita 120 including road reserve.
 
Ina upana wa mita 60 toka katikati ya barabara kwenda kila upande. Kwa maana hiyo ina upana wa mita 120 including road reserve.

Kama nimemsikia vizuri kwenye Jicho la ng'ombe kwenye clouds leo,Bwana Magufuli amenukuliwa akisema kutoka mnara wa askari mpaka ubungo ni mita 60 na kuanzia ubungo mataa na kuendelea ni mita 300, na akathibitisa Jengo la Tanesco na Wizara ya Maji vipo ndani hifadhi ya barabara
 
Wakubwa, nalileta hili ktk sehemu hii maana linagusa uchumi kwa maana ya miundombinu, pamoja na mali za watu na mashirika. Eneo la hifadhi ya barabara, ni mira ngapi kutokea katikati ya bara bara? Nimeona bomoa bomoa imeanza mkrogoro road, wadau wenye uelewa naomba watuelekeze.

Hifadhi ya barabara ya Ubungo hadi Kibaha ni mita 300 i.e. mita 150 toka katikati ya barabara kila upande....Kibaha mlandizi ni mita 150 (i.e. mita 75 kila upande)....
Kiujumla barabara nyingine hifadhi ilikua mita 45, ila siku za karibuni imebadilishwa na kuwa mita 60 i.e. ikamaanisha mita 30 toka kati ya barabara kila upande!
 
Nadhani Morogoro Rd kuna sehem ni 90m kila upande, 150 kila upande, 60 kila upande, 30 kila upande, ili mradi tu kuna confusion hapa na pale. Lakini pia inabidi tuangalie cost benefit analysis hasa katika suala la kuondoa majengo ya umma!!
 
Kubomoa majengo ya umma kama la TANESCO Ubungo maana yake ni - umma ulijenga kwa vibali vya kufoji na sasa umma wenyewe unaamua kubomoa. Matumizi mazuri ya pesa.
 
Sasa pamoja na hifadhi kubwa namna hiyo mbona kila siku wanajenge tubarabata twa kupitishia mikokoteni tu badala ya barabara za maana?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom