kadodamsomi
New Member
- Sep 16, 2010
- 1
- 0
Many thanks
aaaa nimekuwa nje sana ya ulingo wa kupost na kushiriki mijadala sasa nimechoka nataka kuweka mambo sawa kwamba ngudzu ni mvumo kwa lugha yetu na nitakuwa navuma si kukaa kimya hapa. Haya mambo ya kuchangia jf pia nimeona kama huduma hizi za kipesa za kitelephone hazipo zaidi ya kutuma vocha hebu nazo basi zisajiliwe tuchangie mawazo na mshiko pia.
Kwa habari ya rais nadhan kubwa linalotusumbua watanzania ni woga na unafiki. Hatuko tayari kufanya mabadiliko hata kwa kutembea hatua moja tu mbele. Tunadanganywa mchana kweupee na runakubaliana tu na status quo. Mambo yaliyoshindikana tangu uhuru leo watu wanadnaganywa na wanashangilia. Naomba niseme mawili tu. Hivi pale tanga yale mashamba tangu enzi tumeanza kusikia serikali inataka kuyagawa kwa wananchi imeshapita muda gani. Hapo sitaji ya kilosa na mvomero ambako watu wanauana kila siku. Juzi jk anwaambia atayagawa cheki shangwe zilivokuwa kwa maskini wale. Checki pale mvomero aliposema atafikiria la kufanya kuhusu shamba la sumaye la ekari 300 watu walivyoshangilia. Hivi jk atafanya nini na shamba la sumaye? Tuache woga na unafiki watanzania tunamhitaji rais jasiri, jabali na shupavu wa kusimamia maneno yake. Aaaa basi bwana leo siku yangu ya kwanza. Tuko pamoja sana! Na idumu jf