Hey,wanawake sijawasikia kuhusu hapa!

Eiyer

JF-Expert Member
Apr 17, 2011
28,258
20,706
Huwa najiuliza,nyie wanawake mnadai haki sawa,kuna eneo sijasikia mnalizungumzia liondoke,suala hilo ni kuwa;Mwanamke anapoolewa kwanini anabadili ubini?Hii si inakua kama "Umemilikiwa"?Unakuta anaitwa Lydia James Rweyemamu,akiolewa na John Bernad Mushi,anaitwa Mrs Mushi au Lydia Bernad Mushi,Why?Au eneo hili kwenu ni poa?
 
Siku hizi wapo wasiobadili.

Iliwahi kuwepo mada nadhani mtu alikua analalamika kwamba mke wake amketaa kubadili au kitu kama hicho, tukajadili sana. Mwisho wa siku ni maamuzi , na siku hizi wanawake (sijui kama ni wengi) wanaamua kubaki na majina yao ya mwisho.
 
Hivi kwanza hiyo ilianzia wapi?Maana sidhani kama ina mahusiano na "kuolewa"!Kwenye harakati za kudai haki zao wanawake yapo ninayoyapinga ila kwenye hili nawaunga mkono!
 
sio wote wanaobadili.
Mke abadili jina au asibadili haimfanyi kutokua mke wa alomwoa.
 
sio wote wanabadili, kama mimi sijabadili na wala sina huo mpango...
 
Nadhani suala la ubini ni hiari zaidi. n way,beijing inatoa mwongozo gani hapo?
 
wanaangalia na ukoo na jina analotoka mwanaume.....

ukoo wenye jina na status...lazima atabadili hata kama mume kasema sio lazima.....
 
Nilivyoona mimi, wapo wanawake wengi wasio na mpango wa kubadili ubini watakapoolewa siku hizi. Lakini wapo wanawake wengine ambao wana mpango wa kubadili, ila si kwa sababu wanakubaliana na dhana ya kwamba mke ni mali ya mume wake, bali wanabadili maana ni desturi wao (na hawafikirii kwa undani zaidi). Na wapo wengine wanaobadili kwa sababu tu hawapendi majina yao. It really depends on the person.
 
Back
Top Bottom