Evari77
JF-Expert Member
- Apr 25, 2015
- 631
- 626
Check kwenye Web yao kama umepata mkopo awamu ya tatu
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kuwafahamisha waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 kuwa imetoa orodha ya Awamu ya Tatu yenye jumla ya waombaji wa mwaka wa kwanza 6,915 waliopangiwa mikopo.
Kati ya waombaji hawa waliopangiwa mikopo, waombaji 4,642 ni wale wanaojiunga na shahada ya kwanza katika vyuo mbalimbali nchini na waombaji 2,273 ni wanafunzi wanaojiunga na Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kwa msingi huo, Bodi inapenda kuufahamisha umma kuwa hadi sasa imekwishawapangia mikopo jumla ya waombaji mikopo wenye sifa 47,751 wa mwaka wa kwanza. Katika awamu ya kwanza, Bodi ilitoa orodha yenye jumla ya waombaji 12,282; Awamu ya Pili wanafunzi 28,554 na Awamu hii ya Tatu wanafunzi 6,915 wamepangiwa mikopo.
Majina yote ya waombaji waliofanikiwa kupangiwa mikopo kutoka katika awamu zote tatu yanapatikana kupitia mtandao wa Bodi wa olas.heslb.go.tz na tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz). Aidha, orodha hizo pia zimetumwa vyuoni kwa ajili ya taratibu za usajili.
Mwisho.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Novemba 13, 2015