HESLB Wanavyotafuna Mikopo na Uchunguzi wa Bodi 2011

Tanzania imelogwa. Hii issue ya board na mikopo ya wanafunzi imekuwa ni ya wanafunzi tu, kwa wenzetu wa nje ni issue ya wazazi na wanafunzi (wananchi wote) Leo mtoto wa mwenzio kakosa loan unatulia kesho zamu ya mwanao na tusikusikie ukilalamika. tuungane tuwaangamize hawa wezi.
 
HESLB jamani mwenzenu hata nikiona neno hilo kichwa huuma,make nimekua mhanga toka Feb 2011 nimekua nakatwa ka-mshahara kangu eti nilikopa huko ili hali ninaka-diploma kangu nimefuatilia wee hadi nimeamua kuacha baada ya kujadili mda mrefu na mwajili wangu juu ya swala hilo na akakubali kustisha makato hayo.
Nilienda Bodi wakaniambia niandike barua na kuambatanisha vielelezo mhimu kama salary slip n.k na nikahidiwa baada ya wk moja ningeweza kujibiwa na kusitisha makato hayo huku nikujulishwa utaratibu wa kurejesha pesa yangu niliyokwisha katwa,lakini hadi leo sijapata feedback yoyote wapo kimywa.Hao ni wezi wakubwa!!!Kuna uozo mwingi wanafanya mfano.kuna rafiki zangu wawili wameshawahi kuingiziwa pesa mara mbili hali huku wameshamaliza vyuo!!.
Yaan basi tu TANZANIA ni nchi yangu lakini sina uzalendo nayo tena natamani bora kua mkimbizi nchi nyingine kuliko kua mtanzania mwenye kudhulumiwa na watanzania wenzangu!!!
 
Hapo ndiyo tatizo langu.. nadhani ingekuwa rahisi zaidi kuivunja bodi ya sasa na kuleta watu wapya ambao ndio wataangalia matatizo yaliyopita na kuja na mapendekezo mapya kuliko kuunda kundi jingine la watu ambalo likimaliza litasababisha uwepo wa kundi jingine. Uchunguzi pekee binafsi naamini ungefanywa na CAG ambaye ofisi yake ipo tayari kufanya huo uchunguzi wa masuala ya Bodi hiyo ya mikopo.
Miaka nane baadaye .. watu wanashtuka na ripoti ya CAG kuhusu Bodi ya Mikopo?
 
Back
Top Bottom