Heshima kwa Mafundi wa Kichina Waliojenga Tazara

Mama Mdogo

JF-Expert Member
Nov 21, 2007
2,961
2,138
Mheshimiwa Nape Nnauye aliandamana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Nd Liu wakitoa heshima zao kwenye mnara wa kumbukumbu za mafundi wa Kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara. Mnara huu uko Majohe,Gongo la Mboto jijini Dar. Hapa katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC ya CCM, Nape Nnauye anaonekana kavaa vazi lisilooana na tukio. Nilitumaini kuwa kwa cheo chake angeziingatia protokali na kuvaa nguo nyeusi au ya deep bluu kama wenziwe. Cha kushangaza zaidi ni kuwa utoaji huu wa heshima kwa utamaduni wa mashariki ya mbali (kuinama au ku-bend) naona hana uzoefu nao. Haya basi, yetu macho na masikio.


NAPE.jpg
 
Na wala hatoi heshima hapo, unaona namna wenye shughuli yao walivoinama?
 
attachment.php


Tofauti utaiona tu! wenzetu wachina ni wachapakazi sana na wanaheshimu sana mambo ya msingi, Hapa alichofanya Nape inaweza isiwe dharau, bali ni kwamba hatuna utamaduni huo wa kuheshimu na kuthamini wengine. Kingine wachina ni watu wanaojali sana afya zao , ndio maana si ajabu ukakuta mchina anaishi mpaka miaka 120 na kuendelea.., kwetu hapa suala la afya tunalichukulia kimzaha, kijana akipata visijenti hakawii kujirusha kiti kirefu, matokeo yake ndio hayo, ya Vitambi visivyotarajiwa.

Kiufupi hatuna Heshima , na wala hatujiheshimu!
 
Labda kwa kuwa Nape ni mrefu ndo maana ameshindwa ku bend kama wachina? Lol...
 
Aaaaaaaa wapi mbona kuna picha inamuonyesha kwenye naniii akiwa amepinda kama upinde, hamna lolote, ubazazi na umagamba wake tu unamsumbua!
 
Back
Top Bottom