Herufi ya mwanzo ya jina lako inabeba tabia yako

Si kweli,nimesoma maelezo ya herufi nyingi hapo si kweli labda umetafiti ktk ukoo wenu but IT IS WRONG,VERY WRONG hata erufi ya jina langu umechemka vibaya sijui umetoa wapi idea hizi

Kweli mangifi hamkosekani
 
Una source yoyote mkuu? Kama ni utafiti umeufanyia wapi, lin nchi zip? Kama ni mawazo yako mtu anauhuru wa kutoa maoni, ila kwa utabiri uko 100perc wrong!!

Mbona umekuwa mkali kama pilipili au herufi yako imekuchafua?
Usipaniki mkuu kawaida
 
ungekua ata na riference ungenishawishi au mfano wa mtu kama E lowasa apo kwenye herufi E mkuu haendan kabisa na hayo maelezo ni wazi kwamba umekurupuka usingizin ukakosa kitu cha kukuweka bize ukatunga hii kitu ukaona ni vyema kupotosha watu

Waswahili mnamatatizo sana sijuwi kuna mtu kakushiki bakora kusoma na kukubali
Au nimekugusa ndio maana unalalama
Lowasa aje asome mwenyewe aone kama sijamgusa
 
Duuu, nimeitafuta herufi V sijaiona, nilitamani sana nione wana tabia gani.
 
Duuu, nimeitafuta herufi V sijaiona, nilitamani sana nione wana tabia gani.

Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara pia anaendekeza usiano nje ya ndoa
 
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara pia anaendekeza usiano nje ya ndoa

rekebisha sentence ya mwisho
 
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara pia anaendekeza usiano nje ya ndoa

W sijamwona, baelezee hapa
 
Kuna ukweli mana hata Bible imeandika jinsi jina la mtu lilivyo ndivyo alivyo mtu mwenyewe . Jina langu linaanza na A najaribu kujitathmini na tabia zilizoorodheshwa hapo juu ni kweli
 
Umeeleweka kiongozi

Na kuonyesha kama nimeelewa ipasavyo, nasisitizia na hii hapa.....

HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.

Sasa sijajua kwa wale wenye majina zaidi ya moja inakuwaje? Hapa simaanishi mambo ya ID za JF, la hasha yale majina yetu halisi.
 
Mbona V, W X Y Z hakuna
HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi
 
Back
Top Bottom