Heri nisiwe DIWANI kuliko kuwa GAMBA...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mwishoni mwa juma nilikuwa nyumbani nilikozaliwa-Visiga,Kibaha.Nikiwa sina hili wala lile,nikapata ugeni nyumbani kwetu.Wakaja jamaa watatu wakidai kuwa na ujumbe wangu.Nikawakaribisha.Salamu zikafuata halafu mazungumzo.

Wakaniarifu kuwa,wao wameagizwa na wazee na vijana wa kata yangu waje kuniambia uamuzi wa wanakata juu ya nani anatakiwa kuwa Diwani wa Kata yetu hapo 2015.Wanataka kumandaa kabisa.Wanadai wamemchoka Diwani aliyepo kwakuwa hakufanya lolote kwa miaka yake 12 aliyokuwa madarakani.Pia,kwakuwa ni Darasa la saba.Wanamtaka msomi na mwenye uchungu na maendeleo ya Kata.Wameniona mimi nafaa.

Wageni wangu wakanieleza mchakato mzima uliwafikisha katika uamuzi wao huo.Mwishoni nikawauliza: kwa chama gani? Wakanijibu: CCM.Mwili wangu ukasisimka kama nimepigwa shoti ya umeme.Sikuwafokea.Nikawajibu kistaarabu tu: Ni heri nisiwe Diwani kuliko kuwa Gamba.Walionyesha kushtuka.Hawakuchelewa kuaga.

Eti WanaJF,nimekosea hapo?
 
Nadhani kwa kutii kile moyo wako unapenda, haujakosea.
The unseen is illustrated by the seen.
 
mkubwa!ulikosea kitu kimoja,kwanza ungewaanzia hapohapo u-M4C(ungewavua magamba ukawavalisha magwanda) alafu mwisho ndio ungewapa hilo jibu,il wakirudi huko kwa waliowatuma washangae jamaa waliondoka wakiwa gamba na wamerudi na magwanda
 
​Uko sahihi mkuu! watu wa pwani wanahitaji ukombozi wa fikra, ipo siku na wao wataikataa ccm
 
Mwishoni mwa juma nilikuwa nyumbani nilikozaliwa-Visiga,Kibaha.Nikiwa sina hili wala lile,nikapata ugeni nyumbani kwetu.Wakaja jamaa watatu wakidai kuwa na ujumbe wangu.Nikawakaribisha.Salamu zikafuata halafu mazungumzo.

Wakaniarifu kuwa,wao wameagizwa na wazee na vijana wa kata yangu waje kuniambia uamuzi wa wanakata juu ya nani anatakiwa kuwa Diwani wa Kata yetu hapo 2015.Wanataka kumandaa kabisa.Wanadai wamemchoka Diwani aliyepo kwakuwa hakufanya lolote kwa miaka yake 12 aliyokuwa madarakani.Pia,kwakuwa ni Darasa la saba.Wanamtaka msomi na mwenye uchungu na maendeleo ya Kata.Wameniona mimi nafaa.

Wageni wangu wakanieleza mchakato mzima uliwafikisha katika uamuzi wao huo.Mwishoni nikawauliza: kwa chama gani? Wakanijibu: CCM.Mwili wangu ukasisimka kama nimepigwa shoti ya umeme.Sikuwafokea.Nikawajibu kistaarabu tu: Ni heri nisiwe Diwani kuliko kuwa Gamba.Walionyesha kushtuka.Hawakuchelewa kuaga.

Eti WanaJF,nimekosea hapo?

Hongera kwa kumkana shetani na ghiliba zake tena ukamshuhudia Mungu mbele ya watu wa mataifa....Ila inekuwa heri kama ungefanya yafuatayo..
1. Kukubaliana nao halafu uwaombe ukae nao mjadili mstakabali wa kata yenu- Naimani wangekubali hilo kwani wwe umewakubalia kwenye lao la kuwa kiongozi wao.....
2. Hapa ungapata nafasi ya kuwa maana ya SISI TUNA MUNGU NA WAO WANA UFISADI wakiwa wote, pamoja na ugumu wa mioyo yao watu wa PWANI, naimani wasingeeuka nyuma ili wawe jile la CHUMVI bali wanekuamini na kukufuata wewe Jabali lao.. Hapo ukombozi unetimia....

Ila hongera sana kwa kile umekifanya...
2.
 
hongera kwa kumkana shetani na ghiliba zake tena ukamshuhudia mungu mbele ya watu wa mataifa....ila inekuwa heri kama ungefanya yafuatayo..
1. Kukubaliana nao halafu uwaombe ukae nao mjadili mstakabali wa kata yenu- naimani wangekubali hilo kwani wwe umewakubalia kwenye lao la kuwa kiongozi wao.....
2. Hapa ungapata nafasi ya kuwa maana ya sisi tuna mungu na wao wana ufisadi wakiwa wote, pamoja na ugumu wa mioyo yao watu wa pwani, naimani wasingeeuka nyuma ili wawe jile la chumvi bali wanekuamini na kukufuata wewe jabali lao.. Hapo ukombozi unetimia....

Ila hongera sana kwa kile umekifanya...
2.
usichangamane nao shetani naye ananguvu ila big up
 
naomba uongoze katika kutoa elimu ya uraia,pia m4c maana hao wananchi wahitaji ukombozi wa kifikra
 
Hujakosea, kama kweli wanakutaka watakukubali kwa chama chochote.
 
Back
Top Bottom