Henry Dafa Shekifu sasa Hivi ni "Dr Henry Dafa Shekifu"

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Kuanzia leo yule mbunge wa Lushoto kupitia CCM bwana Henry Dafa Shekifu anajulikana kama Dr. Hendry Dafa Shekifu.
Souce Bungeni.


Dr. wanazidi kuongezeka.
 
Mhhh kwa wananchi wake hiyo doctorate yake inawasaidia nini
Au kuipata ameleta mabadiliko gani kwa wananchi wake
Bunge limejaa wasomi kibao lila u8tendaji kazi wake ni kama mle ndani hakuna kitu
hatuyaoni mabadiliko au ufanisi wao kwenye kazi kulingana na usomi wao
 
Huyu mtu ni mwizi hakuna mfano. Alishiriki sana katika kuyaua mashirika yetu ya umma kwa vile RTC na Sukita. Ni mnafiki, mchawi na mpenda madaraka. Ndiye aliyekuwa kampeni meneja wa jakaya 2005 na 2010 Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

Nyerere alishawahi kumweka rumande kwa ajili ya ulanguzi.
 
Madokta wengi wa kisiasa wana mafuvu matupu hawana msaada wowote na hawataki kujishughulisha zaidi ya zaidi ya kunyemelea ubunge na kusubiri huruma za rais ili wapewe uwaziri, ubalozi, ukuu wa mikoa na hata Wilaya. Madokta wa nchi za wenzetu utawakuta wakifanya tafiti iwe ni maabara au tafiti za kijamii au nyinginezo za kuisaidia jamii lakini huku kwetu akina Paseko Kone na wenzake akina Makofuli wanafanya nini cha maana?
 
Huyu jamaa namkumbuka alivyokua mkuu wa mkoa wa Manyara kabla ya kua mbunge alitaka kuzipiga kavukavu na yule mbunge wa Simanjiro bwana Ole Sendeka! Polisi ndio waliinusuru ile patashika jamaa mkorofi sana!
 
Mbona ma-Dr wapo wenge tu lakini hakuna la maana lolote, mfano si huyu Dr kichwa nazi kutoka msoga!!
 
Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua! Cheo cha heshima tu hicho kakangu. Ningekithamini zaidi kama angekuwa AMEKITOLEA JASHOOOO!
 
Kuanzia leo yule mbunge wa Lushoto kupitia CCM bwana Henry Dafa Shekifu anajulikana kama Dr. Hendry Dafa Shekifu.
Souce Bungeni.


Dr. wanazidi kuongezeka.

Hata angeitwa debe haina tatizo,shida inakuja ktk uwajibikaji kwa wananchi ndio Jambo la msingi hayo mengine hayawahusu wananchi kabisa.Wanajiita madokta kiingereza cha darasa la Saba hawakielewi!!!!
 
CCM hata km angeitwa Professor bado ni walewale. Halafu vyuo gani hivi hawa wanasiasa walio wengi wanasomea? Ila jana kidogo nilie mbele ya TV wakati wagombea wakijinadi bungeni. Kuna mgombea mmoja kutoka Zanzibar amejieleza kuwa ana Masters degree 2, MBA na nyingine nimeisahau. Uzoefu wako ni pamoja na kuwahi kuwa Deputy Secretary wa wizara ya elimu SMZ nk. Miongoni mwa mwaswali aliyoulizwa ni challenges & opportunities if any za Tanzania ndani ya EAF, yule bwana amesema bila aibu kwamba hajui. Nimejiuliza maswali mengine na bado hata sasa najiuliza sipati jibu. Mtu amekuwa hadi deputy secretary tena wizara ya elimu huwezi kujieleza maswali ya form 4. Hivi huyu bwana alifikaje kwenye nafasi hyo? Mtu umechukua form, umejaza, umerudisha hadi unaenda unaulizwa swali km hilo unasema sijui!!!!!!!!!!!. MUNGU LISAIDIE TAIFA HILI
 
Kuanzia leo yule mbunge wa Lushoto kupitia CCM bwana Henry Dafa Shekifu anajulikana kama Dr. Hendry Dafa Shekifu.
Souce Bungeni.


Dr. wanazidi kuongezeka.

Ni zile za kupewa kama za Mwenyekiti wao wa chama?
 
PHD English Zero= Useless.

kwani wamepata PHD za linguistic? By the way, ningependa kujua thesis yake ilihusu nini na hiyo PHD ni ya kutoka chuo gani, isije ikawa kama PHD ya Diallo ama ile ya Nchimbi na Kamala ambao walilazimika kusoma upya Mzumbe
 
Inaelekea kuna shimo wenzangu wanaenda kuokota takataka inayoitwa Phd aka u dokta. Sijui linapatikana wapi!!
 
U-Dr wake ni wa chuo kikuu gani? Hebu tupeni taarifa kamili. Obama ana PhD lakini hamna mtu aliyem-adress hivyo. Lakini ni mchapa kazi sana. Hapa kwenu mtu akitaka kuwa fisadi anatafuta PhD. Aibu tupu!
 
What is the hell is This nonsense!! Walioshindwa wanapoteza hela za kodi kujisomea Shahada Zisizo na Maana yoyote!! Aka....... Mbali!!
 
waeshimiwa huyu mkuu alikuwa ni mkuu wa mkoa wa manyara na si wilaya kabla ya kuwa mbunge huko tanga nakuiachia nafasi hiyo ya ukuu wa mkoa nafasi ambayo inashikiliwa na bwana Eraston mbwilo kwa sasa. ((kuweka tu kumbukumbu sawa)) na kama si kumchokoa chokoa kikwete kuwa anadumbukiza ndugu jamaa na rafiki kijana alikuwa anaukwaa uwaziri
 
Madokta wengi wa kisiasa wana mafuvu matupu hawana msaada wowote na hawataki kujishughulisha zaidi ya zaidi ya kunyemelea ubunge na kusubiri huruma za rais ili wapewe uwaziri, ubalozi, ukuu wa mikoa na hata Wilaya. Madokta wa nchi za wenzetu utawakuta wakifanya tafiti iwe ni maabara au tafiti za kijamii au nyinginezo za kuisaidia jamii lakini huku kwetu akina Paseko Kone na wenzake akina Makofuli wanafanya nini cha maana?

mkuu umenimaliza mbavu 'MAKOFULI'
 
Back
Top Bottom