Hemorhoids

Mwaka wa pili nasumbuliwa na HEMORHOIDS .Nimetibiwa Kwa mvungi na Kairuki kwa kupewa Anusol cream na ANUSOL TABLE .LAKINI HAKUNA NAFUU .JE KUNA TIBA MBADALA? NAOMBA USHAURI.
Jaribu hii maji ya ganda la mgomba unaponda na kupaka kwenye unyeo kutwa mara tatu kwa wiki mbili.mi nimepona .anusol haikunisaidia pamoja na kuitumia kwa miaka miwili .mgomba just two wiki. usipopona nenda hospitalini kafanye Oparesheni ya ukataji hiyo Hemorhoids source https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/147367-kinyama-sehemu-ya-haja-kubwa.html
 
Labda wengine hatujaelewa una tatizo gani, maanake kama wewe si Medical personnel ni vigumu kuelezea hasa nini maana ya haemorhoids. Lakini kuna nnamna nyingi za kutibu haemorhoids sio tu kutumia rectal suppositories (anusol). Nenda kwa madaktari waliosoma watakutibu.
 
Ni kitu gani?
Hemorhoids au Anal Fissure au Piles kwa kiswahili ni Mwatuko wa mfereji wa haja kubwa (Anal Fissure) Imeandikwa Na Dr.Henry Mayala




ndani.jpg
Ni tatizo ambalo huathiri wote wanaume na wanawake, vilevile watu wa rika yote kwa ujumla. Tatizo hili husababishwa na mpasuko au mchaniko katika eneo la mwisho la mfereji wa haja kubwa.


Nini husababisha mwatuko wa mfereji wa haja kubwa?


-aina yoyote ya ajali katika mfereji wa haja kubwa husababisha mwatuko kama ifuatavyo:


• Kupata choo kingi na kigumu kwa muda mrefu
• Tatizo sugu la kuharisha
• Kuvimba kwa eneo la mfereji wa haja kubwa (inflammation)


-sababu nyinginezo ni kama zifuatazo:



  • Ngono ya njia ya haja kubwa
  • Kansa
  • Virusi vya ukimwi
  • Kaswende
  • Kifua kikuu
anal_fissures.jpg
Watu gani wanaweza kupata tatizo hili?



  • Watoto chini ya mwaka mmoja (infants)
  • Umri mkubwa- kwasababu kuna upungufu wa ugavi wa damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa
  • Kupata choo kigumu kwa muda
  • Wanawake wakati wa kujifungua
  • Crohn’s disease

Dalili:

  • Maumivu mara baada ya haja kubwa
  • Damu kwenye kinyesi na huonekana kwenye karatasi ya chooni (toilet paper)
  • Maumivu huweza kuwa makali mpaka kumfanya mtu ajizuie kwenda msalani.
  • Kuwashwa
Vipimo na uchunguzi:

  • Sigmoidocopy
  • Colonoscopy
Matibabu:

1. Huweza kutibiwa kwa dawa katika hatua za hawali;


• Dawa za kulainisha choo

• Sitz bath
• Cream za kupaka (Anusol, zinc oxide)
• Nitroglycerin
• Botox
• Calcium channel blockers (nifedipine and diltiazem)

2. Kama tatizo hili limekuwa sugu na halitibiki kwa tiba nyingine, basi Upasuaji ndio huwa tiba mwafaka

• Partial lateral internal sphicterotomy
• Anal dilation

Jinsi ya kuzuia mwatuko wa mfereji wa haja kubwa:

• Vyakula vya kulainisha choo- matunda na mbogamboga
• Kunywa maji mara kwa mara
• Na fanya mazoezi

Source:Mwatuko wa mfereji wa haja kubwa (Anal Fissure)

Chanzo:
https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/146913-mwatuko-wa-mfereji-wa-haja-kubwa-anal-fissure-bawasiri-au-futuro.html

chanzo
http://en.wikipedia.org/wiki/Hemorrhoid

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom