Helpless:...My Dad's Gone!

PJ,

Nimesikitika sana kupata hizi habari. Nami naungana na familia ya wana JF kukupa pole za rohoni kabisa....nikitumai yote yatokeayo hapa duniani ni mipango ya mwenyezi MUNGU. Nae akapate kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kumkosa Baba Duniani lakini tukiwa na Imani kuwa ijapo siku tutajaonana tena!.

Niungane na wengi kuwa nawe Kiroho kutokana na sababu za kijiografia!.

DAIMA IMEMPENDEZA YULE ALIYE TUFANYA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!

AMEN.
 
what can i say? Pole PK, i understand your pain, may the one and only true God confort you. And may the soul of your father rest in peace, amen!
 
Pole sana PJ,Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu,naamini kuwa Mugu atakupa faraja ya kipekee kabisa.
 
Pole sana ndugu yetu. Mungu akutie shime wewe na familia yenu kwa ujumla katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na baba yenu mpendwa.
 
duh, pole sana mkuu kwa msiba huu mzito na Mwenyezi Mungu akupe nguvu zaidi wakati huu mgumu.

Mungu hailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
Pole sana PJ, na familia.
Wote tunapitia huko. Wengine tumepitia hayo na makubwa zaidi, ila cha kufariji tu ni kuwa Mungu yupo...and He's got your back!!

RIP Mzee
 
Pole sana mkuu! Mungu akupe ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
 
Kuhusu maandalizi ya maziko:-

Maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu yanafanyika nyumbani kwa Mhandisi Protas Mwasyoke, Ukonga Kipunguni.

1. Iwapo una gari binafsi unafuata njia ya kwenda Gongo la mboto, kabla hujafika Ukonga Magereza unakata kushoto eneo linalojulikana kama Banana. Unafuata njia ya lami (ni kama km 2.5 kutoka Banana) hadi kituo cha Matembele. Ukiuliza Mr. Mwasyoke hapohapo Matembele watakuonesha nyumbani kwake, ama ukipiga namba za simu hapa chini utaelekezwa.

2. Iwapo unapanda daladala, unapanda zile za kwenda Gongolamboto, unashuka Banana. Pale unapanda daladala za kwenda Kitunda, unashuka Matembele. Hapo Matembele ukiuliza kwa Mr. Mwasyoke basi utaelekezwa au unaweza kupiga namba za simu zilizooneshwa hapo chini.

Mawasiliano:
0784 374 166
0754 829 855
0755 235 323
0713 329 635

Asanteni

Idimi

 
Pole sana kiongozi..Mungu akutie nguvu na uwe jasiri katika kipindi hiki kigumu...tafadhali ni PM unipe number yako tusaidiane kwa yale yatakayowezekana hapa Dar ..pole sana mkuu wangu
 
Dah poleni sana wakuu najua mpo katika kipindi hiki kigumu. Tupo pamoja kisala na maombi.
R.I.P baba PakaJimmy,
Bwana ametwaa lihimidiwe jina la bwana.
 
Pole saaaaaaaaaaaana brodah!!! may his soul rest in peace!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom