Help me please, msaada na ushauri!

Mtoa mada... nimependa swali lako kwa sababu lina uhalisia... ni muhimu kuwa na uhakika wa madhumuni hasa ya mahakama hii. itahusika na vitu gani? Na inawaweka katika sehemu gani wale ambao si waislamu ila wameolewa na waislamu (kama dada zako). Nina maswali mawili
1. Je baada ya dada zako kuolewa, walibadili dini? yaani kuslimishwa? maana kwa jinsi ulivyosema huyo anatewekewa tinted ni kama ameslimu? hebu tufafanulie hapo vizuri.
2. Kama hawakubadilisha dini, nini makubaliano yao na waume zao?, ni kila mtu abaki na dini yake na aheshimu dini ya mwenzake au ?

Kama jibu la swali la 1 ni ndio basi hiyo haikuhusu wewe kwa kuwa dada zako ni waislamu na mambo ya mahakama ya kadhi ni yao wewe hawakuhusu.

Kama jibu la swali la pili ni kuwa walikubaliana na kuna makubaliano flani juu ya dini zao, basi ni wakati mzuri wa dada zako kuwauliza waume zao nafasi yao wao katika mahakama hii. Na ikiwezekana wakubaliane kimaandishi kuwa if anything happens then mahakama itakayomaliza matatizo yetu ni Ya Jamhuri na Muungano na si vinginevyo!! ama sivyo basi ndo uwaambie dadizo waanze kupunguza investment kwa waume na ndoa zao bali wajiwekee akiba au waivest kisiri siri just in case.........lol!!
 
Aisee jamaa yangu mambo ya kidunia tuyaache duniani, tusijaribu kuchanganya mambo hapa. Hakuna muislamu aliyeishi kwenye uislam thabiti akaoa dini nyingine bila mwanamama muhusika kusilimu aliko kuwa muislam. Kwa hiyo hao dada kama ni kweli wameolewa na waislamu basi nao ni waislam ispokuwa wewe uliebaki ndio mkristo. Na sheria zote za dini ya kiislam hao kina dada wanatakiwa wazifuate bara'bara. Mix Grill katika uislam haipo labda wawe vitoweo tu na hao pia kidini hawatambuliki kama wake na waume bali ni wazinifu tu.

........ Uyasemayo ni kweli kabisa ndugu yangu tena kidini inaelezewa wazi but in practical wapo wanaoishi pamoja ilhali si wa dini moja......... hawa tunawaelezeaje?
 
Kama jibu la swali la pili ni kuwa walikubaliana na kuna makubaliano flani juu ya dini zao, basi ni wakati mzuri wa dada zako kuwauliza waume zao nafasi yao wao katika mahakama hii. Na ikiwezekana wakubaliane kimaandishi kuwa if anything happens then mahakama itakayomaliza matatizo yetu ni Ya Jamhuri na Muungano na si vinginevyo!! ama sivyo basi ndo uwaambie dadizo waanze kupunguza investment kwa waume na ndoa zao bali wajiwekee akiba au waivest kisiri siri just in case.........lol!!
Jibu la swali la pili likiwa ndio, ina maanisha wote hao wamehasi dini zao na kuamua kuishi kivyao vyao bila ya kufuata misingi ya dini.

Kwa hali hiyo basi si kanisa wala Msikiti utakao husishwa kwenye kesi zao... Jinsi hiyo basi hakuna suala la Mahakama ya Kadhi kuhusika hapo... Kwa maana hata huyo aliye itwa Muislam amekwisha hasi dini yake sawa sawa na hao madada.
 
JADILI KWANZA ILIKUWAJE WAKAHAMA HUKO WALIPOKUWA na urekebishe hayo ili waweze kurudi kwa kuona ubaya wa uislam, tuondolee hizi hadithi zako za abunuwasi humu

Hapa naunga mkono kabisa.

Wakristo wengi wenye ndugu zao ambao wameingia kwenye Uislam, kwa hiari yao, huwa wanakataa kukubali kwamba ndugu zao hao - wa kike au wa kiume - wameingia kwa hiari yao, wanaona kwamba WALILAZIMISHWA.

Tujiulize:

1) Kuna ushahidi wowote kwamba huko ambako Wakristo hao wa zamani wamenyanyashwa au kudhalilishwa, kwa kuwa tu wamekuwa Waislam?
2) Je, kuna ushahidi wowote kwamba hao waliokuwa Wakristo wamelalamika kwamba wamedhalilishwa au kudhulumiwa haki zao?

Hapa duniani maisha ni mafupi kabisa. Kama mtu amechagua kuwa na imani yake, basi, abakie na imani yake, na kama mtu anataka kubadili imani yake, abadili na asitishwe.

Yapo mambo mengi ambayo Uislam umepotoshwa juu yake, kwa mfano:

1) Nchini Marekani, watu wengi - licha ya Obama kuitwa Barack Hussein Obama (na katika kuapishwa kwake aliapa kwa jina hilo...) - wanaamini kwamba WAISLAM WOTE ni magaidi.
2) Hapa nchini, baadhi ya madhehebu (ingawa neno hili si sahihi...) ya Kikristo huwafundisha (nje ya 'katekista') kwamba Waislam ni watu wabaya, wasiomcha Mungu, washirikina, wenye "kufuga majini", na kadhalika...

Nauliza:

1) Wapi kwenye Quran imeandikwa kwamba ukiwa Muislam shurti uwe mshirikina au ufuge majini?
2) Kuna ushahidi gani kwamba ni Waislam pekee wenye kufuga majini?

Pale ambapo sisi wote tutakapotambua kwamba, (1) Mungu habagui, (2) Mungu hajasema kuna dini iliyo bora zaidi ya yule kwenye Kuamini pekee, na (3) kwamba Siku ya Hukumu kila mtu atahukumiwa kwa "matendo yake" peke yake, na hatokuwa na fursa ya kusema, "nilifanya hivi kwa ajili ya kumfuata fulani..." basi siku hiyo itakuwa ya FURAHA KUU!

Wanadam, kumbukeni, kila unachokisema, kibaya, juu ya IMANI ya mwenzako, Mungu anakuhukumu kwa hilo. Malaika wako wanaandika rekodi yako, matendo mema upande wa kulia, mabaya upande wa kushoto. Siku ya Hukumu (Al Qiyama), mizania yako ya kushoto ikiwa nzito kuliko ya kulia, njia yako ni motoni tu... hutauona mlango wa pepo.

Unayejiita "Mwana wa Mungu", rekebisha kauli yako, tubia makosa yako.... Ni Amri ipi ya Mungu inayosema "usimshuhudie jirani yako uongo"?

Nimezaliwa Muislam, sioni haya kuitwa Muislam, na katu sitaacha kuwa Muislam. Ukiona Uislam unapigwa vita mbele, nyumba, kushoto na kulia, basi ujue kwamba HIYO NDIYO NJIA SAHIHI ZAIDI ya KUMCHA MUNGU!

"Mwana wa Mungu", tafuta Quran uisome, ujue Mungu anakuambia nini, kabla ya kubwatuka na kashfa za rejareja, unajichulia dhambi kwa maneno yako ya UONGO!

./Mwana wa Haki

P.S. Hao dada zako "wanawajua" majini kweli, wanayolazimishwa kuyafuga? Au unawashuhudia..... ?
 
Hata Mtume Muhammad alipinga wezi kukatwa mikono. Yeye alisema tu kwamba,''nisipoweka hizi adhabu kali,watu watasema mimi nashirikiana na mafisadi''
 
Ili sheria ya kiislam katika mambo ya ndoa na mirathi iweze-kutumika lazima mahakama iangalie ''mode of life test'' ya familia. kama ndoa ilifungwa kwa taratibu za kiislam na maisha ya wanandoa hao ilikuwa kwa misingi na taratibu za kiislam, basi miradhi itafuata taratibu za kiislam na itakuwa jukumu la mahakama ya kadhi kusikiliza shauri hilo.

Endapo muislam na asiye muislam wamefunga ndoa (labda bomani au kimila) au wanaishi pamoja, miradhi yao haiwezi kusikilizwa na mahakama ya kadhi. Kwa kifupi mahakama ya kadhi ni kwa waislam pekee na haiwezi kutoa hukumu yoyote kwa asiye muislam. Pia mahakama ya kadhi haishughuliki na kesi za jinai.

Nashangaa kuona unatoa mifano ya Somalia ambayo hata serikali yake haijulikani, kwa nini usitoe mifano ya Zanzibar ambapo kuna mahakama ya kadhi na hatujasikia mtu amekatwa mkono. Vile vile Kenya na Uganda kuna mahakama ya kadhi na hakuna aliye katwa mkono.

Tusipende kupotosha mambo kwa imani ya kidini zetu.

''mwana wa mungu''- je wewe unataka kufaidika na miradhi ya dada zako? Na imekuwa vipi dada zako wote wawili ambao wametoka katika familia ya kilikole kuolewa na waislam? tena wenye misingi mizito ya uislam? nadhani dada zako wamewapenda sasa hao waislam na ndio maana kwa kipindi chote wameishi nao na hata kupata idadi hiyo ya watoto. nadhani kinachokutisha ni kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi kutakufanya usipate urithi kutoka kwa shemegi zako!!! Mali ya shemegi zako waachie warithi dada zako na watoto wao bwana.

Nimeona uchangia wako wa maada wa leo na jana katika ile habari ya ajali ya mabasi ukizungumzia kufuga majini na uislam. Jaribu kuheshimu dini za wenzako na sikutegemea mtu kama wewe ambaye leo umejitambulisha kuwa "mlokole" ukitoa habari ambayo huna hakika nao. Inawezekana kuna muislam mmoja ana tabia ya kufuga majini, lakini unaweza ku-conclude kuwa waislam wote wanafuga majini? Juzi kuna mchungaji wa kilokole mwanza ameshikwa na viungo vya albino, je na waislam nao wa-conclude kuwa walokole wanauwa albino??? Huu ni mtazamo finyu na sidhani kama jamii forums ni jukwaa la mtu mmoja kutoa kashfa za kidini. Jamii forums ni sehemu ya watu wastaarabu ambao wanaheshimu dini na tamaduni za watu.
 
nafikiri hauijui dini yako. kuna wanawake wangapi wa kiislam wa ulaya mashariki,na middle east ambao wanalazimishwa hata kujilipua, wakiambiwa wataenda kwa mungu, wakitishiwa kuwa wakikataa watasingiziwa kuwa wamezini na kupigwa mawe hadi wafe? HAUJUI HILI?

Acha kuongopa. Hizo habari si za kweli.
 
Mwana wa Mungu - kwanza pole sana kwa jinsi issue ya dada zako ilivyokuingia moyoni. Napata picha kuwa umezaliwa na kulelewa katika familia iliyo attached - kupendana, kujaliana, kutakiana mema etc. Elewa familia nyingine hawajali sana nini kinampata ndugu yake - kila mtu na hamsini zake - kila mtu ana maamuzi yake etc. Hivyo kwa hilo nakupongeza sana na nawapongeza wazazi wako kwa malezi mema.

Pili swala kama hili - sio la kutaka ushauri - mambo ya imani ni mambo ya rohoni - hivyo litatue katika ulimwengu wa roho - nikiwa na maana kuwa MAOMBI NI SILAHA KUBWA SANA - chukua hatua ya kufunga na kuomba ili Mungu aingilie kati katika swala zima la dada zako - anaweza kuwaokoa hao shemeji zako kama ndio unachopenda - SOMA YEREMIA 33:3 - Mungu anaahidi kukuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua.
GOD CHANGES THINGS, CIRCMUMSTANCES, ENVIRONMENT - USIOGOPE
WE HAVE A POWERFUL LIVING GOD AND HE IS ABLE - anawapenda WANADAMU WOTE SOMA JOHN 3:16 - anawapenda wanadamu wote kwa ujumla na anataka wote wafike mbinguni
 
Kwa vile ndoa zao hazikuwa za kupangwa ni hiari yao wenyewe, basi wee endelea kuwapenda tu dada zako, na kwa vile una hofu kubwa watateseka jipange na kujiandaa kuwasaidia kama hili litatokea. Lisipotekea basi ni heri. Huyo ambae unaona anateswa kwa kuwa ndani ya tinted nafikiri ni hisia zako tu...anampenda mumewe na ndio maana yupo humo. Angalia wewe usijekuwa ndie utakayemletea shida katika ndoa yake.

Ukweli ni kwamba hata katika ndoa za kikristo wapo wanaoteseka sana na maswala yote hayo unayodhani yataletwa na mahakama za Kadhi. Sasa usitumie hili kama ndio sababu, mila zetu na desturi zipo zinazowanyima wanawake na watoto haki na hizi je? utazifanyia nini pale dada yako mwingine atakapoolewa na wenye kushika mila hizi. Acha hofu tunza familia yako. Wee biblia si imekufundisha dada yako ataachana nanyi ataambatana na mumewe...chokochoko tena za nini?
 
Back
Top Bottom