Hellen Kijo Bisimba ni nani?

Unaloongea ni kweli.... Lakini kumbuka demand si lazima kudai kwa ubabe.... Waweza dai bila kutumia huo Ubabe. Maybe sababu J.K ana madhaifu kibao na wananchi hawamtaki wanaona sawa tu! But at the end of the day kauli ya "NAMTAKA" moja kwa moja is not respectful.... Ni sawa na wewe uko kwako anakuja mwanao kazini mbele ya wafanyakazi wenzio na kukudemand "Baba nakutaka uende sasa hivi nyumbani ukashughulikie swala la Umeme".....

You are quite correct AshaDii, Hellen Kijo Bisimba amevuka mipaka ya uhuru kwa kujieleza kwa kumtamkia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kusema NAMTAKA! Hicho kivuli cha NGO anachokitumia akumbuke amepewa kwa niaba ya huyohuyo anayemshurutisha.
 
....ameamua ku-take advantage ya mgomo wa madaktari nayeye apate kusikika.....mbona muda mrefu sijaisikia hii asasi ikikemea lolote japo matukio chungu tele ya uvunjaji wa haki za binaadam yanatokea kila kukicha...:juggle:
 
Dah! CCM wameshtuka, wanaanza kumtengenezea kesi ya uraia! Kazi kweli kweli! Yaleeeeee ya Jenerali! Ukiwakamata pabaya...wewe si raia...Bashe walisema hivyo hivyo...Sioi wakasema nae sie...sasa Helen! Itakuwa ngumu!
 
mama Kijo ni mtusi tusidanganyane hapa aliolewa na mtanzania kuna habari kuwa ama ana uraia wa nchi mbili au hajaukana uraia wake wa Lwanda.
Kwani uraia wa nchi ya Tanzania unapatikanaje? Je sheria za Tanzania zinaruhusu kuwa na uraia wa nchi mbili?
 
HELLEN KIJO BISIMBA NI................. Mama wa kitanzania anayekusaidia wewe uliyeandika Utumbo katika safu hii ukihoji Hellen Bisimba ni nani ????? kufahamu yale yote yanayofanyika katika nchi hii hasa kwa watu wa aina yako ambao hawajui kinachoendelea katika chi yao viongozi wanapo shindwa kutimiza majukumu yao kwa wananchi waliowaweka madarakani mfano kiongozi wa nchi J.Kikwete anaposhindwa kuona matatizo yanayowakabili watu wake hata kama yapo nje ya uwezo wa serikali yake kinachotakiwa sio vitisho kwa wananchi bali ni kukaa nao ili kupata ufumbuzi wake kwa njia ya mazungumzo.
Sasa tangu mgomo wa madaktari wetu mwezi uliopita Kiongozi wa nchi yetu hajapata kuzungumzia lolote linalohusiana na mgomo wa madaktari yeye ameamua kukaa kimya kana kwamba hakuna tatizo lolote katika nchi yake ndipo akijitokeza mama Hellen Kijo Bisimba na wenzake ambao baada ya maisha ya Wtz yamepotea au yatapotea ameamua kukusaidia wewe ambaye unaonekana unafikiri kwa kutumia makalioooo.........ili uweze kutambua tuko wapi katika dunia ya leo au ndugu yetu wewe mpaka Uumwe ndipo ujue umuhimu wa madaktari wako na kile wanachopaswa kupata, Kama hawana umuhimu basi mbona wenzetu wakiumwa haoo wanaruka nje ya nchi kwa matibabu zaidiiiiiiiiii leo tunapozungumzia hoja ya waganga wetu mmoja wa viongozi wabovu wanaosababisha hali hii ngumu kwetu sisi na wataalamu wetu wanaoangalia Afya zetu yupo Ujerumani kwa matibabu je unalijua hilo?? hiyo fedha ya kwenda huko kaipata wapi kama sio kodi yetu?????????? je unalijua hilo ?? ni lipi kosa kukaa kimya bila kutatua tatizo lililopo mbele yetu au kukosoa neno alilolitamka mama Bisimba kwa kumwambia kiongozi wake wa nchi au na wewe ni miongoni mwa wale washauri wabovu wa rais wa Tanzania????????? hata kama pengine hufiki pale Ikulu unaungana na uozo ulio mbele yako kama huna la kuandika ni vyema ukakaa kimya hakuna atakaye kulaumu. Mama Bisimba Aluta Continua...........endelea uwaamshe wtz ambao bado wanaona wako usingizini hakuna kosa ni wepesi kukosoa kwenye ukurasa kama huu lakini usiwaambie twende kuuliza kulikoni watakuacha pale Jangwani hawavuki hata daraja mfano ndogo unauona hata kinachogusa mwili wake bado mtu anatetea makosa. mujwahuzia
 
Pamoja na kujua kuwa HELLEN KIJO BISIMBA ni Mkurugenzi wa Kituo cha haki za binadamu , Kauli zake za hivi karibuni kuhusiana na mgomo wa Madaktari zimenifanya nisiishie kumjua kwa wadhifa huo . Nanukuu kauli zake “NAMTAKA RAIS KIKWETE AWAFUKUZE KAZI WAZIRI WA AFYA NA NAIBU WAZIRI WAKE LUCY NKYA” aidha NAWATAKA SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA WATNZANIA ANNE MAKINDA NA NAIBU WAKE JOB NDUGHAI WAWAOMBE MSAMAHA WATANZANIA “
Je Nguvu ya Mama huyu inatokana na moja kati ya haya yafuatayo?

  • Ni Mkurugengi wa haki za binadamu nchini?
  • Ni kwa sababu anataka kuonesha wahisani kuwa pesa wanazowapa hazipotei?
  • Au Mama ana mambo binafsi nje ya kazi dhidi ya Waziri wa afya na naibu wake maana naye ni binadamu na ni mwanamke na inawekana kabisa kuna wataki amEikosa haki yake ya msingi kama binadamu na labda mmoja kati ya viongozi hawa wawili ndiye chanzo na akaamua kutumia nafasi hiyo kuutuliza moyo wake?

Mimi naamini kwa Msomi na hasa Mwanasheria kama BISIMBA ambaye siyo mwanasiasa manake mwanasiasa siyo lazima awe amekwenda shule asingeweza kutumia neno “NAMTAKA” kwa viongozi wa ngazi ya juu kama Rais au SPIKA.
Nawasilisha.

Kama mtanzania na mlipa kodi sisi wote ni waajiri wa wanasiasa wote na rais. Tunapaswa kulipwa huduma stahili na hawa waajiriwa wetu. Hellen anatoa message kwa watanzania wote kuwa "we (wananchi) we are all right holders and the state is nothing else but duty bearers"
Wote tunatakiwa tuelewe maendeleo ni haki yetu na siyo fadhila toka serikalini kwa sababu tumeyalipia. Zile kauli za "Tunaomba" rais au mawaziri nk ZIFE na kushika nafasi "Tunataka/Tunadai". Hellen ahsante kwa kutumbusha kutumia kauli muafaka "Ninamtaka".
 
You are quite correct AshaDii, Hellen Kijo Bisimba amevuka mipaka ya uhuru kwa kujieleza kwa kumtamkia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kusema NAMTAKA! Hicho kivuli cha NGO anachokitumia akumbuke amepewa kwa niaba ya huyohuyo anayemshurutisha.
Nafikiri wote muende mkajifunze maana ya neno respect. Mkajifunze vile vile majukumu ya serikali kwa watu wake. Nyie wote ndio mnaowafanya wanasiasa wakawa "MABWANA" kwa raia waliowachagua badala ya kinyume chake. Hatutaweza kuwa na demokrasia ya kweli kufikiri kwa namna yenu.
We the citizen (tax payers) we have the right to demand and not to request and the state has an obligation to fullfill our rights (not privileges). Neno ninamtaka ni neno la kudai (demand). siyo tusi hata kidogo.
Jamani tuache uchonganishi huyu helen anafahamu sheria na utawala wa kisheria.
 
Jk angekuwa kama kagame tusingesikia kauli hizo kagame si kiongozi wa kulea migomo.

Na nchi yake ameboresha kila sekta/huduma muhimu,amepunguza kasi ya umaskini kwa asilimia kubwa na uchumi wake unakua kwa kasi ya ajabu,amewaunganisha Wanyarwanda wote na kua kitu kimoja,sasa migomo ya nini wakati nchi inasonga in a right direction?
 
Nafikiri wote muende mkajifunze maana ya neno respect. Mkajifunze vile vile majukumu ya serikali kwa watu wake. Nyie wote ndio mnaowafanya wanasiasa wakawa "MABWANA" kwa raia waliowachagua badala ya kinyume chake. Hatutaweza kuwa na demokrasia ya kweli kufikiri kwa namna yenu.
We the citizen (tax payers) we have the right to demand and not to request and the state has an obligation to fullfill our rights (not privileges). Neno ninamtaka ni neno la kudai (demand). siyo tusi hata kidogo.
Jamani tuache uchonganishi huyu helen anafahamu sheria na utawala wa kisheria.

Matamshi hayo yanatumika sana kwa nchi ambazo wananchi wanaelewa haki zao za msingi!mfano Uk,Us na hata majirani zetu Kenya uwa wanawataka viongozi kufanya hivi au vile,uwa hawawaombi
 
Kama nakumbuka sawasawa kuna wakati nilisoma kuwa Mama Hellen Kijo Bisimba ni mzaliwa wa Upareni na kwa hiyo ni mpare.Ila suala la kabila sio uhimu bali tuzingatie anayoyafanya kama ana dhamira nzuri au mbaya ?
 
Mleta uzi unaonekana kama ni usalama wa Taifa uliyechoka kifikra umebaki na mbinu za kizamani na uliyelelewa katika nidhamu ya uwoga hasa ukizingatia elimu yako ni ya kuungaunga. Ukweli umebaki wananchi hawewezi kuiomba serekali itekeleze matakwa yao zaidi ya kuitaka. Wananchi wanasababu gani ya kuomba haki yao na kwanini serekali iombwe haki ya wananchi. Hii ya kuiomba serekali ndio tumejikuta hakuna uwajibakaji bali viongozi wa serekali wanadhani kuwahudumia wananchi ni hisani. Na kwataarifa yako wewe tunajua uko serekalini, na ni mmoja wa watendaji wabovu na kuendeleza ukiritimba wa kipumbavu na kuishia kutoa mbinu za kichovu zilizoishia kutuletea umaskini watanzania huku mkiendeleza kauli za kwamba taifa letu bado changa.
 
Usimfundishe nidhamu ya woga, huyo aliyemtaka asimamie haki ya wananchi yuko kwa niaba ya wananchi na wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho. Kama wewe umezoea kujipendekeza ili ulishe tumbo lako kwakuwa hujui haki zako na hao unaojipendekeza kwao wamelewe madaraka si Bi Kijo. Bi Kijo anajua haki zake na anajua wajibu wa Rais, na rais si Mungu. Kwa taarifa yako hata rais akiangalia ulichoandika na anachokitaka bi Kijo anajua kabisa ki wajibu na kisheria bi Kijo ndio yuko sawa labda kama hana utashi wa kutekeleza haki.
 
Kwanza kabisa hakuna nchi inayoitwa "Lwanda".
Pia ningependa nikujulishe na kukuhakikishia 101% kuwa huyu mama, Dr. H. K. Bisimba ni mTanzania, amezaliwa Tanzania na ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro. Wazazi wake ni waTanzania sasa sijajua uraia mwingine unaouongelea unatokana na nini. Namfahamu kwa ukaribu sana; ni mwanaharakati wa kweli kama wanaharakati wengine na ni mtetezi wa haki za binadamu ambacho naamini ndio kazi yake katika ofisi aliyopo sasa. Kwa dondoo tu, "Kijo" ni ubini wake kabla hajaolewa na Bisimba ni baada ya kuolewa, i.e. jina la mumewe.
alaaa kumbe wa kule kule na wa chama kile kile,ndio maana kashubalia.pumbaf....
 
Back
Top Bottom