Hekaya za viwanja vya Gezaulole

Kwa habari nlizonazo mimi ni kwamba fomu zilizotolewa ni 2800 na plot zilizopo ni 700 tu...ratio itakuwa ni 1:4 na fomu hizi ziliisha tangu jana mjira ya saa tano asubuhi. Watu walikuwa wengi sana ukilinganisha na idadi ya fomu zilizokuwa zimeandaliwa sasa kama ilikuwa tumepanga foleni ya masalia ya viwanjwa walivyokwisha gawana watakuwa wametuumiza sana na pia kutupotezea muda wetu. Km habari hizi ni za kweli basi taifa letu linapotea maana ni km vile walikuwa wanatu enjoy tu. Pia ratio ya mgao haitakuwa km ninavyodhani.
Viwanja ni vyao wenyewe, sie tumeenda kuchukuwa form na tumeambiwa zimeisha, sasa wewe fikiria form zimeanza kuuzwa jana na zimeisha jana hiyo hiyo, jamani hii imawezekana. Si bora wasingetangaza tu tujue viwanja vimeuzwa kisirisiri. Hao waliobahatika kupata form zenyewe sidhani kama watapata hivyo viwanja.
 
jamani manispaa temeke wametangaza viwanja 2800, watu waanze kujaza form tangu tarehe 30 may mpaka tar 3 june, jana ndio siku ya kwanza, saa saba wanasema hakuna couponi zitakuja baadaye. Leo asubuhi watu wanaambiwa viwanja vimeisha na eti kuna watu walishajiandikisha tangu zamani na ndio wamepewa priority. Sasa kwa nini walitangaza?
Hao waliojiandikisha walijiandikisha kwa misingi ipi? Si kuna harufu ya ufisadi hapo?

yaani mama yuva jana nimepatwa na hasira isiyomithilika, ujinga mkubwa, wizi, udanganyifu, kupotezeana muda, wizi na ufisadi mtupu. Hakuna lolote la maana, wanajua walichokifanya. Jana naongea na baadhi ya watu wananiambia kuna jamaa zao walishachukua form 2 weeks before walichokuja kufanya ni kukamilisha zoezi.
Jamani mamlak husuka ziko wapi katika kukabiliana na huu uchafu wa kuchezea wananchi? Ni lini haya yatakwisha? Na je inakuwaje mtu mmoja nakuja kuchukua form za viwanja 5 mpaka 10 wakati kuna wananchi wanahitaji kiwanja kimoja tu kwa ajili ya makazi? Inakuwaje muda wa kutoa majina na kulipia gharama za upimazi ziwe katika kipindi cha siku 14 tu, je huyo muuza mahindi na maembe ataweza kumudu kulipia?
Pccb wapo wapi, wanafanya nini......hii mamlaka nadhani inapaswa kufutiliwa mbali kwani sioni kipi wanachokifanya zaidi ya kutumia kodi za wananchi bure.
 
Ratio wanasema 1:5 kwa kila iliyouzwa jana, saa tano zilikuwa zimeisha kutimiza taratibu pro-rata itatumika ktk allotment na technical no who itaendelea kufanya kazi. Kiukweli demand ni kubwa kuliko idadi ya viwanja
 
Mimi ninachoshangaa ni kuona serikali yetu inapenda kufanya kila kitu kiwe ni shida hata vile ambavyo vimo ndani ya uwezo wake...watanzania hatuna shida ya ardhi, tuna ardhi kubwa sana. Hivi serikali (manispaa/halmashauri) zinashindwa nini kupima viwanja vingi hata kupita mahitaji ya wananchi na hivyo kuiua biashara ya viwanja inayofanywa na baadhi ya watumishi wa ardhi na kusababisha kero na malalamiko kwa wananchi.
Kwa nini idara ya ardhi ktk kila manispaa/halmashauri wasiwekewe malengo ya kila mwaka ya kupima viwanja vya kutosha wakati kuna wafanyakazi walioajiriwa na wanalipwa kwa kazi hiyo?
Wanalipwa na pesa ya wanachi ili wapime viwanja kwa ajili ya mwananchi na sio wao na vigogo..hii inatuuma sana sisi wananchi walalahoi kwa kutusaliti..lakini kilio chetu hiki ipo siku kitafika kwa MWENYE KUIUMBA MBINGU NA ARDHI HII wanayotufanyia biashara haramu..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom