Hekaya za viwanja vya Gezaulole

mama yuva

JF-Expert Member
Aug 3, 2010
226
47
Jamani manispaa Temeke wametangaza viwanja 2800, watu waanze kujaza form tangu tarehe 30 may mpaka tar 3 june, jana ndio siku ya kwanza, saa saba wanasema hakuna couponi zitakuja baadaye. leo asubuhi watu wanaambiwa viwanja vimeisha na eti kuna watu walishajiandikisha tangu zamani na ndio wamepewa priority. sasa kwa nini walitangaza?
hao waliojiandikisha walijiandikisha kwa misingi ipi? si kuna harufu ya UFISADI hapo?
 
Are you a complete amateur at sarakasi kwenye ardhi katika nchi yetu? Utakuta hapo kwanza ni wafanyakazi wa ardhi kwanza wanajigawia
 
Habari za kuaminika kutoka kwa mtu wa ardhi ninayemfahamu ni kwamba, viwanja hivyo ni kwa ajili yao wafanyakazi wa ardhi. Fomu walizotoa ni danganya toto. Kigamboni eneo la KISOTA waliuziana kwa laki tano na sasa wanauza kiwanja kuanzia milioni 20.
 
Ni kweli ni mradi wa kifisadi maana sisi tuko jirani kabisa hapa tumewatuma vijana wakatuchukulie form wameambiwa zimeisha na may be eti huyo dada anasema kama tuko serios tunahitaji tutoe Laki moja extra ili tupatiwe form. Jamani huu ni ufisadi uliopindukia Mama Tibaijua Waziri wa Ardhi kazi unayo mama!!!!
 
Wanasema kuna watu wamenunua fomu 50! Sasa sielewi hao watu wanaenda kuzifanyia nini!
 
Huu mradi ni kama wa Kinyerezi yote ni wizi mtupu huu ndia wakati muafaka wa kuwawajibisha wakurugenzi na kuwafukuzia mbali kwani ndio wanaoleta mchezo mchafu kwenye zoezi zima
 
Viwanja vilishagawiwa zamani na waliopewa kati yao ni wabunge wetu ila walitaka kukamilisha taratibu tu. Nchi hii inakoelekea maskini hana chake tena.
 
ndio maan watu wanajichukulia ardhi

unakuta wameshauziana na baadae wanakuja kutulangua

mtu mwenye akili anaona kabisa hujuma hii, na kibaya zaidi tabia hii ndio chanzo cha maeneo yote yaliyopimwa kukosa kasi ya ujenzi... wanaonunua ni haohao
 
Subilini baadae mtaambiwa walio chukua fomu ni 12000 na viwanja vipo 2800 watafanya bahati nasibu.
 
JF members!
Is there anything whch can be done on this!!
This is very serious issue! inauma sana

Kama serikali inatoa viwanja kwa wananchi kwa bei ya serikali, halafu watu wa Ardhi wanajiuzia ili baadae waviuze kwa Faida, Huu ni ufisadi mkubwa kuliko ule wa akina Rostam na Lowasa.

Nani wa kumuandikia Barua hapa? Hili suala nafikiri ni Nyeti sana, Na lingefaa kujadiliwa Bungeni, Lakini wabunge wetu ndo hivyo tena, Sijui Bungeni wanafuata Nini? (hivi ni nani ameshawahi sikia Rostam akichangia mada Bungeni?)

Lets fight this out! La sivyo tutabakia kulalama huku JF huku wahusika wakiingia humu humu na hizi Hidden ID na Kujaribu Kuonesha How a thread like this should be taken as a crap and be trushed!!!

Lets stand up for our rights please!!!
 
Form za viwanja ziliisha jana mchana na wamesema kama unataka inabidi usubiri mpk mwezi wa nane wakishapima shamba la NAFCO (Manji) hapo wanategemea kupima na kupata viwanja elfu 5
 
Huu mradi ni kama wa Kinyerezi yote ni wizi mtupu huu ndia wakati muafaka wa kuwawajibisha wakurugenzi na kuwafukuzia mbali kwani ndio wanaoleta mchezo mchafu kwenye zoezi zima

kwahiyo afukuziwe mbali abaki na viwanja vyake? I say no. waturidishie viwanja vyetu!!

Hivi si kuna Data base ya umiliki wa Viwanja? kama ipo, Tunaomba an Indepedent auditor apate majina ya watu waliowahi kufanya kazi ardhi for the last 20 yrs! from here angalie Historia ya umiliki wa viwanja, japokua najua wengine wanatumia majina ya Close relatives or friend katika ufisadi huu!!

Hivi mpaka tuvae mabomu tijilipue kwenye hayo maofisi yaliyojaa uozo ndio mjue tumeyachoka na watendaji wake wote!
 
Form za viwanja ziliisha jana mchana na wamesema kama unataka inabidi usubiri mpk mwezi wa nane wakishapima shamba la NAFCO (Manji) hapo wanategemea kupima na kupata viwanja elfu 5

Mwezi wa nane pia tutakwenda na kuambiwa yale yale , unadhani story itabadilika? kama ni hivyo si wapokee form watakaobaki wawafikirie august?
 
Kwa habari nlizonazo mimi ni kwamba fomu zilizotolewa ni 2800 na plot zilizopo ni 700 tu...ratio itakuwa ni 1:4 na fomu hizi ziliisha tangu jana mjira ya saa tano asubuhi. Watu walikuwa wengi sana ukilinganisha na idadi ya fomu zilizokuwa zimeandaliwa sasa kama ilikuwa tumepanga foleni ya masalia ya viwanjwa walivyokwisha gawana watakuwa wametuumiza sana na pia kutupotezea muda wetu. Km habari hizi ni za kweli basi taifa letu linapotea maana ni km vile walikuwa wanatu enjoy tu. Pia ratio ya mgao haitakuwa km ninavyodhani.
 
TULIENDA TUKAKUTA THE SAME STORY...nilichoshukuru walisema si vizuri kuchukua pesa wakati hutapata
 
Back
Top Bottom