Mpasuajipu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 836
- 49
Katika mwaka mmoja, Abunuwasi aliamua kuwa mfugaji mbuzi. Alinunua mbuzi na akanza kufuga na huku akiwa na tamaa ya kumuongezea kipato chake pindi tu mbuzi huyo atapoanza kuzaa watoto, naye atawafuga hadi wawe wengi na kuwa tajiri mji mzima kwa mbuzi wake hao.
Siku moja Abunuasi akipokuwa anampeleka malishoni mbuzi wake njiani alikikuta kiatu kimoja kizuri sana kati kati ya njia. Alisimama na akakingalia na kilimpendeza na alisema "kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu" alitafuta kiatu chengine pembezoni mwa ile njia hakukiona. Akaona hakina maana kukichukua kwani hawezi kuvaa kiatu kimoja.
Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na akakiwacha kile kiatu pale pale. Aliposonga mbele kidogo akakikuta kiatu chengine kama kile ambacho kilikuwa ni cha mguu mwengine wa kile cha mwanzo. Abunuasi alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo na kwa sasa vingelikuwa tayari vishatimia pea moja. Ndipo alipoamua kumfunga mbuzi wake pembeni ya njia na akakiweka kiatu kile pale pale alipomfunga mbuzi ili arudi akakichukuwe kiatu kile cha mwanzo.
Aliporudi pale kilipokuwepo kiatu cha mwanzo hakukikuta tena kiatu kile, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akaona kuwa ametokea mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake. Nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Ikawa amemkosa mbuzi na pia viatu hakuvikuta, Abunuasi ndoto zake zote za utajiri ziliruka na akabaki na umasikini wake kwa ubaya wa tamaa zake.
Hapo nilipiga mstari: Mafisadi inabidi tuwadhibiti sasa, la sivyo tukisema tutawarudia baadaye tutakosa kila kitu!