Heche,prof safari wawasihi wanadar-es-salaam kubadilika

USTAADHI

JF-Expert Member
May 10, 2011
1,516
136
Katika eneo la keko leo katika wilaya ya Temeke, chadema kanda maalumu ya Dar es salaam wamefanikiwa kuendelea na kampeni ya ondoa ccm Dar mkutano uliokuwa umesheheni vijana mbali mbali waliojitambulisha kwa vyeo na majina pia hata kuhutubia huku wahutubiaji wakiwa bwn john heche,mwkt wa bavicha taifa,pia ndg henry kileo katibu wa mkoa kinondoni pia prof safari wakili mahiri na mjumbe wa kamati kuu katika mkutano huu Ujumbe umejikita katika kuwabadilisha watu wa Dar es salaam kuwa chachu ya mabadiliko km majiji mengine walivyofanya ikiwemo Nairobi,bulawayo,kinshasha na kwingineko kwani ndiyo walio karibu na vyombo vya habari na mitandao' katika mkutano huo pia kadi zaidi ya 175 za chama zimeuzwa
 
Wapigeni nondo za uhakika hao watu wa Dar,sisi Mwanza kazi ilishaisha ndiyo maana hata watu hawana habari na besidei ya magamba,mpaka imebidi wawalazimishe wafanya biashara waliopanga kwenye vibanda vya uwanja wa Kirumba kuvipakaa rangi za kijani kwa gharama zao na wengi wamegoma na kuamua kufunga biashara zao mpaka sherehe hizo zipite.
 
Aluta continua wanacdm kwan hata si vijana wa kusoma 2po nyuma kwenye hizi harakati.
 
Mijana mchana mida ya saa tisa hivi nimekuta gari ya chadema ikiwa na bendera na vipaza sauti juu pale kariakoo barabara ya uhuru kadi na calender zilikuwa zikigawiwa pale kama kawa kweli chadema inawabunifu yaani wameamua kuwafuata watu waliko hukohuko makazini kwao kweli viongozi wa Chadema ni majembe,Hongera Mnyika na Dr Slaa kwa program hiyo.
 
Hao kina safari na mwenzake ni njaa tu zinawasubua,hawana lolote.Safari si alikimbia CUF baada ya kuukosa uenyekiti ngoja na hapo ataujaribu akiukosa anakimbilia TLP kwa Mtaalam
 
kalenda kwako ndio ubunifu?
 
mambo yanaendeshwa kisayansi,hakuna kukurupuka kwa kuwapakia kwenye malori kutoka vijijini,vijana ndo chachu ya mabadiliko ya kweli kokote kule duniani.big up sana Mh. Heche hiyo ndo kazi ya vijana
 
Hao kina safari na mwenzake ni njaa tu zinawasubua,hawana lolote.Safari si alikimbia CUF baada ya kuukosa uenyekiti ngoja na hapo ataujaribu akiukosa anakimbilia TLP kwa Mtaalam
nenda kwenye hoja acha kujadili mtu huuu ni upupu wa magamba au ndo unagoma hata kukubali ukweli? kwani safari alikosea kuja CHADEMA?
 
Kwanini uataje majiji menmgine ya Afrika kama Nairobi, Bulawayo Kinshasa?

Majiji ya humu humu Tanzania tayari yalishaanza tangia 2010, kama vile Mwanza, Mbeya
Arusha, Moshi etc. Mkakati for 2015 ni kuwafukuza kabisa CCM mijini. DSM msituangushe
please.
 
Dar inabidi tufanye kazi ya ziada, watu wanadanganyika sana na furana na 5000. Jiji linatakiwa kuwa mfano ila sisi tunawaangusha majiji mengine kama mbeya, arusha na mwanza

Tunahitaji kuamka sasa wakati umefika wa kuwaonyesha CCM kuwa watanzania wanaweza kama wanataka madaraka wapeleke mafisadi wote gerezani
 
Back
Top Bottom