nge utamaduni wa kumhukumu mtu kulingana na perfomance yake.Tujenge utamaduni wa kuangalia mtu ana vision gani kwenye community...Tuache majungu.Kamanda Mwita Waitara anatukanwa hapa hapa na watu waliokuwa wanaunga mkono mapambano aliyoongoza Igunga.Hebu tujenge chama tuache ku-promote mgawanyiko.Kamanda Ester Matiko anafanya kazi nzito,kila mtu anakumbuka harakati za nyamongo.
Kitu kingine cha muhimu,tuzingatie dhana ya uwajibikaji.Ukishutumiwa jibu hoja badala ya kulilia BAVICHA,UVCCM,CUF nk. Hizi rhetorics zinendekeza mduara wa uzembe na kukwepa wajibu wa kisiasa.Tuwe mfano halisi wa mabadiliko tuyatakyo
Tafadhali wakuu hebu tujenge chama,huu ugonjwa wa kutokujiamini kisiasa unaleta matatizo makubwa kiutendaji.
NB: JF inashushwa thamani na wimbi la Rumour mongers lililoingia,tusikubali kuwa trapped sasa kwenye majungu
Balance story Heche na Waitara wote wametukanwa hapa ,ukiangalia mleta thread ni kwamba ameweka mazingira ya kuwaingiza hawa vijana wawili wenye nia njema kwenye chama chao kuleta mgogoro la kuwafanya ni wao kutokufuata ushabiki wa mashabiki wao na wabaya wao ambao kwao ni cherekochereko wakiona nyuzi kama hizi, wajitahidi kuupuza stori hizi hata kama zina ukweli,uongo au uzushi lakini waangalie yale waliyoyapanga kukujinga chama chao manake mambo mangapi ya mitandaoni utakuja kuyajibu yaani mtu huna kazi zako zingine
Siku za karibuni umezuka mtindo wa kuvuana nguo kwa wanachadema hapa , sijui kama ni wanachadema kweli au ni watu wa fake IDs na Fake uanachama hii ni cyber space mtu anaweza kutengeneza scenerio tuu ,
Kwa maoni yangu nadhani wafuasi na wanachama wachukulie kwamba hiyo ndio changamoto chama kinapokua kwa kasi ya ajabu ,haya yote yatajitokeza , wengine watataka hili liwe lao,wengine watadharau wengine,wengine watajiona wao ni bora kuliko wengine,si ajabu ni silka ya kibinadamu mwisho wa yote lazima kuwe na makubaliano na zaidi kikubwa ni watu kutokuangalia allegations za mitandaoni,watu wahangaike pale kunapokuwa na facts na hizo zizungumzwe kati ya wanaotuhumiana au kwenye vikao husika
Lakini haya ya hapa ya watu kuattack personalities za watu umekuwa mtindo mbovu,kutaka kucheleweshana tuu kwenye mabadiliko na ukombozi wa nchi yetu