NZURI PESA
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 5,959
- 2,938
Wana jf naomba tukumbushane kwa wale tuliokuwepo enzi hizo, na kwa faida ya wanetu wa sasa, kinachonifanya nisisahau kikubwa kuliko vyote
kuna kanga zilikuwa zinaitwa teleza za polister nilikuwa nimembebea mdogo wangu nikaenda kisimani wakati najitwisha ndoo nguo ikafunguka mtoto akatumbukia kisimani, kingine
vita vya amini,
kukamatwa kwa jua,
Unga wa yanga
Wenzangu mnakumbuka nini?
1.Unga wa yanga
2.Sabuni ya mawingu
3.Kitambaa cha madurufu a.k.a MAFAFA
Vitenge vyaMawingu a.k.a BATIK
Maduka ya NMC na RTC,Ukitaka SEMBE LA YANGA kg1 UNALAZIMISHWA KUNUNUA NA PAKET YA SIGARA hata kama SI MVUTAJI.
au Sukari kg 1 na BETRI 4,hata kama REDIO HUNA.