Hebu tukumbushie tuliozaliwa miaka ya sabini na....

faizah

Member
Jun 22, 2011
62
26
Wana jf naomba tukumbushane kwa wale tuliokuwepo enzi hizo, na kwa faida ya wanetu wa sasa, kinachonifanya nisisahau kikubwa kuliko vyote
kuna kanga zilikuwa zinaitwa teleza za polister nilikuwa nimembebea mdogo wangu nikaenda kisimani wakati najitwisha ndoo nguo ikafunguka mtoto akatumbukia kisimani, kingine
vita vya amini,
kukamatwa kwa jua,
Unga wa yanga
Wenzangu mnakumbuka nini?
 
Potelo unazikumbuka? Baada ya Kokakola kupotea!

Na yule chizi mmoja aliyejenga kibanda cha makuti pale jangwani peke yake unamkumbuka?

Baadaye nikipita pale jangwani nimekuwa nasema kimoyomoyo machizi wamekuwa wengi sana siku hizi!
 
Nakumbuka buluga! Ule mchele Kama ngano kutoka USA pamoja na maziwa ya unga ya njano kabisa zaidi ya nido hii ni kwa waliokulia vijijini
 
Unakumbuka enzi zile jangwani kulikua poli simba nje nje,nyumba zilikua zinaishia lumumba tu pale sisiemu!
 
Weweeee..... naona utakuwa unaanza kuzeeka vibaya. Hiyo unayoelezea nadhani itakuwa taswila ya 59 hadi 60 .
Miaka ya 70 mbona nyumba zishaanza kusogeasogea. Bulga sawa, zilikuwapo, na mafuta ya alizeti ya bure
kutoka watu wa marekani.

Wewe kwenu mlikuwa na radiogram? Au turn-table?
Ilikuwa inabeba sahani za santuri ngapi.
 
Nakumbuka maduka ya ushirika,foleni za kupanga mawe!magari ya ugawaji yakisambaza bidhaa madukani!!
 
radio Tanzania hotuba za jkn mwanzo mwisho! Ukisikiliza radio Burundi Idhaa ya kiswahili muziki safi na salamu za wasikilizaji(wengi wakiwa watanzania) kwa wingi.

Vita vya Kagera: wananchi tunafundishwa kuchimba na kutumia mahandaki....hivi niulize kazi ya haya mashimo ilikuwa nini?
 
Nakumbuka kuangalia Sinema : Cameo, Avalon, Empire n.k. Nakumbuka maduka ya RTC; National Milling (NMC); kusafiri kwa warrant; kutumia Slide ruler; BORA SHOES; vitambaa vya tetron, krimplin, mashati ya Juliana; barozi wa nyumba 10 n.k.
 
Nakumbuka foleni kwa kila huduma. Hupati mahitaji yoyote mpaka upitie kwa balozi wa nyumba kumi.
 
Jumapili kuendesha gari mwisho saa saba mchana, zaidi ya hapo lazma uwe na kibali. TV ilikuwa TV ya znz peke yake ina ilikuwa inaonekana chenga chenga.movie ni drive in wale tuliokuwa tunakaa nje ya ukuta, ilikuwa inaitwa tiket mmbu..barabara ya migombani, basi la kamata lilikuwa linapita mpaka kule mwisho linageuza, palikuwa na bar inaitwa zena garden. Kuna siku asubuhi wanafunzi wa forozani walimtukana dereva wa basi la kamata, dereva akaamua kulipindua, mtoto wa wa mzee kiluvya akafa palepale....
 
Aise wewe na BoonaBaana mna kumbukumbu nzuri. Deti yangu ya kwanza na kabinti fulani "chuma sana" kutoka Tanga ilikuwa pale Empire. Sitakaa nisahau usiku ule. Mamake kakubali tutoke lakini kaweka sharti; Chukua na wadogo zake mwende wote. Du...Mama yule alinikomesha kwelikweli.

Jumapili kuendesha gari mwisho saa saba mchana, zaidi ya hapo lazma uwe na kibali. TV ilikuwa TV ya znz peke yake ina ilikuwa inaonekana chenga chenga.movie ni drive in wale tuliokuwa tunakaa nje ya ukuta, ilikuwa inaitwa tiket mmbu..barabara ya migombani, basi la kamata lilikuwa linapita mpaka kule mwisho linageuza, palikuwa na bar inaitwa zena garden. Kuna siku asubuhi wanafunzi wa forozani walimtukana dereva wa basi la kamata, dereva akaamua kulipindua, mtoto wa wa mzee kiluvya akafa palepale....
 
Kusafisha tiketi ya basi kwa mafuta ya break ili kudai pesa zaidi ya kiwango halisi kwa zile sehemu ambazo warranty au garimoshi haifiki
 
sie wa kusini tulikuwa na mabasi yetu maarufu TITICO na MALOLOTA, kuna wakati basi la MALOLOTA lilipotea na abiria wote kijiji cha MANDAWA RUANGWA, likaja kuonekana baadaye.
 
Duh! Nakumbuka Warrant kila mwisho wa term na marejesho ya nauli kwa kutumia mabasi kwenda na kurudi shuleni. Tanzania ilikuwa inajali sana Watoto wake. Wenzangu enzi hizo watakumbuka tulivyonyoa Push back na kuvaa "don't touch my shoes" Aisee list ni ndefu mno.
 
ah umenikumbusha jambo. usafiri wa miaka ya 70. unajua ilikuwa inachukua siku ngapi kufika dar es salaam kwa treni kutoka mwanza? au basi la relwe kutoka mbeya hadi dar? ilikuwa kichekesho nakwambia. yaani wakati mwingine mi nikisikia mtu katumia dakika 120 kutoka mwanza kuja dar kwa 540 hubakia tu mdomo wazi. kama si ufisadi nchi hii kuna vihatua imepiga

sie wa kusini tulikuwa na mabasi yetu maarufu TITICO na MALOLOTA, kuna wakati basi la MALOLOTA lilipotea na abiria wote kijiji cha MANDAWA RUANGWA, likaja kuonekana baadaye.
 
Kusafisha tiketi ya basi kwa mafuta ya break ili kudai pesa zaidi ya kiwango halisi kwa zile sehemu ambazo warranty au garimoshi haifiki

Aaah! hiyo ya kufuta ticket kwa mafuta ya break ili kuandika upya kiwango cha pesa umenikumbusha mbali sana!Ni kweli tulikuwa tunafanya hivyo,pia unatafuta na ticket nyingine inayoonyesha unatoka mji wa mbele zaidi ya ule unaotoka!.
 
kumbe ufisadi tumetoka nao mbali? du! na itakuwa hao wafutaji wa tiketi ndio haohao weshakua ma-CEO wetu. mbona shuhuli!
 
zama za club la leo shooooooooooooooooooooooooo haikuwa enzi izo kweli
Ila nina hamu na buluga!
Wapi maduka ya ushirika mnaenda kwa jina la dingi kuchukua sukari kwa foleni unaweka jiwe gari likaribia tuu unaitwa
 
  • Thanks
Reactions: ram

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom