HEBU TEMBELEA BLOG HII upate kumshauri kijana huyu

Ni kweli wanalifaa taifa kumbuka mficha ugonjwa kifo humfichua. Sisi ni kweli ni masikini sana. Ni masikini wakati tunamali asili nyingi sana zinachukuliwa huku tukiona kwasababu ya watu wasiokuwa na uchungu kama baba wa taifa.
Tutegemee kuwa masikini zaidi kama hatutabadilika na kuubadili mfumo na uongozi.
 
Ukisoma blog hii unatamani kulia!!! Ni tajiri wa rasilimali lakini masikini wa kutupwa!!!!!
 
inauma sana
kila ninapopata taarifa kama
hizi natamani ningekuwa meja genearal nipindue hii nchi peke yangu
najua wengi wenu waoga nisingetaka ushirika wenu
ni bora mara 1000 kupata jasiri mmoja apindue hii nchi
Mateso wanayopata watu ni kama wako kuzimu.
maisha wanayoisha viongozi wetu duh kwa kweli ni kitendawili
 
Nimeona suala la kuuza vitumbua hapo,mimi binafsi nimeuza sana vitumbua,i decided kufanya hvo kutokana na hal ya maisha,wakat nipo darasa la 1 na la 2,asbui natembeza vitumbua,mchana ndo muda wa darasan nazama class,lakin hata nilpokua nipo highschool,nikajikuta asbui ni lazima nisambaze vitumbua madukani,then ndo naenda shule,pesa hzo ndo zimenisomesha,tena bibi yangu ndo alijiusisha na kaz ya kuchoma vitumbua,nakumbuka alifarik kabla sijamalza elim yangu ya sec,kwa hyo wazaz na watoto wanaweza s0meshwa kwa vitumbua,maana hata shangaz yangu,ambae amelelewa na huyohuyo bibi yangu alitinga SUA kwa biashara ya vitumbua na maandazi!
 
Hiyo blog ikipata umaarufu utasikia imeanzishwa na CDM wakati hiyo ndiyo hali halisi iliyopo Bongo.
 
Dah,imenikumbusha mbali sana,...picha zote hizo ni kama mimi
reflection ya nilipotoka,ingawa huko niliwaacha wengi sana

Help us God
 
Hiyo blog ikipata umaarufu utasikia imeanzishwa na CDM wakati hiyo ndiyo hali halisi iliyopo Bongo.

Ndiyo zao,lakini mungu amesikia kilio cha watanzania,umaskini wa kutengenewa utapata ufumbuzi tunakoenda,tumwombe mungu aongeze wapiganaji wa kweli katika shamba lake,ili kila mtanzania ale na kushiba,watanzania waachane polepole na jembe la mkon,watanzania wapate umeme kama sehemu ya huduma muhimu sio anasa nk,haya yote yanawezekana baada ya kuondokana na ukoloni wa chama cha magamba
 
Dah!nimeipitia hiyo blog hizo picha zimenihuzunisha sana,halafu utawasikia wa magamba wanasema'ari mpya nguvu mpya na kasi mpya'-Ntakuja nimtwange mtu maneno bila vitendo!!?viongozi wa ccm jamani kuweni na huruma
 
Katika picha zote nimevutiwa na za kikombe! Sasa hawa viongozi wetu, wengine mabilionea, nao walipanga foleni ya kikombe. Nimecheka sana. Ama hakika ikija kwenye maradhi binadamu wote ni sawa! Pamoja na kujitibu mamtoni na kikombe wamesukumizia. Nadhani viongozi wote Tz wamepata kikombe, what I don't know wana maradhi yepi au wamekunywa kama kinga!
 
Duh bora umenifungua macho na hi blogu manake itanisevu sana kwenye ishu flani. Haya ndio mambo ya kuweka kwenye blogu, hali halisi ya nchi hii. Sisi ni maskini hilo halifichi. Kumbuka silimia 70% ya watanzania wanaishi maisha haya, jamaa ana akili sana na anaona mbali.

Cha kushangaza ataambiwa anachochea serikali kwa kuikosoa na kutoona mazuri inayoyafanya.
 
Dah!nimeipitia hiyo blog hizo picha zimenihuzunisha sana,halafu utawasikia wa magamba wanasema'ari mpya nguvu mpya na kasi mpya'-Ntakuja nimtwange mtu maneno bila vitendo!!?viongozi wa ccm jamani kuweni na huruma

KATIKA PICHA ZOTE HII KALI
ingelikuwa mimi ningelivunja nikauze tofali zake!!!!!

ari_mpya_nguvu_mpya.jpg
 
Yaani hiyo blogu imenitoa machozi jamani. Hata sina cha kusema.
 
Back
Top Bottom