Hebu someni utafiti huu!

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Tafiti nyingi zilizofanywa kuhusiana na upotezaji muda unafanywa na waajiriwa ni kwamba, wafanyakazi maofisini huwa wanapoteza saa tatu kila siku katika kufanya mambo ambayo hayana maana kwa mwajiri au kwa kazi zao. Kwa wale ambao wan mitandao ya intenet maofisini mwao na wanaweza kuiangalia kwa kadiri wanavyopenda hutumia dakika 54 kwa siku kuangalia mitandao hiyo.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 18 kila siku kuchungulia madirishani. Hata wale ambao viti na meza zao katikati ya ofisi, huwa wanasimama na kwenda kuchungulia madirishani mara kwa mara. Kwa wastani hutumia dakika 18 kutwa.

Watumishi wa maofisini hutumia dakika 14 kwa kwenda kujisaidia au kwa wanawake kwenda kujipamba au kujipodoa upya bafuni au vyooni. Ile nenda rudi ya kujisaidia au kujipodoa upya huchukua wastani wa dakika 14 kila siku. Kumbuka, kuna watu hujisaidia haja kubwa hata kwa dakika kumi.

Watumishi wa maofisini yaani wale ambao hukaa ofisini, hutumia dakika 35 kila siku kupiga soga zisizohusiana na kazi na pengine zisizo na maan sana. Soga zinazohusu mpira, siasa, ufuska, majungu na umbeya mwingine hutawala.

Halafu hutumia dakika 17 katika kunywa kahawa au chai na pengine soda. Inaweza kuwa wananywea kwenye mighahawa ya kazini au pale ofisini walipo. Wengine wakati wakiwa wanakunywa kahawa au chai hawagusi kazi kabisa.

Siku hizi maofisini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuteka mawazo au akili ya watumishi. Vitu kama mitandao, viriba vya chai na kahawa vya kujichotea na mengine mengi yanafanya kujikuta mtumishi ameacha kazi na kuingia katika kitu kingine.

Lakini watumishi wengi wa maofisini hasa wale ambao wanatumia muda mwingi ofisini,inadaiwa kwamba, hawafanyi mazoezi. Hii inasababisha watumishi wengi wa kazi za aina hiyo kufa au kustaafu mapema kutokana na ubovu wa afya.

 
haha hii kweli kali, hiyo ya kuchungulia madirishani imeniacha hoi na ni kweli kabisa ofisi yetu ipo barabarani basi ikisikika tu breki kali, watu wanamwagika madirishani kuchungulia, mkulu akipita zile siren watu madirishani, story za mpira ndo balaa, mademu hahaaa kweli aliyefanya utafiti kapatia
 
Pana ukweli fulani, na kwa baadhi ya ofisi hali ni mbaya zaidi ya huo muda uliostate hapo!
Thanks.
 
Watumishi wa maofisini hutumia dakika 14 kwa kwenda kujisaidia au kwa wanawake kwenda kujipamba au kujipodoa upya bafuni au vyooni.
hahahahahahahaha!
 
Hakuna mashine/ closed system iliyo 100% efficient, it is against the laws of physics, particularly the second law of thermodynamics and the entire concept of entropy.

The best one can do is reduce inefficiency.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom