Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,709
Tangu tumezaliwa tumesikia neno UPENDO,mimi binafsi wazazi wala shule sikuwahi kuambiwa maana ya hili neno!Nilikuja kulitafuta mwenyewe!Nakumbuka kwenye mafundisho ya dini tulikua tunaambiwa tupendane,nyumbani hivyohivyo.Nilipokua nikajua kuna kumpenda mwanamke,hawa walionieleza kuhusu upendo hawakuwahi kunifafanulia,nikajiuliza kuna tofauti kati ya kumpenda mama yangu na jirani yangu pia vipi kuhusu mwanamke?Nilibaki mtupu!Lakini niliamua kutafuta maana na nimepata tafsiri hii;Upendo ni kumkubali mtu bila masharti.Yaani kama ni mwanao sio mpaka afaulu mtihani ndo apendwe,kama ni jirani rio mpaka awe na pesa ndo apendwe,upendo ni kutoa tu bila kujali unaempenda anakurudishia nini,yaani wewe ni kutoa tu,na ukiwa hivi hautaona shida kuishi na mke/mume mkorofi.ANGALIZO,kwenye ndoa ni hatari kuishi na mtu mwenye tabia za hatari kama kupiga,kufuja,kudhalilisha n.k,hapa unatakiwa usitishe haya mahusiano,kufanya hivi haimaanishi unamchukia.Unaweza ukatengana nae lakini mkawa pamoja kwenye mambo mengine.Sasa kama niko sahihi,kuna upendo siku hizi?Na kama siko sahihi,tafsiri yako ni muhimu hapa,tuambie......