Hebu sikieni ninavyowaza!!

LD

JF-Expert Member
Aug 19, 2010
3,014
574
Mwenzenu nilivunjwa moyo miaka miwili iliyopita, Tangu moyo ulivyovunjika nimekuwa nikimuomba Mungu aniponye na nina Imani ameniponya kabisa, manake najiona sina kinyongo, wala uchungu na huyo heart breaker, na ninachomshukuru Mungu zaidi nina furaha na Amani, na maisha yanaendelea vizuri.

Pamoja na hivo ninamshukuru Mungu kwa sababu amenisamehe dhambi niliyokuwa nimeitenda, kwa sababu nilijidai ninampenda sana huyo mtu kuliko hata Mungu, nikampa vyote, nafsi, roho na mwili. Wakati mwingine hata muda wa kwenda kuabudu ulipungua kwa kumpa huyo heart breaker muda mwingi zaidi.

Baada ya tukio hilo,niliamua kujipa likizo ya kumpenda mwanaume, yani nikaziba madirisha yote ya kumkaribisha mwanaume moyoni mwangu.
Siwachukii lakini nimejipa likizo kwa muda wa miaka mitano hivi, na sasa huu ni mwaka wa pili, ina maana bado miaka mitatu.

Je uamuzi wangu wa kujipa likizo ni sahihi?
Najiona ninaweza kuendelea na likizo hadi miaka mitatu iliyobakia iishe, je ni kweli au
naidanganya nafsi yangu.

Angalizo Marufuku kunitania Broken Heart!! Umesikia GY, Asprin, TF, Askofu na Teamo T, bila kumsahau Bigirita. Mjukuu mtiifu umesikia!! na wewe St. RR.
 
mi naona unajidanganya sababu kwa jinsi nnavyojua lov inakuja yenyewe labda ujiweke mbali na watu, ninacho kiona hujaonana na mtu atakayeteka moyo wako, ukimuona unasisimka, ukiongea nae unapata raha, hapo ndipo utakapo amini miaka 3 ni kifungo cha maisha.
 
hata mimi ilishawahi ntokea nikajipa likizo ya mwaka kutotaka kumsikiliza mwanaume.Hiyo yako ni ndefu mno maisha mafupi ya nini ujikoseshe raha?
nadhani hiyo miwili imetosha sasa anza kusikiliza kidogokidogo.

ANGALIZO:usimkaribie mtu asiye na hofu ya mungu, kuna wakaka kibao wanakwaya/wainjilisti makanisani kama vipi anza kujifua kuima nadhani hili halitamchukiza MUNGU manake unamtaka kondoo wake kwa nia safi.
 
Asante Subzero, kwa hiyo unanishauri niendelee na likizo mpaka hiyo hapo kwenye red itakapotokea siyo?
 
hata mimi ilishawahi ntokea nikajipa likizo ya mwaka kutotaka kumsikiliza mwanaume.Hiyo yako ni ndefu mno maisha mafupi ya nini ujikoseshe raha?
nadhani hiyo miwili imetosha sasa anza kusikiliza kidogokidogo.

ANGALIZO:usimkaribie mtu asiye na hofu ya mungu, kuna wakaka kibao wanakwaya/wainjilisti makanisani kama vipi anza kujifua kuima nadhani hili halitamchukiza MUNGU manake unamtaka kondoo wake kwa nia safi.

Asante Martina, kumbe inwezekana kwenda likizo ukiamua, mwaka mmoja nayo nahisi kwa watu wengine ni mrefu sana.
Hao wakaka hapo bwana duuuuuuu!!! Au acha nisiseme kitu.
 
Mshiki nina swali Dogo tu kwako!! Hivi baada ya hiyo miaka Mitano then utaamua kupenda tena kama zamani? utapenda kidogo? au utafanyaje?
Nasubiri jibu ili nije na maswali mengine!!
 
hehehe let me reserve my comment kwenye hiyo red!!
 
Naanza kumwona anakua st. theresa.....just 3yrs ahead...!
 
Asante Martina, kumbe inwezekana kwenda likizo ukiamua, mwaka mmoja nayo nahisi kwa watu wengine ni mrefu sana.
Hao wakaka hapo bwana duuuuuuu!!! Au acha nisiseme kitu.
usijichanganye kwa wapiga vinanda, au kwaya masters kwani hao ni wanamziki kama walivyowengine ha matendo yao hayana significant difference.Kumbe unawajua eeh
 
kujipa likizo ni kujiongezea stress....

it's like a woman whose kid dies JUST AFTER giving birth,halafu ''akajipa likizo'' ya miaka kadhaa ya kutokuwa na mtoto....

i'm telling you my dear.....UNAPATA MADHARA MAKUBWA SANA KISAOKOLOJIA
 
Kila kitu ni uamuzi LD, kama umeamua utaweza, miaka mitano siyo mingi ukiwa unaishi na amani....................
fuata nafsi yako. kupumzika hasa baada ya kuvunjika moyo ni kuzuri sana ingawa wadada wengi hawataki kufanya hivyo, na matokeo yake unajikuta unahama kwa mkaka mmoja baada ya mwingine maana kila mwanaume unakuwa humwamini.
My advice to u LD, take as much break as you can, hata ikifika miaka 10, so long as you are happy.
 
Asante Martina, kumbe inwezekana kwenda likizo ukiamua, mwaka mmoja nayo nahisi kwa watu wengine ni mrefu sana.
Hao wakaka hapo bwana duuuuuuu!!! Au acha nisiseme kitu.

Hivi LD, heart breaking huwa ni kwa akina dada tu, au hata wanaume?
Naona akina dada wengi ndo wahanga sana wa hii kitu!
 
Kila kitu ni uamuzi LD, kama umeamua utaweza, miaka mitano siyo mingi ukiwa unaishi na amani....................
fuata nafsi yako. kupumzika hasa baada ya kuvunjika moyo ni kuzuri sana ingawa wadada wengi hawataki kufanya hivyo, na matokeo yake unajikuta unahama kwa mkaka mmoja baada ya mwingine maana kila mwanaume unakuwa humwamini.
My advice to u LD, take as much break as you can, hata ikifika miaka 10, so long as you are happy.
kwenye bold hapo ni UPOTOSHAJI.....!
mi sitaki kuamini kuna maisha ya ''being happy'' kwenye hii likizo.....
 
Mshiki nina swali Dogo tu kwako!! Hivi baada ya hiyo miaka Mitano then utaamua kupenda tena kama zamani? utapenda kidogo? au utafanyaje?
Nasubiri jibu ili nije na maswali mengine!!

Nahisi nitapenda kama zamani, lakini kwa tahadhari sana.
Nafasi ya Mungu ibaki pale pale pia.
 
Unaweza sana mimi hiyo miaka niliwahi kabisa kukaa toka 19... mpaka 2001. Ila hiyo sababu ilikuwa bab kubwa na sitaweza kusahau mpaka naingia kaburini maana nilikuwa nachukia kila mwanaume.
 
Back
Top Bottom