Hebu jikumbushie 'Siku ya Gulio Katerero'

Paka Jimmy
Makari Hodari
Paulo usije kucheza na sisi
Mama linda kuku zako, huja nunda.
Kiswira binti mfalme aliyetaka ule mwezi uwakao usiku utunguliwe.
 
Kipindi hicho niko Majengo primary - Moshi. Kuna mwalimu alikua anachapa fimbo balaa, alikua anaitwa Mbando na mwingine alitoka JKT alikua anaitwa kijeshijeshi.
 
Saa ya kwenda kwetu x2
Kweheri mwalimu kwaheri x4
Ya kuonana keshoooooooooooo...... Mbio home kusaidia kukamua maziwa na kuchanja kuni...
 
unavaa kaptula 3 kukwepa bakora zisikuingie mwilini tena za jeans au unaweka maboksi na makaratasi kwenye makalio duh!zamani bakola zilikuwa zinatembea sana!

Daaah! Mkuu umenikumbusha mbali, nakumbuka nikiwa darasa la nne nilikuwa mkorofi sana hivyo kila siku lazma niadhibiwe. Nilikuwa naweka kaptula tatu kabisa. Siku moja mwalimu akaona zmevimba sana akaniamulu nivue mbele ya wanafunzi wenzangu nikabaki na moja tu ndo akaniadhibu. Bahati mbaya zilikuwa chafu nilihabika sana yaani kitendo hicho kiliniuma zaidi ya fimbo na tangu siku hyo nilibadili tabia. Ila huwa nawaza ningekuwa najitambua kama sasa hivi ningempeleka kwenye vyombo vya sheria.
 
lugha.JPG

Kitabu cha 8=Darasa la sita. Humo ndio utakuta wimbo wa Tanzania, tanzania nakupenda kwa moyo wote... na shairi la Tuipende Tanzania.. hapa naweka verse mbili, tatu:
Sina budi kuisifu, nchi yetu Tanzania
Kwa shairi maarufu, na vina kupangiia,
Nipange na kusanifu, shairi kuwaimbia
Tuipende Tanzania,nchi tuliyozaliwa.

Kuna mlima mrefu, kwa sifa twajivunia
Ukiwekwa kwenye safu, urefu kukadiria,
Hapawi ulinganifu, Afrika yote pia,
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.

Hapawi w kulingana, wala kuukaribia
Hawaupati wa Ghana, Uganda wala Zambia
Milima kila namna, yote haitofikia
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.

Una vilele viwili, majina nawatajia
Mawenzi ni cha awali, hapa nawahesabia
Kibo kilele cha pili, jamani nawaambia,
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.

Naacha mlima ule, na vilele vyake pia
kusudi nisongembele, kwenye mbuga kuingia
nifike hapa na pale, nichungue kila njia
tuipende tanzania nchi tuliyo zaliwa

Nifikapo Serengeti, au Mikumi kwa nia
Kwa jitihada na dhati, wanyama kuangalia
kuna makundi ya nyati, nyumbu na pundamilia
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.

Mbuga na misitu hii, na nisivyowatajia,
Huvutia watalii, kila mwaka kutujia,
Nao hawavumilii, wanyama kuwasifia,
Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa...
 
Mmojaa anaimbisha..
Kiibanga...darasa zima tunaitikia...ampiga mkoloni! tumsifu! Tumsifu kibangaa, ni shujaa mkuuu!! Wimbo huu ulihit kinyama!
 
Back
Top Bottom