Headache au maumivu ya kichwa

Jaribu kunywa maji nayo ni tiba nzuri kwa kichwa imenisaidia sana nami nilikuwa na matatizo kama hayo.. kuna post humu ya maji kama dawa ijaribu mpendwa...
 
Onana na Dr yawezakan moja kati ya haya au jengine

-Upuungufu wa macho labda unataka glasses
-Migrane kama ni one side
-Gas pia inasabisha, angalia chakula chako. Once I thought nina cance ya kichwa kumbe gas ilikuwa inanisumbua:A S-cry:

Hivi madame macho nayo huwa yanapungua?
 
wandugu,naomba mnisaidie kumpata daktari wa maradhi ya kichwa.

Kichwa changu huwa kinauma sana na nimeshakwenda hospital nikapatiwa miwani mara mbili ila bado kinanisumbua.

naomba kwa yeyote anayemfahamu daktari anayetibu maradhi ya kichwa maana hii hali inazidi kuniumiza.
 
Pole sana ndugu ,hata mimi nina rafiki yangu anakunywa panadol na hedex kama pipi,naye ameshapewa miwani lakini haijamsaidia,kwa wanaojua jamani saidieni hili.
 
Pole sana!!Ila watu wengi wanashindwa kufuata masharti ya kuvaa miwani,unapopewa miwani ya kichwa unapaswa kuvaa muda wote isipokuwa muda mfupi ukiwa unaoga,mazoezi na kulala.Sasa wengine anavaa akiwa anatoka nyumbani tu.
 
Mawazo yanahusika kwenye uumwaji wa kichwa kwa muda mrefu.Nitarudi baadae kufafanua.
 
Mi siyo daktari, lakini kadiri nijuavyo, kichwa huwa hakiumi chenyewe tu.

Daima kunakuwa na sababu ya kufanya kiume: au una mawazo mengi kichwani (haunting issues), au una ugonjwa fulani, mf. BP (kapime), macho (=ndiyo maana wamekuvalisha miwani), au ugonjwa wowote ambao mwisho wake unakuletea hiyo migrane headache.

Kwa ushauri, usitibu kichwa kama kichwa bali tafuta source ya tatizo; na kupata chanzo hicho unapaswa kufanya check-up ya mfumo mzima wa mwili wako.

Pole sana mkuu.
 
Pole sana ndugu ,hata mimi nina rafiki yangu anakunywa panadol na hedex kama pipi,naye ameshapewa miwani lakini haijamsaidia,kwa wanaojua jamani saidieni hili.

Kuna daktar hapa Dodoma anaitwa MATOVOLWA ana hospitali yake maeneo ya AREA "A" inaitwa MATOVOLWA alinitibu maumivu ya kichwa yaliyodumu kwa MIAKA 10 yaliyoambatana na KUKOSA USINGIZI.km upo Dom jaribu kumuona YEYE MWENYEWE.
 
hivi kuna uhusiano kati ya kuumwa kichwa mara kwa mara na maambukizi ya UKIMWI.
mimi kichwa huwa kinaniuma lakini natumia maji tu kinatulia niligundua mara nyingi nikiwa safarini ndio kichwa kinaniuma hivyo huwa sisahau maji,
causes nyingine ni kutumia kompyuta muda mrefu so huwa natafuta muda napumzika dalili yake huwa naona macho yaaona maluweluwe so na relax.
ni vizuri uwe unaweka record ya unavyoumwa kichwa na probable cause inaweza kukusaidia kuepuka maumivu.
 
wandugu,naomba mnisaidie kumpata daktari wa maradhi ya kichwa.

Kichwa changu huwa kinauma sana na nimeshakwenda hospital nikapatiwa miwani mara mbili ila bado kinanisumbua.

naomba kwa yeyote anayemfahamu daktari anayetibu maradhi ya kichwa maana hii hali inazidi kuniumiza.

Mimi sio doctor, lakini na mimi nina matatizo hayohayo, nikajaribu kusoma Advance Biology Book nlipokua form 6.
Matatizo yake wameandika kwamba macho ya mgonjwa huwa hayana uwezo wa kupunguza ukali wa muangaza unaotakiwa kupita katika retina ya jicho (the eye failed to regulate the threshold value intensity of the light to the retina) hivyo huifanya retina kuwa moto (over heated) na kichwa kuuma.
Na ndio maana wengi wenye matatizo haya huwajia wakati wa jua kali na wakati mwengne wasiweze kutembea kwenye jua kali.
Madaktar huwapa wagonjwa miwani ambayo hupunguza ukali wa muangaza (light intensity) na mara nying miwan hii huwa ni photo glasses. (nlizowah kutumia mie ni black-photoglasses na grey-photoglasses)
Kutumia miwan ndo suluhisho lake
 
Ili tatizo la kusumbiliwa na kichwa na mimi limenianza kama wiki mbili hivi zimepita baada ya kumeza dawa za malaria kichwa kimeniuma mfululizo hasa nyakati za usiku, nimecheck dama hiko 13 ambapo dakitari ameniambia ni kiwango kizuri kwa mwanaume, typhoid sijapima bado. natoka jana na nimeanza kusikia misuli ya macho ikikaza, hivyo leo jioni nimepanga nikacheck typhoid na Macho.
 
nmekuwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa hasa upande wa kipandauso nmejtahd kumeza dawa za kutuliza maumivu lkn kinaniuma,inaweza ikawa n nn?
 
Ili tatizo la kusumbiliwa na kichwa na mimi limenianza kama wiki mbili hivi zimepita baada ya kumeza dawa za malaria kichwa kimeniuma mfululizo hasa nyakati za usiku, nimecheck dama hiko 13 ambapo dakitari ameniambia ni kiwango kizuri kwa mwanaume, typhoid sijapima bado. natoka jana na nimeanza kusikia misuli ya macho ikikaza, hivyo leo jioni nimepanga nikacheck typhoid na Macho.
Mkuu ulipona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom