Hazina imekauka - pensheni za wastaafu zakatwa

Katika kile kinachoonekana sasa serikali imefilisika, imewakata nusu ya pensheni ya wastaafu ya mwezi February.

Kwa mfano wastaafu wengi hupokea sh 300,000 kila baada ya miezi sita. Sasa wamepewa 150,000/=!.

Nakumbuka, Slaa alisema watanzania mkilogwa mkamchagua JK, mjue ni janga la taifa. sasa yanatokea, wacha tuyaone ni kutosikia kwetu. Wenye magari ni jahanamu- TRA, Fire dept, trafic ni moto wa jahananu barabarani-eti wanakusanya kodi.
 
Wacha wakatwe tu hizo ela zao. Wazee hawa hawa si ndo wanasema ccm imewalea, ccm inawafanya waishi kwa amani, afu kipindi cha uchaguzi si wanaipigia kura ccm, huku wakiwa na nyuso za furaha kwenye ma t-shit na makofia yao ya njano na kijani...
Baba mwanaasha endelea kuwapini mpaka wakome!
 
Na bado mpaka kieleweke!
CCM juu,
Kuna dingi analaani uyo nadhani CCM watapata laana maana hawa wazee lawama zao hufika kwa mola straight!
 
Wacha wakatwe tu hizo ela zao. Wazee hawa hawa si ndo wanasema ccm imewalea, ccm inawafanya waishi kwa amani, afu kipindi cha uchaguzi si wanaipigia kura ccm, huku wakiwa na nyuso za furaha kwenye ma t-shit na makofia yao ya njano na kijani...
Baba mwanaasha endelea kuwapini mpaka wakome!

Mkuu sio wazee wote wako CCM, wazee maeneo ya pwani ndo wengi kijani, kwanza si wastaafu wengiwao walikua wakicheza bao. Sidhani km kuna mzee mstaafu anaikubantia CCM kwa sasa.
 
Katika kile kinachoonekana sasa serikali imefilisika, imewakata nusu ya pensheni ya wastaafu ya mwezi February.

Kwa mfano wastaafu wengi hupokea sh 300,000 kila baada ya miezi sita. Sasa wamepewa 150,000/=!.

Huu ni uonevu mkubwa kupita kiasi. Hawa wazee walifanya kazi nzuri sana wakiwa na nguvu zao sasa wanaonekana hawana maana na ndiyo maana hazina wakiishiwa wanawakata hata hicho kidogo wanachostahili wazee wetu wasitaafu.

Wabunge mnaosema maisha yamepanda Dodoma na mnataka 200,000/= kwa siku, mnaona lakini serikali yenu inavyo wafanyia wastaafa? Au manjifikilia nyie tu?
 
Siwezi kuongelea kukauka kwa Hazina ila kuna mabadiliko katika mgao wa pensheni za wastaafu wanaolipiwa hazina. Kuanzia january mwaka huu serikali imebadilisha utaratibu wa kulipa badala ya miezi sita sita itakua inalipa miezi mitatu mitatu. Huu utaratibu wa miezi sita sita hata mimi mlikua siupendi naona bora watumie wa miezi mitatu mitatu au wakiweza walipe mwezi mmoja mmoja.
 
Imenisikitisha sana, yani serikali imeamua kuwanyonya hata hawa wazee! Visenti vyao kidogo halafu vinakatwa, hii ni laana.

Na hii laana ndiyo itakayakatisha maisha ya ccm kabla ya 2015
 
Si wazee wote wamekatwa bana! mbona mimi babu amepata zote? Hebu wekeni orodha ya hao babu zenu hapa.
 
Badala ya kuwaonea hawa wazee wastaafu, kwanini wasawakate viongozi wakuu wa KITAIFA wastaafu ambao ndiyo wanapata marupurupu makubwa eg 80% ya mshahara wa kiongozi aliyeko madarakani, mishahara ya walinzi wawili, dereva 1, House Maid 1, posho ya mafuta etc. Viongozi hawa tunao lundo na serikali ingeweza kupata mi-pesa mingi kutoka kwao
  1. Julius Kambarage Nyerere
  2. Rashid Mfaume Kawawa
  3. Edward Moringe Sokoine
  4. Alhaji Ali Hassan Mwinyi
  5. Aboud Jumbe Mwinyi (VP)
  6. Abdul Wakil Juma
  7. Dr. Omari Ali Juma
  8. David Cleopa Msuya
  9. Salim Ahmed Salim
  10. Joseph Sinde Warioba
  11. John Samwel Malecela
  12. Benjamin William Mkapa
  13. Frederick Tuluway Sumaye
  14. Edward Ngoyayi Lowassa
  15. Adam Sapi Mkwawa (Speaker)
  16. Pius Msekwa
  17. Samuel Sitta (?)
  18. Francis Nyalali (CJ)
  19. Augustin Ramadhani
 
Kilio hiki kipo kweli. Wazee wanalalamika na hawajui nini wafanye. Serikali haitakiwi kuwachakachua wazee hawa, bora kuangalia namna nyingine lakini si kuwachakachua wazee!

Hivi watu wote wanalipa kodi kama inavyostahili especially wafanyabiashara wakubwa wenye connection za kisiasa? Kodi inadaiwa kwa nguvu kwa watu choka mbaya ndo maana hazina haiwezi kujaa. Wenye kufanya biashara kubwa nina shaka sana kama wote wanalipa kodi jinsi inavyostahili
 
Laki 3 kila miezi sita,imekatwa tena.Si wangejipunguzia mishahara yao?Sasa wanawakata wazee wa watu just because hakuna wa kuwakingia kifua.

Vijana ndo mnatakiwa kufanya mapinduzi ya hii nchi ili tupate kuwatetea wazee wetu hawa
 
Siwezi kuongelea kukauka kwa Hazina ila kuna mabadiliko katika mgao wa pensheni za wastaafu wanaolipiwa hazina. Kuanzia january mwaka huu serikali imebadilisha utaratibu wa kulipa badala ya miezi sita sita itakua inalipa miezi mitatu mitatu. Huu utaratibu wa miezi sita sita hata mimi mlikua siupendi naona bora watumie wa miezi mitatu mitatu au wakiweza walipe mwezi mmoja mmoja.

taarifa nilizopata nikwamba, fedha hakuna...wanasingizia tu kubadili mfumo, kwann wabadili wakati huu?. Kuna wengine watapokea 50000 wakipewa kwa mwezi. Utazifanyia nn sasa, hata kununua kiroba kidogo cha sukari hazitoshi.
 
Tanzania yaweza kuwa mahali hatari sana kuishi maana serikali hajali wananchi,poleni sana wazee MUNGU alkiwajalia kufika 2015 wahukumuni kupitia kisanduku cha kura.
 
Si wazee wote wamekatwa bana! mbona mimi babu amepata zote? Hebu wekeni orodha ya hao babu zenu hapa.

mkuu sijakurupuka! acha uwongo babu yako kapewa ngapi?. Mzee William wambura, mzee Joseph shereli, mzee Makuru jonathan, mzee Josia kirigiti, mzee msila abbel. Hao ni baadhi yao mkuu hata pension a/c zao ukitaka nikupe. Hii kitu si porojo, ipo.
 
nimewakumbuka wazee wa east africa walivomwagiwa na maji ya ***** hadi nimetokwa na machozi
 
Hizo za viongozi kulipana posho, kwenda ziara nje ya nchi, sherehe nk zinatoka wapi? Serikali yetu imejaa usanii!
 
Back
Top Bottom