Hazina hoi

Haahaaa! Nchi hii inaendeshwa kwa maneno maneno tu. Mtu akikuambia kitu inawezekana hamaanishi. So, it could be true wamefulia.
 
Wayapige mnada yale malori yaliyoandikwa Signal,transfuel na lake Oil madogo waendelee kusoma.
Big up wafadhili kwa kuamua kupeleka ela kwenye miradi naona uko sijui wataamua kuiba cement!
 
hili halina ubishi maana leo wajumbe wa loan board walikuwa TBC1 kwenye jambo waliulizwa wakakili hawajapta hela kutoka hazina
 
Wayapige mnada yale malori yaliyoandikwa Signal,transfuel na lake Oil madogo waendelee kusoma.
Big up wafadhili kwa kuamua kupeleka ela kwenye miradi naona uko sijui wataamua kuiba cement!

Mh una akili kama Newton!
 
kunatetesi hazina imefulia na imeshindwa kuwapa loans board pesa za kukopesha wanafunzi , Hadi sasa vyuo vitatu tu ndio vimepewa fedha na loans board mwenye taarifa sahihi atujuze

watu wa bodi wanasema akaunti yao inasoma '0'
 
Wayapige mnada yale malori yaliyoandikwa Signal,transfuel na lake Oil madogo waendelee kusoma.
Big up wafadhili kwa kuamua kupeleka ela kwenye miradi naona uko sijui wataamua kuiba cement!

ni ya serikali?????
 
Hata loan boad nao ni serikali wewe unataka aseme nani,,,,,?????baada ya maandamano ya wanafunz wa cbe na st john dar heslb wamesema akaunt yao inasoma zero,,,,,
Huku UDOM hali ya maisha kwa wanafunzi si nzuri je serikali ituelezee maana ya kuwa na bujeti ya mwaka.
 
jamani BOT juzi tu walieleza tuna akiba ya dola bilioni tatu. sasa tetesi zatoka wapi?

Kookoliko,

Hizo dola Bilioni 3.6 zilizoko BOT ni foreign exchange zinazokuwa reserved kwa ajili ya matumizi ya dharura kama manunuzi ya bidhaa muhimu na mali ghafi toka nje ya nchi tena kwa miezi 4 tu!!!Hela inayokaa hazina ni ile inayokusanywa na TRA kwa ajili ya matumizi ya kila siku ya Serikali. Kwa sasa Hazina kweli iko DRY na Kiwete anaendesha serikali kwa CASH BUDGET. Hela inayokusanywa kwa siku ndiyo inayoenda kutumiwa siku hiyohiyo!!!!!

Kuna gazeti leo limeripoti kuhusu mtafaruku ya Waziri na Naibu wake kutofautina kuhusu hali ya kifedha serikalini(hazina). Nasikia Waziri mmoja kasema Serikali haina pesa mwingine akakanusha kuwa serikali ina pesa!!!

Huu mkanganyiko unaweza ktoa picha halisi kuwa HALI YA KIFEDHA SI SHWARI ndani ya Serikali. Sasa mimi sielewi hawa ma-DC wamelipwa nini kama HAZINA IMEKAUKA! Je, wamekopeshwa au ndiyo kusema kile kilichopatikana hazina ndicho kimekombwa choote????
 
Kila mkutano wa nje ni lazima JK aende? Hivi hao wasaidizi wake kazi yao ni hapa tz tu.
 
Ni kweli. Sasa hivi wakuu wa wilaya wamepewa assignment moja kali sana. Ya kudeal na makampuni kwa vitisho. Utawal wa CCM hadi kufika 2015 sijuiii!!
 
Tuna matumizi ya ajabu sana nchi ambayo yanatumaliza; katika uteuzi wa wakuu wa wilaya kuna ambao wameachwa.......jaribuni kuchunguza kiinua mgongo chao ni kiasi gani mtajua kwa nini Serikali haiwezi kuwa na mapato yanayozidi matumizi
 
Jamani wafanya biashara hawana makosa maana wakati wa uchaguzi mkuu waliichangia CCM na bakuli la CCM lilipita kwa wale wafanya biashara potential. Kinachotokea leo ni marejesho ya pesa zao walizochanga wakati wa kampeni, wengine walikopa toka benki, wakajaribu kupandisha bei ya vitu walipoona kuwa hawalipwi fadhila. Tuwaonee huruma maana ni haki yao.
 
Back
Top Bottom