Haye na Klitschko kutwangana Julai pili

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Link
http://magictv.co/
Stream 1 & 2
Mpambano wa ubingwa wa ndondi za uzito wa juu duniani kati ya David Haye na Wladimir Klitschko, sasa utafanyika tarehe 2 mwezi wa Julai, mjini Hamburg, kwa mujibu wa meneja wa Klitschko, Bernd Boente.
110303130809_wladimir_klitschko_david_haye_304x171_bbc_nocredit.jpg


Baada ya mazungumzo ya kina awali Haye bingwa wa uzito wa juu wa WBA na bingwa wa IBF na WBO Klitschko, walikubaliana kutwangana katika tarehe na sehemu ambayo haikupangwa.

Lakini Boente amethibitisha ukumbi unaoingiza watazamaji 57,000 wa Imtech Arena nchini Ujerumani ndipo makonde ya miamba hao yatakapovurumishwa.

"Pambano litakuwa tarehe 2 mwezi wa Julai mjini Hamburg. Hili nathibitisha kwa asilimia 100," alisema Boente.

"Tulikuwa na mtazamo tofauti na tumefanya mazungumzo kwa nchi nyingine. Switzerland ilikuwa moja wapo, Ukraine na sehemu nyingine za Ujerumani pia zilifikiriwa.

"Lakini mara zote alikuwa ni meneja wa Haye, Adam Booth pamoja na mimi, tuliyezungumzia masuala hayo, kama vile muelekeo tofauti wa kibiashara na baadae tukaamua kwa mpambano huo ufanyike Hamburg."

Haye awali alipangwa kupambana na Wladimir, mwenye umri wa miaka 35, mwaka 2009 lakini alilazimika kujiondoa kwa sababu ya kuumia mgongo na mara zote mazungumzo ya kufanyika pambano hilo yamekuwa yakikwama.

Klitschko amekuwa katika matibabu baada ya kuumia tumboni mwezi wa Desemba - kuumia ambako kulivuruga mipango ya pambano baina yake na Muingereza mwengine Dereck Chisora.

Haye, mwenye umri wa miaka 30, ambaye kwa sasa anafanya mazoezi ya kujiandaa mjini Miami, ana matumaini baada ya kumalizana na Wladimir achakazane na kaka yeke Wladimir, ambaye ni bingwa wa WBC Vitali Klitschko.

Hata hivyo, Haye mwenye maskani yake jijini London, amesema hatavuruga mipango yake ya kustaafu atakapofikisha umri wa miaka 31 mwezi wa Oktoba, akiwa amekamilishan ndoto ya kuwatwanga ndugu hao wawili.

BBC Swahili - Habari - Haye na Klitschko kutwangana Julai pili
 
hahaaaaaaaa bwana mie napenda sana huyu black ashinde unajua klitchko anashinda kwa point wakati Haye anashinda kwa knockout kazi ipo tungoje tuone itakuweje
Haye ana kazi kubwa hapa...nampa 50-50 chances...
 
hahaaaaaaaa bwana mie napenda sana huyu black ashinde unajua klitchko anashinda kwa point wakati Haye anashinda kwa knockout kazi ipo tungoje tuone itakuweje

YouTube - Wladimir Klitschko Vs David Haye July 2 Promo

Haye ni mwepesi na ana kasi lakini Klischko ana experience na pumzi ya kumaliza round zote...All in all litakuwa pambano kali cause wana style tofauti za kupigana...

Japo tutarudia enzi za kukesha kusubiri boxing kama wakati wa Tyson!
 
duh inabidi uiweke kwenye calender yako julai 2 ni siku ya mkesha kaazi kwelikweli ila siku hz kuna cm za mkononi unaweka lam tu itakuamsha pia utakua na uwezo wa kucalculate masaa!!hawa jamaa wanainyanyua sana nchi yao ya ukraine tz tungekua na watu wa namna hii ingekua poa sana!!!mimi naombea sana haye ashinde hilo pambano maana black tumepotezwa kabisa siku hz baada ya kuondoka kina tyson!
YouTube - Wladimir Klitschko Vs David Haye July 2 Promo

Haye ni mwepesi na ana kasi lakini Klischko ana experience na pumzi ya kumaliza round zote...All in all litakuwa pambano kali cause wana style tofauti za kupigana...

Japo tutarudia enzi za kukesha kusubiri boxing kama wakati wa Tyson!
 
David Haye believes he will take an army of fans to Germany for his unification showdown with Wladimir Klitschko, which has been confirmed for July 2.



article-1303322252965-0BB5CDC000000578-621010_636x300.jpg
 
Mbona Haye aliongea maneno ya kashfa vile wakati wa kupima uzito? Mi nimependa jinsi Wladmir alivyojibu maswali kiprofesheno na sio kitaarab kama msuka nywele Haye!
 
shughuli iliyo mbeleni mwa haye ni nzito kuliko alivyofikiria ni hii imeanza kujionyesha hata katika tour za kupromote pambano hili...anaonyesha kupoteza confidence aliyokuwa nayo mwanzoni kabla pambano halijawa rasmi!i dont see haye winning this fight,i go for dr steelhammer!haye asubiri adhabu kali siku ya siku.....steelhammer atahakikisha anashinda kwa point ili aweze kumpa adhabu ya kutosha raundi zote 12 otherwise pambano lisimamishwa na refa au kona ya haye warushe towel ulingoni.....
 
Kwa muda wa miaka miwili sasa ulimwengu umekuwa ukilisubiri pambano la masumbwi kati ya david haye bingwa wa uzito wa juu toka england na yote kati ya wanandugu wawili toka familia ya klitschko vladmir na vitaly. Pambano hili limewahi kupangwa hapo awali lakini kwa sababu kadhaa limeshia hewani ila sasa hakika litafanyika na hakuna wa kumkimbia mwenzie kwani tarehe 2 mwezi julai kwenye uwanja wa mpira wa hamburg arena pambano kubwa na la aina yake ambalo halijaonekana kwa muda wa miaka karibu kumi litafanyika. David deron haye amekuwa akipanda chati za mchezo wa masumbwi kwa kasi ya juu na akiwa na umri wa miaka 30 amedhihirisha uwezo wake wa kupambana katika hali ngumu dhidi ya mabondia waliomzidi kimo , na katika majaribu mbalimbali uwezo wake wa kutumia kasi na akili nyingi ndio humsaidia. Bondia anayetumia nguvu sambamba na akili nyingi david haye hakika anakutana na mtihani mgumu kuliko yote aliyowahi kukutana nayo. Hadi sasa haye ana rekodi ya kucheza michezo 26 ambapo ameshinda mara 25 , 23 kati ya mara hizo ikiwa kwa njia ya knock out huku akipoteza mchezo mmoja tu na amewahi kutwaa medali ya shaba kwenye mashindano ya dunia ya ndondi za ridhaa huko belfast mwaka 2001. Vladmir klitschko aka dr steel hammer kwa upande wake ni mtu ambaye ulimwengu wa masumbwi unamtambua vyema. Kaka yake amechukua nafasi yake katika historia ya masumbwi na sasa ni zamu yake. Siku zote klitschko mdogo amekuwa akiwaonea mabondia aliokutana nao kwa makonde yake yenye nguvu anayotupa kwa ustadi na mahesabu makali . Akili nyingi alizo nazo ambazo zinasaidiwa sana na uwezo wa hali ya juu alionao kwenye mchezo wa chess ambao sambamba na kaka yake vitaly amewahi kuchukulia ubingwa wa dunia unachangia sana akili nyingi anazotumia akiwa ulingoni lakini hata yeye mwenyewe anatambua fika kuwa kiwango cha kujiamini cha david haye na uwezo halisi wa kutupa makonde ya kasi na wepesi ambao siku zote humletea faida ni vitu ambavyo klitschko atalazimika kutumia ujanja ambao hajawahi kuutumia siku za nyuma kama atataka kumshinda muingereza huyu. Vladmir klitschko ana rekodi ya kucheza michezo 58 ambapo ameshinda mara 55, akiwa na knock out 49 huku akiwa amepoteza mara 3. Dr steel hammer pia amewahi kutwaa medali ya dhahabu kwenye michuano ya olimpiki iliyofanyika huko atlanta marekani mwaka 1996 pamoja na medali ya shaba kwenye mashindano ya huko velje iliyofanyika mwaka huo huo wa 1996, julai mbili mwaka huu ni tarehe ambayo itaingia kwenye historia ya mchezo wa masumbwi kwani mmoja kati ya watu hawa wawili, toka ukraine au toka england ataondoka ulingoni akiwa amevalia mikanda minne kiunoni mwake. Je itakuwa vladmir klitschko ambaye ataongeza mkanda mmoja wa wba unaoshikiliwa na haye juu ya mikanda yake ya ya ibo, ibf na wbo au kinyume cha hapo yaani haye kuongeza mikanda inayoshikiliwa na vladmir juu ule wa kwake, jibu litapatikana julai mbili huko hamburg ujerumani.
 
mpambano mkali katika media ila katika ulingo ni wa upande mmoja....haye mwepesi na si heavyweight mkali kama anavyojiongopea, hatotoa upinzani unaofikiriwa!sasa hivi acha aongee ila mavi yatamgonga chupi pale watabaki ulingoni wawili!
 
Aliulizwa BAADA YA GAME ATAKUJA KWENYE press conference akasema NDIO..ila ki ukweli naona Haye ananafasi finyu kumchapa huyu Kiitchko.Leo walifanya public training show
 
Wenye details kuhusu mida ya hilo pambano pamoja na channel zitakazoonyesha mtuwekee hapa Tafadhali coz bado masaa tu.
 
Huyu Haye ana dharau sana, niliona jinsi anavyomtambia Klitchko. Nawapenda kina Klitchko lakini hapa uafrika kwanza, all the best Haye nategemea tambo zako ziwe kweli.
 
Wenye details kuhusu mida ya hilo pambano pamoja na channel zitakazoonyesha mtuwekee hapa Tafadhali coz bado masaa tu.
Mida itakuwa 2145 BST ndo manjonjo yataanza ila kwa saaa za kibongo nadhani itakuwa saa sita usiku!
[video]http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/boxing/13990732.stm[/video]
 
Tale of the tape
Haye Klitschko​

30 Age 35
26 Fights 58
25 (23) Wins (KO) 55 (49)
1 (1) Defeats 3 (3)
6ft 3in (1.91m) Height 6ft 6in (1.99m)
15st 3lb(213lb. 97.5kg) Weight 17st 5lb(243lb. 111kg)
78in (6ft 6in. 198cm) Reach 81in (6ft 9in. 205cm)​
 
Back
Top Bottom