Haya ya s.h. Amon hayakubaliki kabisa;mungu aingilie kati

Status
Not open for further replies.

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,906
22,018
Mgogoro mkubwa umezuka kwenye kampuni ya SH AMON...INAYOUZA VIPODOZI na kuendesha shuguli za mahoteli....baadhi ya wafanyakazi waliofukuzwa kazi wamepokea barua zao bila ya kupewa chochote...

Kati ya wafanyakazi waliopewa barua hizo wapo walioitumikia zaidi ya miaka kumi.....wafanyakazi wamepeleka malalamiko yao kwenye tume ya usuluhishi...iliyopo chini ya wizara ya kazi vijana na maendeleo ya vijana

wanaitaji tume hiyo kumuamuru mwajiri kulipa mafao yao kwa kila mtu kutokana na muda wa kazi aliofanya....wafanyakazi waliofukuzwa wanadai kiinua mgongo na wengine cha hadi miaka 10 ..na wengine wanadai mishahara mpaka sasa...
Tayari Tume imemwita mwajiri sh amon na walalamikaji lakini hakuna kinachoendelea baada ya mwajiri kuwaarifu yeye watakutana mahakamani hakuna mwenye kumlazimisha kwenda kwenye majadiliano...
Mkurugenzi wa SH AMON alipoulizwa alisema wanaolalamika wakutane naye mahakamani.... hataki maswali nje ya mahakama...niemsema sitaki kumsikia mtu akinipigia simu tena tena mkome nyie waandishi mmerogwa alisikika akitukana na kutoa kejeli za maneno mengine yasiyoweza kuelezwa kwa jamii....huyu bwana anaonyesha UDIKTETA kabisa.....

Wafanyakazi wengi wamekuwa wakifokewa ama kuachishwa kazi kutokana na kutoka aouting na mzee...haya ndio mambo yanayoendelea pale S.H. AMON karibu kila mtu amekuwa akitembea na mmiliki mpaka wanawake wenye ndoa zao.....wafanyakzi wanatishwa kila siku
 
wanapandikizwa uwoga wanafanywa vifaranga mbele ya mwewe ni kutaka waparaganyike kila anaapoonekana....

""HAYATI MWALIMU NYERERE KATIKA HOTUBA YA MEI MOSSI 1995 MEI ALISEMA MBINU MMOJA WAPO YA KUJENGA UWOGA NA HOFU KATIKA KAZI NI KUWAFUKUZA WALE WANAODAI NA KUJARIBU KUDAI MALIPO ZAIDI NA HAKI NYINGINE""""

Hili litawafanya wanaobaki wahisi nao watapoteza ajira zao iwapo watadai haki zao mapema....hili ndilo linalolamikiwa na wafanyakazi wa sh amon...wanafukuzwa kama njia ya kujenga hofu na uwoga ili wahisi ajira walliyonayo ni hisani ni tuzo ni baraka na si haki

Huo ni ukiukwaji wa haki za binadamu na sheria za nchi ni wajibu wa kila mtanzania kuendeleza mapambano katika sehemu zao za kazi dhidi ya wahuni kama hawa
 
Kila kitu kina muda wake. Na mbinu hizo zitaishia chini ya carpet tu
 
JF tuanzishe duka letu la vipodozi/biashara ya uhakika............unasemaje Mkuu Invisible
 
Hivyo mnavyosema si kweli so mnataka kazi ya mtu iendeshwe kizembe hapana hilo nabisha kabisha fungueni duka lenu afu muone,....unajua kitu kimoja watanzania tulichokua nacho ni chuki huwezi ukafanya kazi ya mtu kizembe na wala mmilikia wa s.h.amon hagombani na mtu yeye anachotaka kazi ifanyike vizuri jitahidini kufuatilia tu au mnajua hiyo mali kaitoa wapi na kahangaika kiasi gani si vyema kujadili vitu msivyo vijua
 
labda wakienda mahakamani mbivu na mbichi zitajulikana maana jamaa anaconfidence sana hataki majadiliano anachotaka ni mahakamani tu
 
Tanzania kwenye sekta binafsi kitu kinachoitwa kiinua mgongo ni juu ya mkataba wako na mwajiri. Sheria ya kazi haina kipengele cha kiinua mgongo, hivyo ukifukuzwa au kuachishwa kazi itategemeana na mkataba wako wa kazi unasemaje, kinyume na hapo ni busara tu ya mwajiri wako.

Mikataba mingi ya kazi, kwa uzoefu wangu, inasema mwajiri akikuachisha kazi atakulipa mshahara wa mwezi/miezi 1-3, hii ni kwa wafanyakazi wa kawaida. Kwa nafasi za juu, mfano ukurugenzi, suala hili mara nyingi linajadiliwa na kukubaliwa wakati wa kuajiri, ukiwa mwepesi inakula kwako.

Kitu ambacho mwajiri analazimika ni kukulipia mafao (NSSF, PPF, PSPF, n.k), ambayo ni angalau asilimia kumi (10%) ya mshahara wako kila mwenzi. Mwajiri akishatimiza hilo, mengine ni busara na huruma yake. Hiyo ndiyo sheria yetu.

Naamini jeuri ya mkurugenzi wa SH Amon inatokana na hili ndio maana mambo ya kazi na malalamiko ya mafao mara nyingi hayaendi mahakamani bali kwenye tume za usuruhishi au vyama vya wafanyakazi.
 
Acheni wivu wao kike (sorry madam b). Kwa wenye experiencs ya kuajili wafanyakazi wengi wanaboa sn..... kile anachotakiwa kufanya hafanyi. Siamini kwamba unafukuzwa tu bila sababu. Huyo aliyekaa miaka kumi ni bora ashukuru pia kwa kusitiriwa kwa kipindi chote hicho na sio vzr kumkashfu mtu aliyekusaidia kiasi hiko, hiyo inakuwa sawa na kunyea kambi
 
Tanzania kwenye sekta binafsi kitu kinachoitwa kiinua mgongo ni juu ya mkataba wako na mwajiri. Sheria ya kazi haina kipengele cha kiinua mgongo, hivyo ukifukuzwa au kuachishwa kazi itategemeana na mkataba wako wa kazi unasemaje, kinyume na hapo ni busara tu ya mwajiri wako.

Mikataba mingi ya kazi, kwa uzoefu wangu, inasema mwajiri akikuachisha kazi atakulipa mshahara wa mwezi/miezi 1-3, hii ni kwa wafanyakazi wa kawaida. Kwa nafasi za juu, mfano ukurugenzi, suala hili mara nyingi linajadiliwa na kukubaliwa wakati wa kuajiri, ukiwa mwepesi inakula kwako.

Kitu ambacho mwajiri analazimika ni kukulipia mafao (NSSF, PPF, PSPF, n.k), ambayo ni angalau asilimia kumi (10%) ya mshahara wako kila mwenzi. Mwajiri akishatimiza hilo, mengine ni busara na huruma yake. Hiyo ndiyo sheria yetu.

Naamini jeuri ya mkurugenzi wa SH Amon inatokana na hili ndio maana mambo ya kazi na malalamiko ya mafao mara nyingi hayaendi mahakamani bali kwenye tume za usuruhishi au vyama vya wafanyakazi.

Embu nenda kaisome vizuri iyo sheria then uje utueleze kwamba hakuna sehemu ya kiinua mgongo mkuu.

Mshaangalia lakini huu uzi ni wa mwaka gani?
 
Embu nenda kaisome vizuri iyo sheria then uje utueleze kwamba hakuna sehemu ya kiinua mgongo mkuu.

Mshaangalia lakini huu uzi ni wa mwaka gani?

Duh! Mwaka wa uzi sikuangalia. Lakini kuhusu kiinua mgongo, ninayosema ndio hivyo kwa kadiri ya Employment and Labour Relations Act. Kama unahoja tofauti, nipe kipengele cha kiinua mgomgo kwenye hiyo sheria tujadili.
 
Mkurugenzi wa SH AMON alipoulizwa alisema wanaolalamika wakutane naye mahakamani.... hataki maswali nje ya mahakama...niemsema sitaki kumsikia mtu akinipigia simu tena tena mkome nyie waandishi mmerogwa alisikika akitukana na kutoa kejeli za maneno mengine yasiyoweza kuelezwa kwa jamii....huyu bwana anaonyesha UDIKTETA kabisa.....

Watu wanaokuwa n utajiri bila kuwa na elimu wana matatizo sana. Huyu jamaa alimaliza darasa la saba akabangaiza wee biashara ambazo wala zitaki niziseme humu JF na akawa tajiri. Japo alijitahidi kujiendeleza kwa kutumia walimu binafsi bado kuna ka tabia ka tajiri asiesoma kanaonekana kila wakati.
 
Toka lini tajiri akawa msomi na elimu kubwa?
 
Mbona kwa mfumo huu mpya mahakamani atakwenda yeye au ndugu zake manake ukileta ubabe unapasuka sasa ni bora akajadiliana nao sasa kutokana na watu wa siku hizi ni tofauti kabisa na wazamani itamkosti zaidi yeye kuliko hao anaotaka kuonana nao mahakamani. Manake hawana cha kupoteza zaidi yake.
 
Duh! Mwaka wa uzi sikuangalia. Lakini kuhusu kiinua mgongo, ninayosema ndio hivyo kwa kadiri ya Employment and Labour Relations Act. Kama unahoja tofauti, nipe kipengele cha kiinua mgomgo kwenye hiyo sheria tujadili.

Read between lines mkuu, sehemu ya II C ya sheria ya ajira na mahusiano kazini Ibara ya 26 (1) inahusu.
 
ac nyie ni uvivu na ubishooheni kumchafua sauli hata kama hajasoma haijalishi amekusitili miaka kumi ww ulie soma mbona umefeli ukaenda kwa mtu wa darasa la saba huyu bwana amehangaika sana mpaka kufikia hapo alipo amevuka mito na mabonde acheni hzo tabu yenu na suala la kusema anatoka na wafanyakazi hio haina mantiki ulikuwa unasubili ufukuzwe ndio uje hapa kwenye jamvi kutoa pumba zako hzo na uende mahakamani mtakutana huko
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom