Haya Wana-Yanga Afrika, kazi kwenu!

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho CAF, Simba SC sasa watawavaa El Ahly Shandy ya Sudan baada ya Al Ahli Shandi kuwachapa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji jumla ya magoli 3-0.

Katika mchezo wa leo El Ahly Shandy wameibuka na ushindi wa goli 2-0 kwenye Mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa huko Mjini Shandi, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

Bao zote 2 za Al Ahli Shandi zilifungwa na Nadir Eltayed katika Dakika za 14 na 60. Hivyo El Ahly Shandy wamewatoa Ferroviario de Maputo kwa jumla ya bao 3-0 baada ya pia kuwatungua huko kwao Maputo bao 1-0.
12147.gif
Al-Ahli ambao nembo yao ni hiyo hapo juu, wanashika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Sudan, wakiwa na pointi 37, ambazo ni 31 nyuma ya vinara wa ligi hiyo,Al-Hilal baada ya mechi 26 kuchezwa.
Jezi ya nyumbani ya Al Ahli Shandi ni ya rangi ya buluu tupu kama inavyoonekana hapo chini.
Al Ahly.....jpg
Kama ilivyo utaratibu wetu wa siku zote, ni zamu ya klabu hii ya Sudan kupewa sapoti kubwa na washabiki wa Dar es salaam Yanga Afrika ili waweze kutoa upinzani katika mchezo wa raundi ya 16 utakaochezwa hapo Uwanja wa Taifa Aprili 29 na marudiano huko mjini Shandi majuma mawili baadae.
Kuhusu jezi, washabiki wa Yanga wanaweza kuvaa jezi za klabu ya Chelsea, ambazo zimetapakaa kwa wingi jijini Dar, hii ni kuwaepusha gharama za ziada za kutafuta jezi halisi za Ahli, na pia kuwakomoa wafanyabiashara uchwara wanaotumia uhasama wetu mtamu kujipatia fedha za bwerere.
Nawasihi juhudi za kutafuta taarifa zaidi za timu yenu ya muda zianze mapema ili siku ya siku muje uwanjani mkiwa 'full detailed'. Na katika hili mna baraka zangu zote, kwa roho safi.
Tulianza na Kiyovu, ikaja zamu ya ES Setif, na sasa ni Al-Ahli Shandi ya mjini Shandi, Sudan.
Karibuni wadau wa Yanga Afrika ya Umoja wa Mataifa, chama kongwe kabisa humu nchini na lililopigania Tanganyika huru.
Habari kwa hisani ya: SPORTS IN BONGO: Simba kukwaana na Wasudani katika Raundi ya 3
Picha kwa hisani ya:http://www.koorasudan.com/
Taarifa za klabu kwa hisani ya:http://au.eurosport.com/football/teams/al-ahli-shandi/teamcenter.shtml
 
hivi lile pambano la frances cheka na stephano mwasika ni lini vile?nasikia pia tegete amekubali kupanda ulingoni kuzinyuka na japhet kasseba.
Simba mpira Yangu masumbwi!
 
hivi lile pambano la frances cheka na stephano mwasika ni lini vile?nasikia pia tegete amekubali kupanda ulingoni kuzinyuka na japhet kasseba.
Simba mpira Yanga masumbwi!

Hawana wasiwasi, Tibaigana atawapigania...
 
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho CAF, Simba SC sasa watawavaa El Ahly Shandy ya Sudan baada ya Al Ahli Shandi kuwachapa Ferroviario de Maputo ya Msumbiji jumla ya magoli 3-0.

Katika mchezo wa leo El Ahly Shandy wameibuka na ushindi wa goli 2-0 kwenye Mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa huko Mjini Shandi, Mji ambao uko Kilomita 150 Kaskazini Mashariki ya Mji Mkuu wa Sudan, Khartoum.

Bao zote 2 za Al Ahli Shandi zilifungwa na Nadir Eltayed katika Dakika za 14 na 60. Hivyo El Ahly Shandy wamewatoa Ferroviario de Maputo kwa jumla ya bao 3-0 baada ya pia kuwatungua huko kwao Maputo bao 1-0.
Al-Ahli ambao nembo yao ni hiyo hapo juu, wanashika nafasi ya nne katika ligi kuu ya Sudan, wakiwa na pointi 37, ambazo ni 31 nyuma ya vinara wa ligi hiyo,Al-Hilal baada ya mechi 26 kuchezwa.
Jezi ya nyumbani ya Al Ahli Shandi ni ya rangi ya buluu tupu kama inavyoonekana hapo chini.
Kama ilivyo utaratibu wetu wa siku zote, ni zamu ya klabu hii ya Sudan kupewa sapoti kubwa na washabiki wa Dar es salaam Yanga Afrika ili waweze kutoa upinzani katika mchezo wa raundi ya 16 utakaochezwa hapo Uwanja wa Taifa Aprili 29 na marudiano huko mjini Shandi majuma mawili baadae.
Kuhusu jezi, washabiki wa Yanga wanaweza kuvaa jezi za klabu ya Chelsea, ambazo zimetapakaa kwa wingi jijini Dar, hii ni kuwaepusha gharama za ziada za kutafuta jezi halisi za Ahli, na pia kuwakomoa wafanyabiashara uchwara wanaotumia uhasama wetu mtamu kujipatia fedha za bwerere.
Nawasihi juhudi za kutafuta taarifa zaidi za timu yenu ya muda zianze mapema ili siku ya siku muje uwanjani mkiwa 'full detailed'. Na katika hili mna baraka zangu zote, kwa roho safi.
Tulianza na Kiyovu, ikaja zamu ya ES Setif, na sasa ni Al-Ahli Shandi ya mjini Shandi, Sudan.
Karibuni wadau wa Yanga Afrika ya Umoja wa Mataifa, chama kongwe kabisa humu nchini na lililopigania Tanganyika huru.
Habari kwa hisani ya: SPORTS IN BONGO: Simba kukwaana na Wasudani katika Raundi ya 3
Picha kwa hisani ya:صØ*يفة ومنتديات كورة سودانية | كورة سودان | كورة السودان | أخبار الرياضة | الأخبارالرياضية
Taarifa za klabu kwa hisani ya:Al Ahli Shandi - Club details - Football - Eurosport Australia
Siku imefika na lile neno lipate kutimia.
Way to go SSC!
 
.....baadhi ya Wana Yanga wameanza kununua Jezi nyekundu kuelekea pambano la Mei 5, 2012.
 
Back
Top Bottom