Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,598
Kwa siku ya pili leo, nimetembelea duka moja ambalo liko njia ya kuelekea nyumbani. Ni duka kubwa kidogo na wanauza vitu vingi. Jana niliomba waniuzie vocha ya Vodacom ya shs 5000 lakini hawakuwa nayo. Leo pia nilipoulizia hiyo vocha haikuwepo. Ndipo muuza duka akaamua kuniambia kuwa hawawezi kuuza aina hiyo ya vocha kwa sababu hazina wateja. Aliendelea kueleza kuwa vocha kubwa za voda walizonazo ni za shs 3000 na hazitoki kirahisi. Na kwamba Vodacom inapitwa na hata TTCL na Zantel (na hapa ni Tz bara). Kwa kadri ya maelezo ya huyo jamaa, kampuni inayoongoza ni Tigo ikifuatiwa na Zain.
Nilishangaa kiasi kwani sikutegemea kusikia kwamba Voda imefulia kiasi hicho. Ukizingatia majigambo yao yote na taarifa aliyotoa Mwamvua Makamba leo, kwamba Voda ndiyo yenye bei nafuu kuliko kampuni zote nchini. Hii kitu nilichokutana nacho ni hali halisi au ni tatizo la hapa mtaani kwetu?