Haya ni matokeo ya "huu ni wakati wetu"

Taifa_Kwanza

JF-Expert Member
Sep 3, 2010
443
86
Dhana hii imeshika mizizi ndani ya chama cha mapinduzi,
ndani ya serikali, ndani ya bunge, ndani ya baraza la mawaziri,
ndani ya familia za walio kwenye vyombo hivyo, ndugu,
jamaa na marafiki zao, kwamba hii ni zamu yao na wao kula.

Dhana hii ni pana sana lakini leo ntaigusia katika genge la wizi
lililoko nchini linaloiba mali ya uma in whole sale.

Jakaya ndio kiongozi wa genge hili ndio maana hachukui hatua
zozote zile stahiki dhidi wa wezi wote ambao UMA wa tanzania
umepata kuwabaini kwa namna moja ama nyingine.

Sababu kubwa iliyopelekea hali kufikia hapa tulipo ni kwamba,
Jakaya na genge lake na wao wanafanya kama alivyofanya
Mkapa na Genge Lake, ni nini kinasababisha wizi unaofanywa na
Genge la Jakaya ubainike na kuwa wazi zaidi, kitu kinachopelekea
kusakamwa sana tofauti na ilivyokuwa kwa Ben ni viwili
1. Kwanza ni hali halisi, mwisho wao umefika katika namna ya
"Siku ya kufa nyani miti yote uteleza"
2. Hawa wanaiba mbegu tofauti na wakati wa ben walikuwa
wakiiba mazao, wao wakala lakini na wananchi walipata chakula
pia,

Wakati wa Ben mwanya mkubwa sana wa wizi, ilikuwa na sera
ya ubinafsishaji, hapa ndio ujambazi wa kutoa machozi ulipopatia
mwanya,kuanzia kwenye ubinafsishaji wa nyumba za serikali,
mpaka kwenye ubinafsishaji wa mashirika ya uma na mchako
mzima wa privertisation of the economy ambapo ulifanyika
wizi wa kutisha pia (haya yako wazi sana katika jamii yetu sasa
hata nisipokuwa specific and detailed). Enzi za kina ben waliosikika
ni kina DR Kigoda, Sumaye, Idd Simba, Professa Mbilinyi, Magufuri,
Ben Mwenye, Mrs Ben - Ana Mkapa etc

Wizi unaofanyika sasa hauambatani na sera yoyote for a back up,
except kwa wizi ambao umeisha anza kwenye sera ya kilimo kwanza,
hawa jamaa sasa wanaiba iba tu, bila kujali, wanaiba msibani au
kwa yatima, enzi hizi ni wengi zaidi na kuibuka kwa Jairo ni taarifa
kwamba wapo wengi kama mchanga

Kwa mantiki hii, Tusitegemee kuona serious actions wala
mabadiliko ya namna yoyote mpaka hawa jamaa wamalize zamu yao.

Mbona wao walikula, na sisi hii ni zamu yetu bwana,
itaisha 2015. watanzania tuwe wavumilivu.
 
Back
Top Bottom