Haya ni mabaya ya SITTA, niwekee mazuri yake

NILIPO KUWA NIKIMTAZAMA JANA NILIPATA SHIDA KAMA KWELI HUYU NI MTU MAKINI, NILIKUWA NA KAKA YANGU MBELE YA TV, AKANIAMBIA MIMI SITTA HUWA SIMKUBALI, MIMI PIA NIKAMWAMBIA HATA MIMI SIMKUBALI ILA ACHA TUANGALIE ANASEMA NINI ILI TUMFAHAMU VIZURI. TUMEKUWA TUKISOMA HABARI NYINGI SANA JUU YA MTU HUYU KUWA NI MNAFIKI, TUMEKUWA NA SHAKA KUAMINI HAYO KWA KUWA ANATUMIA BUSARA NA AKILI KIDOGO KU-BALANCE ISSUE KIASI KUNA WATU WANAMUONA KAMA NABII na mkombozi wa kweli. KWA JANA NILIWEZA KUTHIBITISHA KUWA HUYU MTU NI HATARI NA NI MNAFIKI KWELI, TENA SINA HAJA YA KUSIKIA ANAWAAMBIA NINI WATANZANIA. NILICHOKIPENDA KWAKWE NI KIMOJA TU, YAANI KUTUONYESHA NI JINSI GANI CCM IMEHARIBIKA NA INAVYOWEZA KUTUANGAMIZA MBELENI, NIMEWEZA KUFAHAMU PIA KUWA CCM HAWAMPENDI LAKINI PIA WAPINZANI WA KWELI HAWAMPENDI! HIVYO AMEKUWA KAMA POPO, RAFIKI YANGU MMJA ALINIAMBIA NI KUNGURU! HANA NIA YA KWELI YA KUPAMBANA NA MAFISADI NA KUWA PUNGUZIA WATANZANIA GHARAMA ZA MAISHA, ANASEMA CHADEMA KULE IGUNGA WALITUMIA PROPOGANDA YA UMASIKINI WA WANANCHI KWA KU-LINK NA UTAWALA WA CCM, SIJUI SITTA UMASIKINI WA WATANZANIA YEYE ANU-LINK NA UPINZANI WA VYAMA VINGI! SITTA NAJUA UNASOMA HAYA, LA MWISHO KWAKO NI HILI, WATANZANIA WAMEKUFAHAMU KUWA SI LOLOTE SI CHOCHOTE, SASA WATANZANIA WANASEMA BORA LOWASA KULIKO WEWE! NIMESHANGAA SANA!

Unachikiona Sita anakifanya kwa uwazi ujue ndani ya CCM kunanuka kuzidi uvundo!! Sita ni mnafiki sana, na nina uhakika anataka madaraka kwa manufaa yake binafsi na si ya umma. Vita iliyopo na wenzake ni baada ya kukosa uwaziri mkuu!! Alitulia alipopewa u-spika, kinyongo kimerudi baada ya kuchezea tiktak akakosa ubunge!!!

Ni yale yale tu...
 
Ni wakati wa vita na baada ya vita.........magari yote jumapili mwisho saa 8 kuhifadhi mafuta.........amri ya serikali
Nashukuru sana,inawezekana vita ya Uganda ndiyo iliuangusha uchumi wetu?Nasikia wananchi walimbiwa "wafunge mikanda" nk.

Na bado hawajaambiwa waifungue!

Anyways nashukuru,sitaki kuwatoa kwenye mjadala wenu.Sina la maana la kusema humu kwenye hili mimi nasoma tu.
 
jombaa, ile ofisi aliyojengewa sio ya spika, ni ofisi ya mbunge. . . . .kwa hiyo wananchi wa urambo wakichagua mbunge mwingine ataitumia.
 
tatizo laki wewe mdada unawivu wakijinga na uvivu wakufikiria, hivi huoni Sitta jinsi anavyolitetea taifa sasa hivi? sahau the past, kama uliangalia ITV jana sa 3 usiku uliona jinsi anavyokataa waziwazi kulipwa kwa dowans na tena alifikia hata kuwaambia vijana kama wewe muingie barabarani kuandamana, sana unataka nini tena?
Nadhani hili jukwaa halikufai, nenda kule kwenye mahusiano na mapenzi panakuhusu sana tu.
Mbona unakuwa mwehu? Hapo uoni umeshaweka mazuri ambayo miss Marytina aliyohitaji?
 
Hua ni mnafiki SITTA ni mnafiki mkubwa,sifa yake kubwa miaka yote hakuwahi kuleta maendeleo katika jimbo lake la Urambo Mashariki.
 
Mwanangu wewe sikuwezi maana hizo picha ulikuwa mpigapicha wake nini? yaani unafaa kuwa cameraman {its jokes}
naomba unitumie picha ya nyerere alivyoweka jiwe la msingi wakati wa muungano nina shida nayo
na picha ya Petero akitembea baharini akataka kuzama pls mwanangu usiniangushe
 
tuma katika hii email pls hizo picha ya Mwl nyerere na petero pls na nyingine mtu aliyefanikiwa katika shughuli zake, na ingine ni
mtu anayeogopa kuanzisha jambo/shunguli au kitu twanga hapa digitalsimage@yahoo.com
 
nimekuwa mzito kumwelewa sitta pls nisaidieni (nionesheni tofauti ya SITTA na mafisadi)

1.ni sitta aliyeizima dowans bungeni (leo tunatakiwa kuilipa)
2.ni sitta aliyejijengea ofisi ya spika kwao (kama vile atakuwa spika milele)
3.ni sitta asiyetaka kuhama kwenye nyumba ya spika hadi leo
4.ni sitta aliyeunga mkono posho (bilioni 900 kwa mwaka)
5.ni sitta anayedai elimu bure haiwezekani (yeye alisomeshwa bure)
6.Alianzisha chama ndani ya chama na kukizima pale alipoahidiwa kuteuliwa spika kwa next term kumbe danganya toto

Nakaribisha list ya mazuri ya SITTA
1.
2.
3.
4.
5.

My take:SITTA NA LOWASSA WOTE WATATUTEKETEZA INCASE WAKIPEWA NAFASI YA URAIS,


Sita alikuwa ni swaiba mkubwa wa R. Mengi na ndiye aliyemsaidia kupata ubunge Urambo, watu wanajua sana hili, na pengine angezirai tena kama ilivyokuwa mwaka 1995 wakati tukiwa Tabora Boys. Ndiyo maana hata issue ya kushtakiwa kwa Adamu Malima bungeni Sita aliikomalia sana, na isingekuwa Lowasa wakati huo Malima angekiona cha mtema kuni, . Sita hawezi kuacha kubwabwaja tofauti na Mengi kwani mpaka sasa bado wapo chanda na pete, ndiyo maana hata kipindi cha jana kilirushwa vile. Kwa uthibitisho zaidi kampuni ya uwakili ambayo inamilikiwa na Sita ( soma hapa uifahamu Esco Law Chambers .. Advocates, Notories and Commissions of Oaths ) ndiyo tu imekuwa ikipewa kazi na IPP Media na ndiyo malawyers wao siku zote, mfano ile kesi ya ze comedy, waliwawakilisha IPP media na kesi zingine kibao. So Sita sio mtu wa kumwamini hata kidogo, yeye tu hakubahatika kujilimbikizia mali za kifisadi kwa sababu wakati wa uongozi wake sehemu alizozitaja jana alikuwa chini ya Nyerere na asingeweza fanya kitu, ila tamaa anayo na nafasi kaikosa ndiyo maana anajifanya kupinga ufisadi. Ufisadi gani anaoupinga huyu wakatyi kipindi chake NIC mwekezaji wake alikuwa ni Mengi tu!!!!!!!!?????? Ajabu sana!!!!
 
Sitta atabaki kuwa Sitta...mizani yake ya mabaya na mazuri imeelemea kwenye mazuri zaidi....ni mtu bomba...namhusudu sana!
 
1. Sitta alikuwa mwanamtandao, lakini akawageuka wenzake baada ya kugundua kuwa nia yao ya kuingia madarakani ni kufanya uporaji wa raslimali za Watanzania.
2. Akiwa Spika wa Bunge aliliendesha kwa standard and speed. Aliboresha kanuni za Bunge na kulifanya liwe la kiwango cha juu.
3. Aliunda tume na kusimamia mjadala uliosababisha kufukuzwa (sio kujiuzulu) kwa waziri mkuu.
4. Amekuwa akikemea ufisadi wazi wazi na hamuogopi mtu. Ni jasiri.
5. Anakerwa na umaskini wa Watanzania
6. Hana kashfa yoyote inayoweza kuthibitishwa zaidi ya majungu yanayoenezwa juu yake.
7. Alipinga uuzwaji wa nyumba za serikali, na yeye ni miongoni mwa vigogo ambao hawakununua nyumba hizo.

Need I say more?

Mkuu kumbe huenda ndio maana ameng'ang'ania kwenye nyumba ya spika!! Na ndio maana akajenga ofisi ya spika Urambo kwa kuwa itakuwa yake tu hadi spika mwingine atoke jimbo la Urambo!!
 
Back
Top Bottom