Haya ndiyo yatakayoiua CHADEMA

Lakini tufike mahali tukubaliane kimsingi tu kwamba GT anavuta kale ka sigara kakali
 
Kila mara inaonekana kana kwamba CHADEMA inakwenda kusambaratika, mara zote hizo ni bahati tu ya mtende inayokinusuru chama hicho kusambaratika. Ndani ya CHADEMA kuna mambo makubwa MATATU yanayokisumbua chama hicho.

Mosi: Katiba yao
PILI: Kujaza wasomi wasio wanasiasa
TATU: Oganizesheni mbovu makao makuu.

Kwa maoni yangu siyo Mbowe, Zitto wala Slaa bali ni haya mambo matatu ndiyo yatakayoiua CHADEMA.

KATIBA YA CHADEMA

Katiba hii ilipitishwa na Mkutano mkuu wa CHADEMA pale kwenye ukumbi wa PTA mwaka 2006. kwenye katiba hii mamlaka makubwa yaliwekwa kwenye mikono ya mwenyekiti na katibu wake na kurugenzi watakazo ziteua.

wakati wa kuipitisha katiba hii kwenye Baraza kuu la wakati huo wajumbe walitahadharisha kwamba mfumo wa katiba hii utaviza chama. Kina kafulila na wenzake Mnyika ndiyo walikuwa vinara wa kuitetea Katiba hiyo.

Wajumbe walimtahadharisha Mwenyekiti kwamba kuondoa ngazi ya kiutendaji ya Mkoa na kuibakisha kama ni ngazi ya kuratibu tuu bila ya kuipa nguvu ya kusimamia ngazi za Wilaya ni kuviza chama kina Danda walikuja Juu.

Kilichoonekana wakati ule ni watu wa makao makuu (Danda, Mnyika,Kafulila) kuogopa nguvu kubwa walizokuwa nazo viongozi wa mikoa kwenye vikao vya Baraza Kuu.

katiba hiyo iliwaondoa viongozi wa mikoa kuwa wajumbe wa Baraza kuu badala yake wakaingizwa viongozi (wenyeviti) wa wilaya kuwa wajumbe wa baraza hilo.

Matoke ya hali hiyo mpaka sasa hakuna kikao chochote kile cha kitaifa ambacho Makatibu wa Mikoa wa CHADEMA ambacho wao ni wajumbe. Au kwa maneno mengine Makatibu wa CHADEMA wa mikoa hawatakutana kisheria kwa miaka mitano mfululizo wakiwa ni watendeji wa chama hicho ngazi ya mkoa.

makatibu huchaguliwa na mikutano ya ngazi zao lakini huthibitishwa na baraza Kuu,chombo ambacho mpaka sasa hakijawathibitisha makatibu hawa waliochaguliwa mwaka huu. Na idadi kubwa ya makatibu wa Mikoa hawajahudhuria mkutano mkuu wa mwaka huu wa CHADEMA kwa sababu wao si wajumbe.

Katiba hii ndiyo ilisanifiwa na kina Mnyika, Kafulila na wenzao ambao leo hii wanalialia kwamba wameonewa. Imekuwa Mchimba kisima kaingia mwenyewe!!

WASOMI WASIO WANASIASA

Hili ni tatizo linatakalo watafuna sana CHADEMA, kwani kila jambo badala ya kutatuliwa kiuhalisia zinaingizwa nadharia za kiusomi. Sina maana kwamba kwenye siasa hatuhitaji wasomi, la hasha, bali tunahiktaji wasomi wanasiasa.

OGANIZESHENI MBOVU

Kutokana na Katiba yenye Utata na wasomi wasio wanasiasa, Chama cha CHADEMA kimekuwa na Oganezesheni mbovu kupita Kiasi.Pale makao makuu kila mtu anatumia rasirimali za chama kujenga chama kwenye maeneo yao wanayotoka kwa lengo la kugombea ubunge.

Kafulila wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa alikuwa Kigoma, Komu Moshi, Danda Njombe, Slaa Karatu, Kigaila Kibaigwa,Mdee kawe na hivyo chama kukosa Oganezesheni ya kitaifa kwa ajili ya uchaguzi huo.

nadiriki kusema huu ni upumbavu..yes i said it ni upumbavu..Kama wewe si mwanachama wa CHADEMA yanakuhusu nini hata ikifa.Nadhani na wewe binafsi una oganizesheni mbovu ndio maana unatumia muda wako kuchambua mambo ya chama kisichokuhusu...Iacheni CHADEMA yetu...
 
CHADEMA hailei watu wanaosumbua na mamluki kama ilivyo kwa li chama fulani hivi..linakumbatia mauozo mpaka wanaowakumbatia wanataka kukipasua chama lakini wanawang'ang'ania tu..
 
Zawadi Ngoda,
Ikiwa Mbowe alikuwa DJ, na mwenyekiti mwingine akiwa askari akiyarudi mayenu ya Mbowe kuna ubora gani kwa huyo mwenyekiti mwingine!
Ubora upo kwa huyo aliyekuwa akiyarudi. Kwa sababu katika free time, likizo au week end kila mtu hutafuta kitu nje ya profesion yake ili kutuliza akili. Wengine huenda kuogelea, wengine kuvua samaki, wengine kucheza mpira au tenis na wengine kwenda Birikana.

Lakini huyu Mbowe, U-DJ NDIO Profesion yake. Hukaa toka j'tatu mpaka ijumaa akifikiria juu ya kuboresha fani hiyo. Yeye hafanyi hivyo kama kupoza kichwa bali yupo kazini.

Kwa hiyo hata Chama anakiendesha ki-DJ, DJ. nA HATA AKIPATA NCHI ATAFANYA HIVYO HIVYO. wAUUUU!!!!!!!!
 
Ubora upo kwa huyo aliyekuwa akiyarudi. Kwa sababu katika free time, likizo au week end kila mtu hutafuta kitu nje ya profesion yake ili kutuliza akili. Wengine huenda kuogelea, wengine kuvua samaki, wengine kucheza mpira au tenis na wengine kwenda Birikana.

Lakini huyu Mbowe, U-DJ NDIO Profesion yake. Hukaa toka j'tatu mpaka ijumaa akifikiria juu ya kuboresha fani hiyo. Yeye hafanyi hivyo kama kupoza kichwa bali yupo kazini.

Kwa hiyo hata Chama anakiendesha ki-DJ, DJ. nA HATA AKIPATA NCHI ATAFANYA HIVYO HIVYO. wAUUUU!!!!!!!!
Reagan alikuwa mcheza sinema na kawa rais tena maarufu wa kusifika, iwe Mbowe...Ama kweli Miafrika bwana inaongozwa na watu wenye Phds kina Mugabe ndio kwanza matatizo yanazidi..Hata katika ndoa za kiafrika ati siku hizi watu wanatafuta mwenza mwenye Phd..
Jamanii eeeh, Ujanja kupata sii kutangulia tena!
Karagabaho!
 
Mkuu Mkandara nilikuwa sijui kama reegan alkuwa mcheza sinema..hahaaa na swazzenerger as well leo hii ni gavana huko marekani..Mitanzania ndivyo tulivyo tunapenda tuongozwe na wenye mi PhD fake kwa kuwa wengi wetu akili zetu ni fake na zinaamini kuwa ukiwa msomi basi ndo unaweza kuongoza....poor mitanzania
 
nne - udini(ukatoliki)
tano - ukabila (chagga)
Inasikitisha sana hoja hii kuendelea kuishikia bango. Kama hayo ni ya kweli, mbona Mwenyekiti Mbowe ni Mlutheri na sii mkatoliki na Katibu mkuu ni Muiraki/Mbulu(kama sikosei) na si Mchaga? Wakati mwingine tuking'ang'ania hoja za kijinga tunaweka wazi ujinga wetu.
 
Back
Top Bottom