Haya ndiyo yanayowafanya wakumbatie muswada wa katiba

Escobar

JF-Expert Member
Sep 16, 2011
574
440
Ndugu wana jopo, binadam yeyote mwenye afya akili bila kujali ni timamu au la huwa anawaza. Nimekuwa nafuatilia kwa muda mwenendo wa namna ya kuwa na katiba mpya na nimegundua kuwa mambo kadhaa yafuatayo ndiyo yanayopelekea vile tunavyovutana leo na endapo vyama vya upinzani na wanaharakati wataahidi kuyaacha kama yalivyo ninauhakika kabisa jukumu la kuandika katiba anaweza kupatiwa hata Kibamba asimamie zoezi hilo.

1. Nafasi ya mke wa rais
2. Uteuzi unaofanywa na raisi ubaki kama ulivyo na asihojiwe juu ya vigezo na sifa za wanaoteuliwa
3. Nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya
4. Tume ya uchaguzi isiguswe
5. Maslahi ya rais
6. Haja ya kuwa na Makamu wa rais na Waziri mkuu
7. Nchi moja marais 5 na waziri mkuu 1 (Tanganyika marais 2 na waziri mkuu 1, Zanzibar marais 3)
8. Kubwa kuliko yote ni Rais kushtakiwa akitoka madarakani endapo alifanya kosa enzi za utawala wake.

Mambo haya yakiondolewa kwenye mjadala wa kuandika katiba mpya i mean yakiachwa kama yalivyo yaani yasiguswe basi hapo roho za watu zitatulia na kazi hiyo watampa yeyote mwenye ufahamu aandike katiba kwanza ni kazi ngumu sana inayofikirisha mno na wataalamu wetu huwa hawana kasumba ya kuumiza vichwa sana unless kuna faida flani anapata katika hicho kitu (rejea mikataba ya madini na ufuajui umeme, inatia shaka kama ilisainiwa na watz wenye nia njema na taifa hili)
 
Wakuu wa mkoa na wilaya ni lazima wagombee. Hii tabia ya wakuu wa mkoa na wilaya kufanya mipango ili wahamishiwe maeneo mengine utaisha . Sehemu ambazo zinahitaji viongozi wazuri zinadidimia kwasababu kiongozi akifanya kazi vizuri anahamishiwa mkoa au wilaya kubwa zaidi sasa hii itaisha kama watu wanagombea kwani watakuwa wenyeji.
 
Elimu itolewe jamani kwa watu bila hivyo hii katiba itakua ya kujinufaisha kwa wao watawala mjizi sisiemu.jamani wanaharakati msikate tamaa tupo sambamba na kuupinga huo mswada.
 
Ndugu wana jopo, binadam yeyote mwenye afya akili bila kujali ni timamu au la huwa anawaza. Nimekuwa nafuatilia kwa muda mwenendo wa namna ya kuwa na katiba mpya na nimegundua kuwa mambo kadhaa yafuatayo ndiyo yanayopelekea vile tunavyovutana leo na endapo vyama vya upinzani na wanaharakati wataahidi kuyaacha kama yalivyo ninauhakika kabisa jukumu la kuandika katiba anaweza kupatiwa hata Kibamba asimamie zoezi hilo.

1. Nafasi ya mke wa rais
2. Uteuzi unaofanywa na raisi ubaki kama ulivyo na asihojiwe juu ya vigezo na sifa za wanaoteuliwa
3. Nafasi za wakuu wa mikoa na wilaya
4. Tume ya uchaguzi isiguswe
5. Maslahi ya rais
6. Haja ya kuwa na Makamu wa rais na Waziri mkuu
7. Nchi moja marais 5 na waziri mkuu 1 (Tanganyika marais 2 na waziri mkuu 1, Zanzibar marais 3)
8. Kubwa kuliko yote ni Rais kushtakiwa akitoka madarakani endapo alifanya kosa enzi za utawala wake.

Mambo haya yakiondolewa kwenye mjadala wa kuandika katiba mpya i mean yakiachwa kama yalivyo yaani yasiguswe basi hapo roho za watu zitatulia na kazi hiyo watampa yeyote mwenye ufahamu aandike katiba kwanza ni kazi ngumu sana inayofikirisha mno na wataalamu wetu huwa hawana kasumba ya kuumiza vichwa sana unless kuna faida flani anapata katika hicho kitu (rejea mikataba ya madini na ufuajui umeme, inatia shaka kama ilisainiwa na watz wenye nia njema na taifa hili)

Na ndipo vita ilipo, makelele yote yale ya JK ni kutaka haya yasiguswe ili tubaki kule kule tulipo!!!
Ningeomba wapitie kwa umakini mkubwa maoni ya kambi ya ipinzani na kuchambua hoja zao ni nini?
 
Back
Top Bottom