Nini hatima ya Lipumba vs Maalim Seif

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,829
3,159
Mchezo unaofanyika CUF ni kama mtoto aliyejiandaa kuoga nje kwenye mvua halafu akakutana na mvua ya mawe hapa lazima atameza taulo tu.

Wakuu wa bara na visiwani mtafunua funua hiyo katiba ya chama mpaka itachanika na kila mtu atakuja na tafasiri zake.

But this is just a tough political game of two mamba, mpambano wa prof. Lipumba vs Maalim Seif, wengine ni washehereshaji tu.

Sasa prof na Maalim amueni sasa aidha mkae chini wawili mjadili mustakhabali wa chama au muendelee kuwa pressurized na non-CUF's ili mkiue chama vizuri.

Ustawi wa CUF hauwezi kuletwa na mtu/watu, chama au vyama visivyo CUF hkika wana- CUF chama mlijenga wenyewe na mkicheza mtakibomoa wenyewe, msisingizie mtu.

Kuna watu walipata ulemavu na hata wengine kupoteza maisha kwa ajili ya maandamano ya CUF na hakukuwepo washereheshaji.

But today in the memory of them mnawakumbuka kwa kuwatengenezea salad ya matango na sukari kweli? Will it work?
 
JINA la Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, limeibuka katika mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF), baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kudai kwamba kuingia kwake upinzani ndiyo chanzo cha matatizo yanayoukumba upinzani hivi sasa.

Kauli hiyo ya Lipumba imeungwa mkono na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, Profesa Kitila Mkumbo, aliyesema kwamba; “Kinachoendelea sasa ni Lowassa kuwatesa viongozi wa Ukawa kama wao walivyomtesa kwa miaka mingi”.

Akizungumza katika mahojiano na Raia Mwema juzi Jumatatu, Lipumba alisema anaamini wafuasi wa CUF wanaomuunga mkono ni wale ambao wanamfahamu na hawakukubaliana na uamuzi wa chama hicho kumuunga mkono Lowassa kuwa mgombea urais wa vyama vilivyokuwa kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Tatizo la kwanza hapa ni Lowassa. Kama Lowassa asingekuja upinzani, maana yake ni kwamba vyama vya upinzani vingetumia fomula tuliyokubalina kupata mgombea. Lakini wenzetu Chadema wakamfanya kuwa mgombea wao na hatimaye wa Ukawa.

“Ni kweli kwamba mimi nilimkaribisha Lowassa kwenye upinzani lakini lengo halikuwa kwamba awe mgombea urais. Kama kule alikokuwa (CCM) aliona hapamfai na akaona atatoa mchango kwenye upinzani, sisi tusingeweza kumkataa. Lakini lengo halikuwa awe mgombea.

“Ndiyo sababu mimi na Dk. Wilbrod Slaa tukasema hapana. Mimi ni mwanasiasa lakini nina maadili. Kuna mambo siwezi kufanya hata ikiwa vipi. Mtu ambaye tumemtangaza kuwa fisadi kwa takribani miaka nane tunawezaje leo kwenda kwa wananchi na kusema huyu ndiye mbeba bendera yetu?

“Hatukusilizwa wakati tunasema hapana. Ninaamini kwamba upinzani ulifanya kosa kubwa kumkubali Lowassa wakati ule. Nilitaka kujiweka pembeni lakini wanachama wakasema Mwenyekiti unataka kuondoka lakini chama kitakufa.

“Lakini baadaye nimeanza kuona dalili za kuua CUF. Ukiona umefika wakati chama kinataka hadi kuwafuta ubunge wabunge wake ambao walipambana katika mazingira magumu kupata ubunge wao, ujue hapo kuna ajenda nyingine.

“Na ajenda yenyewe ni kuhakikisha kuwa CUF inakufa Bara na inabaki Chadema peke yake. Ndiyo sababu sishangai kwamba baadhi ya wana Chadema wamekuwa mstari wa mbele kuchochea huu mgogoro wa chama chetu utadhani wao ndiyo wana uchungu kuliko sisi.

“ Mimi nimeumizwa kwa ajili ya CUF. Nimelala jela kwa ajili ya CUF. Nimetokwa damu kwa ajili ya CUF. Leo nitakaaje pembeni huku jasho, muda na damu yangu iliyotumika kwa zaidi ya miaka 20 ikionekana kutaka kupotezwa. Ndiyo sababu nimeamua kurejea na kuirejesha CUF ile iliyokuwapo huko nyuma,” alisema mchumi mbobezi huyo wa Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani.

Uhusiano wake na Maalim Seif

Katika mahojiano yake hayo na gazeti hili, Lipumba alisema hana ugomvi binafsi na Maalim Seif bali wana tofauti za kisiasa ambazo zingeweza kumalizwa kupitia vikao vya chama pasipo tatizo lolote.

“Sikiliza, mimi na Seif tumeanza kufahamiana zaidi ya miaka 40 iliyopita. Hata huyo Julius Mtatiro (aliyeteuliwa kukaimu nafasi ya Lipumba baada ya mapinduzi ambayo sasa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema yalikuwa batili), alikuwa hajazaliwa wakati nakutana na Maalim.

“Maalim tumeanza kufahamiana mwaka 1973 wakati tukiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Mimi nilikuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa chama cha TANU na yeye alikuwa kiongozi wa wanafunzi waliotoka Zanzibar kuja kusoma Chuo Kikuu.

“Sina ugomvi binafsi na Maalim na ndiyo maana nawahurumia vijana ambao wamejiingiza katika mambo haya. Nadhani tatizo ambalo Maalim Seif analo sasa ni kwamba amekubali kuzungukwa na watu wenye siasa zisizotaka Muungano. Kule Zanzibar amezungukwa na ma-Nationalist (wanaotaka Zanzibar ijiondoe kwenye Muungano).

“ Kama utakumbuka, kwenye Bunge la Katiba, mimi nilieleza msimamo wa chama ambao ni serikali tatu. Lakini Maalim Seif alizungumza kuhusu Muungano wa Mkataba ambao si msimamo rasmi wa chama. Lakini amezungukwa na watu wasiotaka Muungano na hivyo kuna mvutano kidogo.

“ Pengine hao ndiyo wanaomshauri kwamba CUF itumie nguvu zake Zanzibar tu na haina sababu ya kuhangaika na Tanzania Bara. Kwamba CUF kiwe Zanzibar na Chadema ishike Bara. Ndiyo maana hajali kuona wabunge wetu wakifukuzwa uanachama. Hawana shida tena na Bara.

“ Nadhani hapa ndipo tofauti ilipo. Lakini hizi ni tofauti ambazo zinaweza kumalizwa kupitia vikao. Msimamo huo wa watu wa karibu na Seif unaungwa mkono na Chadema kwa sababu watafaidika na hali hiyo.

“ Mbaya zaidi ni kwamba Chadema hawataki Lipumba awe Mwenyekiti wa CUF. Wao wanajua kwamba wamewafanyia dhuluma Watanzania kwa kumfanya Lowassa kuwa mgombea urais. Wanajua kuna wana Chadema wanaoniunga mkono na nikianza kukijenga upya chama changu, nitavuna wafuasi hata kutoka kwao na utakuwa mwisho wa michezo waliyotufanyia mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Kuhusu ruzuku

Kutokana na matatizo yaliyopo sasa kwenye chama hicho, kuna utata kuhusu ni wapi hasa ruzuku ya chama hicho italipwa miongoni mwa kambi hasimu zilizopo. Kuna kundi linaloongozwa na Lipumba na lile la Seif.

Alipoulizwa kuhusu hilo, Lipumba alisema hakuwa amewaza kuhusu jambo hilo lakini akasema ni suala ambalo linaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka na vyombo vilivyo ndani ya chama hicho. Kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, Katibu Mkuu ndiye mtia saini wa malipo ya chama hicho na anapokuwa hayupo, Naibu Katibu Mkuu anaweza kutekeleza jukumu hilo.

Kwa upande wake, Mtatiro amesema kwamba Lipumba hataweza tena kuongoza chama hicho kwa sababu amepoteza ushawishi miongoni mwa wanachama wa chama hicho pamoja na vyombo vya uamuzi vya chama hicho.

“Kama mlivyoona wakati wa kikao cha Baraza Kuu, zaidi ya nusu ya wajumbe hawamtaki Lipumba. Kwenye Kamati Kuu ana watu wawili wanaomuunga mkono. Wabunge wanaomuunga mkono hawazidi nane. Sasa huyu atakuwaje mwenyekiti wa taifa wa chama?,” alihoji.

Mtatiro pia amepinga uamuzi wa Jaji Mutungi wa kumrejesha Lipumba kwenye nafasi yake hiyo, akisema hakuna sheria nchini inayomruhusu msajili kuhoji au kuingilia mambo ambayo yameamuliwa na vikao halali vya chama.

Hata hivyo, Jumatatu wiki hii, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa taarifa mahsusi ambayo, pamoja na mambo mengine, iliweka bayana mamlaka ya msajili huo anavyoweza kuratibu shughuli za vyama vya siasa.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa vyama Dk. Francis Mutungi ilieleza; “Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawaasa viongozi wa kitaifa wa chama cha CUF, kusoma kwa makini msimamo uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuuheshimu, kwani kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Msajili wa Vyama vya Siasa anao wajibu wa kujiridhisha kwamba, mabadiliko yoyote yaliyofanywa katika uongozi wa taifa wa chama cha siasa, ni halali na yamefanywa na mamlaka halali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika.”

Katika andishi lake refu alilolitoa kupitia gazeti hili, Profesa Mkumbo amesema kwamba tatizo linalosababisha migogoro katika vyama vya siasa nchini ni kwa viongozi na vyama vyao kutazama watu na si misingi iliyosababisha kuanzishwa kwa vyama hivyo.

Alisema kimsingi, mgogoro wa sasa wa CUF umesababishwa na uamuzi wa vyama hivyo kumpokea Lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais; wakati vilitumia muda mrefu kumtukana na kumdhalilisha kuwa ni fisadi katika kipindi kirefu huko nyuma.

“Hivyo basi, uamuzi wa kujiuzulu kwa Profesa Lipumba ulijengwa katika misingi ya kuanzishwa kwa Ukawa. Hata hivyo viongozi wenzake waliamua kumeza maneno yao ya miaka mingi na kumkumbatia Lowassa wakiamini kwamba angewawezesha kushinda nafasi ya urais, kitu ambacho kingefuta fedheha ya kumkaribisha ndani ya Ukawa. Hili halikutokea kwa sababu Lowassa hakushinda nafasi ya urais. Ndiyo kusema, katika hali ya kawaida, ile fedheha ilibaki ndani ya viongozi wa Ukawa,” alisema
 
UMECHANGANYIKIWA hujui lipi uamini na lipi usiliamini katika mgogoro unaoendelea ndani ya chama cha upinzani cha CUF? Hauko peke yako. Hata mimi, nazidi kutatanishwa.

Swali moja la msingi sana ambalo nimejiuliza ni je, ni kweli Profesa Lipumba ni msaliti aliyenunuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuleta fujo ndani ya CUF, kama wanavyodai wapinzani wake?

Kumekuwa na ushabiki mkubwa sana katika kulizungumzia suala hili, mara nyingi watu wakiunga mkono upande mmoja au mwingine kutokana na mapenzi na ushabiki, kama ule wa Simba na Yanga.

Hata hivyo, habari ya kambi moja ya vyama vya siasa kutuhumu kambi nyingine kuwa imehongwa imezoeleka sana katika siasa za Tanzania na kwa hiyo hili ni suala la kutazamwa kwa tahadhari, hasa linapotoka kwa watu ambao uongo ni sehemu ya kazi yao.

Ukiangalia historia ya chama cha CUF, wanachama waandamizi wengi wamewahi kutimuliwa au kulazimika kujiondoa baada ya kutuhumiwa kuwa ni wasaliti walionunuliwa na chama tawala, baadhi yao ni Profesa Abdallah Safari na Hamad Rashid na wengine wengi kabla ya hao.

Katika vyama vingine, hali imekuwa hiyo hiyo. Watu wamekuwa wakituhumiana kwa usaliti, ambao mara nyingi hujitokeza pale watu wanapohoji masuala ya msingi au kutangaza nia ya kugombea nafasi za juu zenye wenyewe.

Si hivyo tu, hata hoja zinazotajwa za kuwatia hatiani wanaoitwa wasaliti ni dhaifu. Kwa mfano, inaweza kutajwa kuwa mtuhumiwa alionekana akizungumza na kiongozi wa CCM au kanunua nyumba mpya, gari na kadhalika.

Katika suala hili la Profesa Lipumba, kuna hoja mpya imeibuka. Kwamba, vyama vya CCM na ACT wanashangilia au hata kumsaidia. Hoja hii ina udhaifu kwa sababu pindi taasisi moja ikikumbwa na mgogoro, ni jambo la kawaida mpinzani kufurahia na kuunga mkono upande mmoja ambao maslahi yao yameelemea au tu ili mgogoro uzidi kukolea. Hata Maalim Seif naye anaungwa mkono na Chadema.

Ijulikane kuwa mgogoro wa CUF ni nafuu kubwa kwa chama tawala na serikali yake kule Zanzibar kwa sababu unasaidia kupata hoja za kumshambulia Maalim Seif anayejinasibu na demokrasia na utawala wa bora unaozingatia sheria.

Pia, CCM wana haki ya kushangilia kwa sababu ushindi wa Profesa Lipumba unamuondoa Maalim Seif katika mambo ya msingi ya kupigania ‘ushindi’ wao Zanzibar. Ingawa, adui wa adui anakuwa rafiki, lakini halithibitishi kuwa Profesa Lipumba kalipwa.

Kimsingi CUF ya Lipumba huku bara wana madai ya msingi. Kwa miaka mingi, baadhi ya wanachama wa CUF wamekuwa wakilalamika kukosekana uwekezaji wa kutosha wa kuendeleza chama huku bara. Kama hilo halitoshi, malalamiko ya safari hii ni zaidi ya mambo ya kiutawala na mgawanyo wa fedha wa kuendesha chama.

Safari hii malalamiko yanahusu falsafa na ajenda za chama kutokana na muungano wa Ukawa. CUF -Lipumba wanaamini muungano huo umevuruga malengo ya chama na kukitoa upande wa bara kafara kwa Chadema.

Tukirudi katika suala la msingi, kahongwa au hakuhongwa. Binafsi naamini kuwa kwanza, si sahihi kutoa madai kama haya bila ushahidi. Pili, kilicho dhahiri ni kuwa hata kama Profesa Lipumba angekuwa amehongwa, wafuasi wake wanaamini wa dhati katika mapambano anayoyaendesha.

Mmoja wa wafuasi wa Profesa Lipumba alinipigia simu kuhusu makala yangu ya wiki iliyopita niliyohoji Profesa Lipumba kuendelea kung’ang’ania uenyekiti hata baada kuharibiwa jina kwa kutuhumiwa kupanga utekaji.

Mfuasi yule alidai walimuomba Profesa Lipumba arudi CUF ili kukirudishia chama hicho hadhi na nafasi yake iliyotwaliwa na Chadema, kama chama cha kikuu cha upinzani, ingawa kipindi CUF ikiwa chama kikuu cha upinzani, mchango mkubwa bado ulitoka visiwani.

Ukiacha uchaguzi wa mwaka jana ilipopata viti 10 bara vya ubunge, CUF haijawahi kuchukua viti zaidi ya viwili.

Jambo moja alilomalizia mfuasi yule wa Profesa Lipumba ni kurudisha tuhuma za kuhongwa kwa Maalim Seif. Akaniambia; “Wewe hushangai alikuwa akifanya mazungumzo yeye peke yake dhidi ya viongozi sita wa CCM na amekuwa akienda Chadema peke yake, pana nini hapo kama si rushwa?”

Tuendelee kufuatilia mchezo utaishaje. Watagawana mbao? Nilichojifunza wiki iliyopita ni kuwa Maalim Seif atakuwa amefanya kosa kudharau nguvu ya Profesa Lipumba ambaye anakubalika kule chini kwa watu ambao hawapo mitandoni hususan sasa baada ya kurudishiwa uenyekiti na msajili wa vyama na ukizingatia kuwa aliapa kutotoka CUF ng’o.

Raia Mwema
 
Almost 9 years wimbo wa Lowasa fisadi pasipo kuchukuliwa hatua yoyote (this is the shame to the Government).
Mtu mwenye maadili ya uongozi hawezi kushirikiana hata chembe na kile anachoamini ni kinyume cha maadili. Lipumba anasema ana maadili yet alitaka Lowasa asiwe mgombea bali aongeze tu nguvu, same man anaye muona fisadi!!! Maadili ya wapi !!! Lipumba amerudi kulipa kisasi just wakose wote,period.
 
Kumbe Inshu ni yeye kupigwa kuwekwa maabusu na damu yake kumtoka kisa CUF ndio mana anaamini ni chama chake atakachofanya vyovyote atakavyo?:(:(:(:(
 
Miongon mwa maprofesa wasio jierew huyu ni namba moja anataka kutugombnisha kwa kipenda kwake madaraka bila kuyaweza iv lipumba angesimama uraisi ukawa hata kula milion tungepata?
 
Awalaumu walimu wake waliomfundisha undumila kuwili maana walimpodoa ubongo na alipondoka kweli, vitendo vyake havidanganyi.
 
JINA la Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, limeibuka katika mgogoro unaokikabili Chama cha Wananchi (CUF), baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kudai kwamba kuingia kwake upinzani ndiyo chanzo cha matatizo yanayoukumba upinzani hivi sasa.

Kauli hiyo ya Lipumba imeungwa mkono na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini, Profesa Kitila Mkumbo, aliyesema kwamba; “Kinachoendelea sasa ni Lowassa kuwatesa viongozi wa Ukawa kama wao walivyomtesa kwa miaka mingi”.

Akizungumza katika mahojiano na Raia Mwema juzi Jumatatu, Lipumba alisema anaamini wafuasi wa CUF wanaomuunga mkono ni wale ambao wanamfahamu na hawakukubaliana na uamuzi wa chama hicho kumuunga mkono Lowassa kuwa mgombea urais wa vyama vilivyokuwa kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

“Tatizo la kwanza hapa ni Lowassa. Kama Lowassa asingekuja upinzani, maana yake ni kwamba vyama vya upinzani vingetumia fomula tuliyokubalina kupata mgombea. Lakini wenzetu Chadema wakamfanya kuwa mgombea wao na hatimaye wa Ukawa.

“Ni kweli kwamba mimi nilimkaribisha Lowassa kwenye upinzani lakini lengo halikuwa kwamba awe mgombea urais. Kama kule alikokuwa (CCM) aliona hapamfai na akaona atatoa mchango kwenye upinzani, sisi tusingeweza kumkataa. Lakini lengo halikuwa awe mgombea.

“Ndiyo sababu mimi na Dk. Wilbrod Slaa tukasema hapana. Mimi ni mwanasiasa lakini nina maadili. Kuna mambo siwezi kufanya hata ikiwa vipi. Mtu ambaye tumemtangaza kuwa fisadi kwa takribani miaka nane tunawezaje leo kwenda kwa wananchi na kusema huyu ndiye mbeba bendera yetu?

“Hatukusilizwa wakati tunasema hapana. Ninaamini kwamba upinzani ulifanya kosa kubwa kumkubali Lowassa wakati ule. Nilitaka kujiweka pembeni lakini wanachama wakasema Mwenyekiti unataka kuondoka lakini chama kitakufa.

“Lakini baadaye nimeanza kuona dalili za kuua CUF. Ukiona umefika wakati chama kinataka hadi kuwafuta ubunge wabunge wake ambao walipambana katika mazingira magumu kupata ubunge wao, ujue hapo kuna ajenda nyingine.

“Na ajenda yenyewe ni kuhakikisha kuwa CUF inakufa Bara na inabaki Chadema peke yake. Ndiyo sababu sishangai kwamba baadhi ya wana Chadema wamekuwa mstari wa mbele kuchochea huu mgogoro wa chama chetu utadhani wao ndiyo wana uchungu kuliko sisi.

“ Mimi nimeumizwa kwa ajili ya CUF. Nimelala jela kwa ajili ya CUF. Nimetokwa damu kwa ajili ya CUF. Leo nitakaaje pembeni huku jasho, muda na damu yangu iliyotumika kwa zaidi ya miaka 20 ikionekana kutaka kupotezwa. Ndiyo sababu nimeamua kurejea na kuirejesha CUF ile iliyokuwapo huko nyuma,” alisema mchumi mbobezi huyo wa Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani.

Uhusiano wake na Maalim Seif

Katika mahojiano yake hayo na gazeti hili, Lipumba alisema hana ugomvi binafsi na Maalim Seif bali wana tofauti za kisiasa ambazo zingeweza kumalizwa kupitia vikao vya chama pasipo tatizo lolote.

“Sikiliza, mimi na Seif tumeanza kufahamiana zaidi ya miaka 40 iliyopita. Hata huyo Julius Mtatiro (aliyeteuliwa kukaimu nafasi ya Lipumba baada ya mapinduzi ambayo sasa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema yalikuwa batili), alikuwa hajazaliwa wakati nakutana na Maalim.

“Maalim tumeanza kufahamiana mwaka 1973 wakati tukiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Mimi nilikuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa chama cha TANU na yeye alikuwa kiongozi wa wanafunzi waliotoka Zanzibar kuja kusoma Chuo Kikuu.

“Sina ugomvi binafsi na Maalim na ndiyo maana nawahurumia vijana ambao wamejiingiza katika mambo haya. Nadhani tatizo ambalo Maalim Seif analo sasa ni kwamba amekubali kuzungukwa na watu wenye siasa zisizotaka Muungano. Kule Zanzibar amezungukwa na ma-Nationalist (wanaotaka Zanzibar ijiondoe kwenye Muungano).

“ Kama utakumbuka, kwenye Bunge la Katiba, mimi nilieleza msimamo wa chama ambao ni serikali tatu. Lakini Maalim Seif alizungumza kuhusu Muungano wa Mkataba ambao si msimamo rasmi wa chama. Lakini amezungukwa na watu wasiotaka Muungano na hivyo kuna mvutano kidogo.

“ Pengine hao ndiyo wanaomshauri kwamba CUF itumie nguvu zake Zanzibar tu na haina sababu ya kuhangaika na Tanzania Bara. Kwamba CUF kiwe Zanzibar na Chadema ishike Bara. Ndiyo maana hajali kuona wabunge wetu wakifukuzwa uanachama. Hawana shida tena na Bara.

“ Nadhani hapa ndipo tofauti ilipo. Lakini hizi ni tofauti ambazo zinaweza kumalizwa kupitia vikao. Msimamo huo wa watu wa karibu na Seif unaungwa mkono na Chadema kwa sababu watafaidika na hali hiyo.

“ Mbaya zaidi ni kwamba Chadema hawataki Lipumba awe Mwenyekiti wa CUF. Wao wanajua kwamba wamewafanyia dhuluma Watanzania kwa kumfanya Lowassa kuwa mgombea urais. Wanajua kuna wana Chadema wanaoniunga mkono na nikianza kukijenga upya chama changu, nitavuna wafuasi hata kutoka kwao na utakuwa mwisho wa michezo waliyotufanyia mwaka 2015 kwenye Uchaguzi Mkuu,” alisema.

Kuhusu ruzuku

Kutokana na matatizo yaliyopo sasa kwenye chama hicho, kuna utata kuhusu ni wapi hasa ruzuku ya chama hicho italipwa miongoni mwa kambi hasimu zilizopo. Kuna kundi linaloongozwa na Lipumba na lile la Seif.

Alipoulizwa kuhusu hilo, Lipumba alisema hakuwa amewaza kuhusu jambo hilo lakini akasema ni suala ambalo linaweza kupatiwa ufumbuzi wa haraka na vyombo vilivyo ndani ya chama hicho. Kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho, Katibu Mkuu ndiye mtia saini wa malipo ya chama hicho na anapokuwa hayupo, Naibu Katibu Mkuu anaweza kutekeleza jukumu hilo.

Kwa upande wake, Mtatiro amesema kwamba Lipumba hataweza tena kuongoza chama hicho kwa sababu amepoteza ushawishi miongoni mwa wanachama wa chama hicho pamoja na vyombo vya uamuzi vya chama hicho.

“Kama mlivyoona wakati wa kikao cha Baraza Kuu, zaidi ya nusu ya wajumbe hawamtaki Lipumba. Kwenye Kamati Kuu ana watu wawili wanaomuunga mkono. Wabunge wanaomuunga mkono hawazidi nane. Sasa huyu atakuwaje mwenyekiti wa taifa wa chama?,” alihoji.

Mtatiro pia amepinga uamuzi wa Jaji Mutungi wa kumrejesha Lipumba kwenye nafasi yake hiyo, akisema hakuna sheria nchini inayomruhusu msajili kuhoji au kuingilia mambo ambayo yameamuliwa na vikao halali vya chama.

Hata hivyo, Jumatatu wiki hii, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa taarifa mahsusi ambayo, pamoja na mambo mengine, iliweka bayana mamlaka ya msajili huo anavyoweza kuratibu shughuli za vyama vya siasa.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Sisty Nyahoza kwa niaba ya Msajili wa vyama Dk. Francis Mutungi ilieleza; “Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inawaasa viongozi wa kitaifa wa chama cha CUF, kusoma kwa makini msimamo uliotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa na kuuheshimu, kwani kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Msajili wa Vyama vya Siasa anao wajibu wa kujiridhisha kwamba, mabadiliko yoyote yaliyofanywa katika uongozi wa taifa wa chama cha siasa, ni halali na yamefanywa na mamlaka halali kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za chama husika.”

Katika andishi lake refu alilolitoa kupitia gazeti hili, Profesa Mkumbo amesema kwamba tatizo linalosababisha migogoro katika vyama vya siasa nchini ni kwa viongozi na vyama vyao kutazama watu na si misingi iliyosababisha kuanzishwa kwa vyama hivyo.

Alisema kimsingi, mgogoro wa sasa wa CUF umesababishwa na uamuzi wa vyama hivyo kumpokea Lowassa na kumfanya kuwa mgombea urais; wakati vilitumia muda mrefu kumtukana na kumdhalilisha kuwa ni fisadi katika kipindi kirefu huko nyuma.

“Hivyo basi, uamuzi wa kujiuzulu kwa Profesa Lipumba ulijengwa katika misingi ya kuanzishwa kwa Ukawa. Hata hivyo viongozi wenzake waliamua kumeza maneno yao ya miaka mingi na kumkumbatia Lowassa wakiamini kwamba angewawezesha kushinda nafasi ya urais, kitu ambacho kingefuta fedheha ya kumkaribisha ndani ya Ukawa. Hili halikutokea kwa sababu Lowassa hakushinda nafasi ya urais. Ndiyo kusema, katika hali ya kawaida, ile fedheha ilibaki ndani ya viongozi wa Ukawa,” alisema
maprofesa wa Kitanzania buana!
 
Simuamini kabisa Lipumba hivi mnakumbuka alivyohutubia msikitini kwamba bila yeye na waislam kuweka mikakati thabiti kwny uchaguzi wa 2010 JK asingerudi ikulu kwny mhula wa pili ....Lipumba ni nyoka tena mwenye sumu Kali
 
Siku Mungu anamchukua Mzee Lowasa nadhani Tanzania itageuka Luxembourg ndani ya mwaka mmoja maana inaelekea Lowasa ndio mchawi wetu kila Zigo anabebeshwa yeye

Kwa hiyo Prof Lipumba unasema mtu hana maadili kateuliwa kugombea uraisi ila ulikubali aje kama asingeteuliwa kuwa mgombea Urais

Fair enough tuseme asingeteuliwa ndio angekuwa na maadili ?

Nilikua na mpango wa kuongeza elimu ila kila kukicha napata sababu ya kutofanya hivyo hasa nikiangalia hawa Maprofesa tulionao
 
Ndio hapo wengine walipoteza maisha sasa huyu kingangani alijiuzulu kwa hiyari yake Leo anataka kuvuruga chama ajue hana ubavu walishindwa wengi je yeye ataweza kama anaona walomtuma watamsaidia nakuapia tutamtia wazimu aende uchi Barbarani na huamini utaona
 
Almost 9 years wimbo wa Lowasa fisadi pasipo kuchukuliwa hatua yoyote (this is the shame to the Government).
Mtu mwenye maadili ya uongozi hawezi kushirikiana hata chembe na kile anachoamini ni kinyume cha maadili. Lipumba anasema ana maadili yet alitaka Lowasa asiwe mgombea bali aongeze tu nguvu, same man anaye muona fisadi!!! Maadili ya wapi !!! Lipumba amerudi kulipa kisasi just wakose wote,period.
Aliemtaja na kumtangaza kuwa fisadi si ndio aliemuweka kugombea urais?
Halafu kuthibitisha undumilakuwili wake anasema alie na ushahidi aende mahakamani wakati miaka yote alisema na kusisitiza ushahidi anao ila udhaifu wa serikali ndio tatizo
 
Back
Top Bottom