Haya ndio Mapinduzi ya Zanzibar, yamerikodiwa live na waitaliano 1964

Wickama,

Salaam ndugu yangu.

Haina neno,kama siku zoote nisemavyo yakuwa sisi soote ni wamoja.

Ndo maana pia ni uzuri kuambiana kweli pale inapojiri.

Vipi Mfalme Obama kishaingia hapo,je atafika Mtae!?ahahaa!

Siku njema.

Ahsanta.

Ustadh huku labda aje na zile APACHE helikopers, kwa yeye atavaa T-shirt kwa hali ya hewa lakini kwa wenzangu wa Bongo watavaa Maka-buti hahahahah

karibu bwana
 
Wickama

Faza; Hapa kwa kweli mimi Napata Darsa ya kunisaidia kuwaelewa huko mliko kwa hiyo wajibu wangu mkubwa kwanza ni kusikiliza tuu.

shukran sana

sawa mkuu wewe sikiliza tu , ukiwa na suala uliza wamo humu watakaokupa jawabu uruwa kabisa

tatizo ni pale mtu mkimya akianza kuzungumza

wazanzibar tumevumilia kwa miaka 50, tumenyamaza ijapokuwa tunaumia roho

leo usijali maandishi ya humu kaka, hapa tunazungumza sisi wasomi wenye maisha yetu , nenda unguja au pemba uingie dala dala zetu uwasikilie raia walala hoi wanavosema, utajuwa kweli sasa watu wamechoka......nyinyi watanganyika mutakiwa kujuwa kwamba mukila na kipofu usimshike mkono ....atajuwa kwamba upoo...au vipi
 
Kazi kweli kweli. Haya niombee Mungu Inshallah siku moja nitafika. Ila sijui mtaniita vipi? Mtanganyika PORI? hahahahah
 
Kazi kweli kweli. Haya niombee Mungu Inshallah siku moja nitafika. Ila sijui mtaniita vipi? Mtanganyika PORI? hahahahah

mbona hamna neno kaka, labda uende umevaa shati lenye chapa ya ccm, ndio kidogo wanaweza kukuona umeanza kuuguwa uchizi
 
mbona hamna neno kaka, labda uende umevaa shati lenye chapa ya ccm, ndio kidogo wanaweza kukuona umeanza kuuguwa uchizi

Ahhhh, haitagomba kwa vile rais wa zenj naye anayavaa na antoka huko basi tutampa kampani hahahah, machizi kama wanatukana waanzie wakwao.
 
RED Xs

Sikusema kwamba zanzibar ni sawa na uarabuni, ukiwa utarejea makala zangu utakuta ninsema znz ni sehemu ya watu mchanganyiko. na sisi shatujisikii katik auafrika kama munavojisikia nyinyi huko tanganyika.

Ikiwa Marco Polo kasema kweli basi hiyo ni kuonesha dhahiri kwamba zanzibar ilikuwa ni sehemu ya watu mnyanganyiko tangu siku hizo......sababu mtu mweusi + nywele za singa nadhani mtu huyu anaweza kuitwa chotara..........mix ...kwani mwafrika ana nywele kipilipili.

Kumumbuka tu kwamba marko Polo alikuwa zanizbar mnano mwaka 1295.

sijui point yako hasa hapa uliposema mwarabu anakuwa mwarabu tu kwanza sababu ya lugha...........lakini nitapenda nisikubaliane na wewe kwamba lugha ndio inayompa mtu kabila yake..... ninao marafiki kibao tu hapo dar wenye asili za kinyamwezi, kichaga na kabila nyenginezo za mikoani lakini hawazungumzi lugha zao za kikabila, pengine na wewe ni mmoja katika kundi hilo. lakini bado huniambie mimi ni mchaga au mnyamwezi au kabila ingine lakini nimezaliwa na kukuwa dar siongei kiluga. sasa jee na hao utawasema sio watu wa kabial hizo kwasababu hawaongeo lugha za kabila zao......????

Pia sipendi ufikiri kamba labda hao waafrika waliokuwepo zanzibar miaka hiyo walipofika wasafiri wa kiarabu kama vile Masuud mwaka 916 walikuwa watanganyika. No walikuwa ni wazanzibari, na watanganyika walikuwa watanganyika ijapokuwa nchi 2 hizi zilikuwa na maina tofauti siku hizo

Kiarabu hakifanywa lugha kuu ya kwa zenj empire nadhani walikuwa na sababu hizo hizo kama waliokuwanazo wazungu waliokwenda kule afrika kusini........huku kwetu wakafanya lugha ya kiswahili ...mix kibantu + kiarabu..........kule afrika kusini wakafanya lugha ya Afrikaans..........mix lugha za kizulu + kidachi

Kitabu kizuri sana hiki, utaona mambo mengi ambayo watu wanapenda kudanganyana kila siku juu yao
..lol..nashukuru kaka..tutaendelea siku ingine na mjadala wetu..nimebanwa na pilika..insha allah ramadhani njema..!
 
Haya mapinduzi ya Zanzibar tuliwahi kuyajadili kwa kina sana hapa jamvini miaka takriban saba iliyopita na tukaweka video pamoja na documents nyingi sana. Ingekuwa ni vizuri MODERETA akarahisisha kazi ya kutafiti topiki kusudi wachangiaji wapya wawe wanaongezea kwenye topiki iliyopo badala ya kuanzisha thread mpya. Mambo mengi yaliyoandikwa hapa yaliwahi kujadiliwa na kupatia maelezo ya kina huko nyuma. Najua waanzisha mada ni watu waliojiunga na jamvi hili miaka michache iliyopita, lakini si vizuri kuanzisha thread kiholela badala ya kuendeleza zile zilizoko.
 
mi nafikiri hizi video zinaweza kuleta tafsiri ya huruma kwa wale walioathiriwa na mapinduzi. lakini ktuoka moyoni bado naamini kulikuwa na uhalali wa kufanya mabadiliko ya kisiasa zanzibar wakati ule. na kwa vile udhalimu haukuruhusu mabadiliko ya amani mapinduzi yasinge epukika. madhambi yaliyofanywa na waarabu kuwakamata, kuwatesa na kuwatumikisha weusi kama watumwa lazima yangelipwa tu hata na vitukuu vya waarabu husika. unyanyasaji wa hali ya juu kufanywa na serikali ya Jamshid ndani ya mwezi mmoja baada ya uhuru ulitosha kuiondoa serikali yoyote madarakani. mfano kukamata, kutesa na kufungia wapinzani, kufungia magazeti yanayokosoa serikali, kufukuza kazi polisi wote wenye aasili ya bara na kushindwa kurekebisha mgawanyo wa ardhi wa kibaguzi uliokuwepo ni miongoni mwa uhuni uliofanywa na serikali ilyokabidhiwa uhuru desemba 1963.
Du!, kumbe inawezekana kabisa yale Mapinduzi ya Zanzibar sii mapinduzi tuu, bali ni Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yaliyoleta utukufu fulani?!.

Pasco
 
Shukran sana;

1. Video ya kwanza yenye mauaji na maiti makaburini ni ya rangi. 1964 ni vigumu kikundi cha kiitalia kuwa na colored videography ya ku-shoot zenj

2. Ukiiangalia hiyo helikopta kuna mahali wanatupa kitambaa cheupe, Chanini?

3. Makaburini maiti wamepangwa na wengi wana kofia zao vichwani!!!!

4. Mtangazaji anazungumza Nyerere, Rais Tanzania wakati hakukuwa na Tanzania wakati wa Mapinduzi hayo

5. Maiti wote wameuliwa chini ya MTI wa KIVULI!!!!!!! wamelaliana bila dalili za kukurupuka kuhami maisha yao. Wamefia kivulini!!!!!!

6. Kaburi lilichimbwa siku gani? ya kupindua au kabla au baada? na ukiyaangalia yamefuatana.

7. Angalieni mengine na nyie.
Mkuu Wickama asante kusaidia kwenye hili, vinginevyo watu wanalishwa urongo humu mchana kweupe na wanaingia kichwa kichwa!, wazima wazima wanaingizwa chaka!.

Thanks.

Pasco
 
mi nafikiri hizi video zinaweza kuleta tafsiri ya huruma kwa wale walioathiriwa na mapinduzi. lakini ktuoka moyoni bado naamini kulikuwa na uhalali wa kufanya mabadiliko ya kisiasa zanzibar wakati ule. na kwa vile udhalimu haukuruhusu mabadiliko ya amani mapinduzi yasinge epukika. madhambi yaliyofanywa na waarabu kuwakamata, kuwatesa na kuwatumikisha weusi kama watumwa lazima yangelipwa tu hata na vitukuu vya waarabu husika. unyanyasaji wa hali ya juu kufanywa na serikali ya Jamshid ndani ya mwezi mmoja baada ya uhuru ulitosha kuiondoa serikali yoyote madarakani. mfano kukamata, kutesa na kufungia wapinzani, kufungia magazeti yanayokosoa serikali, kufukuza kazi polisi wote wenye aasili ya bara na kushindwa kurekebisha mgawanyo wa ardhi wa kibaguzi uliokuwepo ni miongoni mwa uhuni uliofanywa na serikali ilyokabidhiwa uhuru desemba 1963.
Weye ni ktk wale majuha mnaodanganywa kuukataa ukweli, lete ushahidi kuhs ayo usemayo, aya mambo ya mauwaji ya waarabu sisi tulishayasikia zamani ktk kwa mababu zetu na ukweli ulifichwa na ukageuzwa na mpaka history maskuli hausomeshwi ukweli, mnaodanganyika ni mbumbumbu kama ivo nyie, biashara ya watumwa ilifanywa na wazungu tafuta ukweli usome acha kupotolewa
 
Hizi ni sinema za kutungwa kutengeneza propaganda.
BADO TULIO YASHUHUDIA MAPINDUZI HATUJAFA. YALIOLEZWA HUMO SIO TU NI UKWELI BALI NI CHEMBE NDOGO SANA TU YA YALE WALIOYAONA

NAKUMBUKA VIVIDLY TANGAZO LA REDIO KUKEMEA NDEGE KADHAA ZILIZOKUWA ZINARUKA KWENYE ANGA YA ZANZIBAR. WAKATI HUO SIKUJUA TU NINI KINAENDELEA KUTOKANA UMRI WANGU. NILISIKIA PIA WAKITAKIWA WAPIGANAJI WASIWADHURU WAZUNGU. HILI NILILIJUA KUWA KUNA MELI YA KIJESHI YA MAREKANI IMEEGESHA KUJA KJUCHUKUA RAIA ZAKE. hakuna cha kutungwahapa. Moja ya kaburi kubwa la halaiki liko kibanda maiti, sasa umegeuzwa jina uwanja wa demokrasia,na sisi wenyeji tunapaita makaburi msafa. Msichangie jambo msililijua. ACHENI TUMALIZIKE,TENA MNAWEZA KUTUNGA HADITHI MZITAKAZO NA KUZIHAKIKI DODOMA. VUTENI SUBIRA KWANZA.
 
Uongo mtupu na povu jingi.
 
Hakika napenda sana kusoma news aina hii.kwanza natoa pongezi sana kwa mleta uzi na pia kwa wachangiaji wote.hongereni sana kwa ilmu yenu tamu.la mwisho ningependa kusema WANZANZIBAR WACHACHE WAPO HAWAJIELEWI NA NDIO WANAORUDISHA NYUMA UHURU WAO.poleni sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom