Haya ndio majibu ya Serikali kwa madaktari!...Inahuzunisha sana!

Kuna haja ya kurudisha heshima kiumeni .......... Its high time wenye inji yao wajue what ua capable of doing..... Msirudi nyuma na kwa umoja wenu mtafanikiwa kupata haki yenu!
 
Madaktari poleni sana kwa kazi ngumu mnazofanya za kupigania maisha yetu walalahoi kila siku iendayo kwa Mungu na katika mazingira magumu. Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu hili sakata kati yenu na serikali kwa muda mrefu sasa.
Kwa kweli madaktari mnaonyesha uvumilivu wa hali ya juu sana zaidi ya ukomavu wa kawaida. Sielewi hii inasababishwa na feeling zenu kwa wagonjwa au ni nyie wenyewe waoga wa kuchukua hatua! Mmeanza na waziri wa afya - hakupatikana, mkaenda kwa naibu waziri akawapiga danadana wee hadi mkachoka, mkaamua muelekee kwa waziri mkuu na huko ndo kabisaaa vitisho, kejeli, kebehi, dharau, kashfa nk. Tunaelewa kuwa kwa jinsi mnavyoendelea kubabaishwa na viongozi wa serikali kuhusu madai yenu ndivyo jinsi mnavyoendelea kufanya kazi kwa mioyo iliovunjika na hivyo kuweka maisha yetu hatarini. Mimi nawaunga mkono 100% madai yenu ila siwaungi mkono spidi yenu mnayoitumia kuamua option ya kuweka vifaa chini. Msituumize kwa majadiliano yasiyo mwisho. Mi nadhani mgome leoleo ili kieleweke mapema kuliko hilo taarab mnaloliendesha na serikali. Sisi tunawaunga mkono ila na nyie msiwe waoga, hata wakenya wamewapiku kwa mbali sana. Kadiri mnavyovutana na serikali kwa maneno ndo jinsi mnavyoanza kutuboa sisi waathirika wa wa ugomvi wenu. Chukueni hatua sasa wakati wananchi tuko nyuma yenu, tunawaunga mkono japo kwa mawazo. Au ni kweli vidonge alivyowapa KM PM:
" Nawashangaa sana nyie madaktari mambo mnayofanyiana, yaani hampendani kabisa,
hamna confidence na hata mkiweka tools down haitowasaidia! "


"Nilifaulu PCB,lakini kwa kutambua ubovu wa MEDICINE mzazi wangu akanisomesha
ACCOUNTS,sasa sijui mnalalamikia nini!, mlichagua wenyewe"


Inawezekana huyu katibu mkuu kwa kiasi yuko sahihi kwa kiasi fulani kwani hata mahudhurio ya mikutano yenu ni hafifu sana ikilinganishwa na idadi yenu hata mlioko Dar tu. Haiwezekani kwenye mapambano kama haya wengine wajifiche majumbani kwao wakitegemea kuwa kuna wachache watapigana kwa niaba ya wengi! Hapa nawagusa zaidi hao wanaojiita maprofesa ambao badala ya kuwa mfano wa mstari wa mbele kwenye kudai maslahi na kusaidia kuleta moderation kwenye vita za maneno, wao ndo wooote wameingia mitini wakingojea vijana ndo wajitoe kafara!!! Kisa? Labda wanaogopa kupoteza marupurupu wanayoyapata kutoka serikali hii hii, sijui!!
Maji mmeshayavulia nguo, sasa vipi mnataka kuahirisha kuoga? Tutawazomea na kuwachukia kwa kuanzisha malumbano yasiyo na tija kwenu na yanayochangia sisi kukosa huduma kwa sababu ya migomo baridi kama ya waalimu! Mnanikumbusha enzi hizo nikiwa darasa la kwanza eti ukitaka kupigana na mwenzio aliyekuudhi basi unachora mstari chini vumbini na kumwambia kama anajiamini auruke mstari umbomoe sura - natamani kucheka ila moyo mzito. Stop politics and take action, you are scientists and not politicians!
l
 
Back
Top Bottom