Haya Nape mbona kimya,tulimwambia akadai wameamua

mkulimamwema

Senior Member
Apr 14, 2011
153
18
Tangu Mkama aseme CCM hawakutoa azimio la siku 90 na kwamba hakuna fisadi hata mmoja atakayepewa barua sijasikia tena Nape akiongea.

Lakini namwona huyu Mzee Mkama naye mnafiki mbona alikuwa anazunguka na Nape kujitambulisha alikuwa wapi siku zote kukanusha kauli hizo za kijana wao.

Hii ina maana wamekaa na kuona vita wanayoianzisha hawatashinda sasa wanajirudi lakini CCM kuondoa rushwa kwenye chama na serikali ni sawa na "MTU KUSUKUMA BASI ILIHALI YEYE NAYE AMEPANDA BASI HILO" wanaoweza kuondoa rushwa kwa sasa ni wale walio nje ya ccm na serikali yake ya waporaji wa raslimali za nchi.

Wito kwa vijana walio ccm ni kukihama chama hiki kisicho na msimamo hivi Nape jamii ya watanzania itamwonaje na maadui wangapi amejitengenezea mimi namshauri atoke huko kulinda heshima yake pia vijana wote Tanzania tuungane kuondoa uozo huu ili tuendae na tunia ya sasa ambayo ianajali vijana kwa kuwapa ajira.

CCM inasema vijana wamepata ajira na wamejiajiri lakini ajira zenyewe ni kuokota chupa za maji, vyuma chakavu ambapo wengine huokota mabomu na kuuza pipi.

Hivi kweli nguvu kazi kama vijana inaachwa ovyo na kuokota makopo bora sasa mkoloni kuliko serikali ya ccm kwa sababu mkoloni aliwapeleka kulima mashamba kwa ujira mdogo kuliko kuokota makopo ni udhalilishaji mwanaume mwenye familia kuokota makopo.
 
Huyu nape na Mukama wanacheza ngoma tofauti kabisa. Muziki wa gamba hawajaulewa. Huyu Nape atapasuka ubongo, bado kidogo tu, amesahau ccm ni nini.:caked:
 
Sisi wana CCM tulikuwa na imani kubwa sana na NAPE ila kwa hili ameanza kututia shaka. Sio siri NAPE ndio kijana pekee wa CCM anaekubalika kwenye kundi la vijana ,ili aweze kujinusuru ni lazima asimamie alichokuwa anakiamini vinginevyo atanza kuingizwa kwenye kundi la vijana wa CCM amboo hawana mvuto kwenye jamii ya watanzania
 
Nape amevishwa jiwe zito la kilo 100,wanamtosa polepole baharini kwa kamba ya nailoni sio ya katani,sijui ni kwa vipi aliamni UVCCM walimpigia chapuo kuingia kwenye sekretariati huku angali akijua walikuwa maadui zake nambari moja,walichomfanyia sasa ilikuwa kumuingizia kaseti kwenye ubongo wake,akiifungulia utamsikia kuna watu wanataka kumchafua raisi na familia yake
Mafisadi lazima wanq'oke katika siku 90 au tutawanq'oa
Tuanjivua gamba kwa sababu tumewasha mwenge wa matumaini
Nilipomuona kwenye kipindi maalumu pale Mlimani TV niliona hofu yake mpaka sauti yake alikuwa anatetemeka nikajua waharibifu wa CCM wameshamharibu NAPE hataweza kuaminika na kuheshimika kwenye jamii ya vijana tena,mazingira yamemzika NAPE pole kijana ajali ya kisiasa hiyo usiwaamini genge la watoto wa viongozi walioko UVCCM ulikuwa mpango waakina shigela Beno,Ridhiwani kukuweka mbele kama human shield ,jifunze kungali mapema
 
Nape amevishwa jiwe zito la kilo 100,wanamtosa polepole baharini kwa kamba ya nailoni sio ya katani,sijui ni kwa vipi aliamni UVCCM walimpigia chapuo kuingia kwenye sekretariati huku angali akijua walikuwa maadui zake nambari moja,walichomfanyia sasa ilikuwa kumuingizia kaseti kwenye ubongo wake,akiifungulia utamsikia kuna watu wanataka kumchafua raisi na familia yake
Mafisadi lazima wanq'oke katika siku 90 au tutawanq'oa
Tuanjivua gamba kwa sababu tumewasha mwenge wa matumaini
Nilipomuona kwenye kipindi maalumu pale Mlimani TV niliona hofu yake mpaka sauti yake alikuwa anatetemeka nikajua waharibifu wa CCM wameshamharibu NAPE hataweza kuaminika na kuheshimika kwenye jamii ya vijana tena,mazingira yamemzika NAPE pole kijana ajali ya kisiasa hiyo usiwaamini genge la watoto wa viongozi walioko UVCCM ulikuwa mpango waakina shigela Beno,Ridhiwani kukuweka mbele kama human shield ,jifunze kungali mapema[/QUN]

Nasikia Kinana alikataa ukatibu mkuu. Kwa uzoefu wake, nafikiri aliona mbali. Kijana alitakiwa kuwa na kauli za kupima na kuangalia msimamo wa mkubwa wake machoni na moyoni.
 
Kuna rafiki yangu nilimtahadhali kuwa ule mziki ni wa chache ndani ya CCM waliofahamu rythm yake.Nape hata mashairi ya muziki alikuwa hayajui akawa anaweka rap zake na vikorombozwo weeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!! utadhani Msafiri Diouf wa Twanga pepeta ya enzi zile.sasa kaaambiwa unafundisha mashairi tofauti wewe dogo.Kinachokuja ni kupata ADHABU KALI KWA UTOVU WA NIDHAMU ikiwa ni pamoja na kuutema ukuu wa district.
 
Huyu nape na Mukama wanacheza ngoma tofauti kabisa. Muziki wa gamba hawajaulewa. Huyu Nape atapasuka ubongo, bado kidogo tu, amesahau ccm ni nini.:caked:

... Huenda muziki wenyewe haujaeleweka na watu wengi. Katika mziki wenyewe namfananisha Nape na mziki ambao Mzee Tingatinga angeucheza kama hakuondolewa kwenye chati na akina nanihii. wale walomchezea rafu Six. Si unaona jinsi Mukama alivyofanya about turn baada ya Mzee wa Loliondo kuteta na JK? Hapo jibu lapatikana. Kwa hiyo Nape na Mukama kila mmoja na kinubi chake, na COMPOSER wake pia!
 
Tatzo lake Nape hajui kama CCM sahvi ni mali ya wateule (capitalists) wachache na wasiozidi 50 na M/Kiti wake akiwemo,bado anawaza CCM ya Nyerere ambayo hata Nyerere mwenyewe alishathibitisha pasi na shaka kwamba CCM ya leo siyo ile aliyoiacha yeye

Nape unaowasuta ndo walimweka M/Kiti wako Ikulu na wakimtaka atoke bado hawajashindwa,kama unabisha sema SU! wewe umevalishwa mask bila kujua wenzio wanakucheka,umebaki VUVU............ZERO
 
vijana wasio na mvuto ccm ni kama vile Ridhiwani Kikwete.January Makamba na wengineo.
 
Tatzo lake Nape hajui kama CCM sahvi ni mali ya wateule (capitalists) wachache na wasiozidi 50 na M/Kiti wake akiwemo,bado anawaza CCM ya Nyerere ambayo hata Nyerere mwenyewe alishathibitisha pasi na shaka kwamba CCM ya leo siyo ile aliyoiacha yeye

Nape unaowasuta ndo walimweka M/Kiti wako Ikulu na wakimtaka atoke bado hawajashindwa,kama unabisha sema SU! wewe umevalishwa mask bila kujua wenzio wanakucheka,umebaki VUVU............ZERO
mkuu nakubali 98% mkuu hii ni kweli na Nape hajui hiloo, analeta mambo ya ujamaa na kujitegemea wakati ilisha feli kitambo!
 
Back
Top Bottom