Haya magazeti yamefia wapi?

Hemed Maronda

Senior Member
Oct 27, 2010
138
43
Nakumbuka wakati mfumo wa vyama vingi unaruhusiwa hapa Tanzania njia kuu ya mawasiliano ya kupata taarifa muhimu za vyama ilikuwa ni magazeti moja ya magazeti mahiri kwa wakati huu yalikuwa ni MOTOMOTO,MFANYAKAZI,JOHARI magazeti haya yalikuwa yanaandika habari kwa umahiri na bila woga wowote lakini baada ya muda yakatoweka,nilikuwa nataka kufahamu hata wahariri wa magazeti haya tuamini kuwa wamekufa kama yalivyokufa magazeti yao?
 
Moto moto lilikuwa la jamaa mmoja anaitwa Justin amefilisika kwa sasa
Mkuu nashukuru kwa taarifa maana jamaa alikuwa anajituma kufanya kazi kwa umakini lakini yawezekana labda alipigiwa hesabu kubwa za kodi na TRA kwa kuwa alikuwa anawachachafya sana Serfikali.
 
...NIlidhani Motomoto lilikuwa la Emmanuel Salehe ambaye nadhani aliishariki, samahani sana kama sivyo, na ambayo mmoja wa waandishi wake Charles Misangu ndio sasa Mhariri wa Habari Tanzania Daima...?

Mfanyakazi baada ya Stan Katabalo kufariki, James Nhende kuhamia Mwanza na Hemed Kimwaga kutimua zake, Likaishia...
 
Mimi nililipenda "WAKATI NI HUU" la Kajubi Mukajanga!
Pia lilikuwepo "HEKO" nadhani lilikuwa la yule mwandishi mahiri: Marehemu Stanley Kamana, baada ya "kusogezwa" ikulu na rafikiye Mkapa, akapotelea huko huko!
 
Kulikuwa na gazeti moja la kila wiki JITAMBUE! Lilikuwa lina habari nzuri za kufungua watu
 
Mimi nililipenda "WAKATI NI HUU" la Kajubi Mukajanga!
Pia lilikuwepo "HEKO" nadhani lilikuwa la yule mwandishi mahiri: Marehemu Stanley Kamana, baada ya "kusogezwa" ikulu na rafikiye Mkapa, akapotelea huko huko!

'HEKO',lilikuwa la Ben R. Mtobwa (R.I.P). Vile vile,kulikuwa na magazeti yaliyokuwa ni MWIBA kwa serikali,nayo ni, 'WATU','SHABA', pamoja na 'TAZAMA' (sio Tazama la sasa. Ni lile la CHARLES CHARLES ,na JULIUS MAPUNDA kabla hawajajisalimisha CCM. CHARLES CHARLES,alikuwa KUBENEA wa wakati huo,kwa habari zake,na ukurasa wa 'KAMA NINGEKUWA MIMI'!)
 
Nasikia Tanzania Daima na Mwanahalisi R.I.P ni magazeti ya viongozi wa Chadema.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom