Haya mabasi yatatuua yatumalize

Huyo dereva si mjinga kama mnavyofikiri, hadi kuamua ku-overtake lazima aliona mbele kumenyooka na hakuna gari
 
DSC2936-web60-copy.jpg

mia

Huyo dereva si mjinga kama mnavyofikiri, hadi kuamua ku-overtake lazima aliona mbele kumenyooka na hakuna gari

Duh! Mbele kumenyooka!!?!?! Wewe unaona hadi mistari ya barabarani ilivyochorwa inaonyesha hauruhusiwi kuovertake hapo!! Sasa suala la kuona kumenyooka mbele hizo si ndio bange na gomba zinazoongelewa hapa?!?!?
 
Hata abiria huwa tunachochea.
Uchochezi wa abiria inategemea mana kuna magari hata ufanyeje wao speed yao kama ni 100 ni 100 tu na nadhani unayajua lakini ni kweli kuna baadhi ya mabasi yanaendeshwa na abiria yani abiria wakisema dereva chochea anachochea, punguza anapunguza.
 
Kuna rafiki yangu amesafiri na basi la TAQWA juzi tu linaloanzia safari yake kutoka Lubumbashi kupitia Zambia,Mbeya hadi DSM. Yeye aluipandia Mbeya saa 5.00 asubuhi. Amenisimulia kuwa muda wote wa safari alikuwa anaona ni muda wa kifo licha ya abiria kupinga mwendo kasi wa dereva. Pia gari lilikuwa linasimama katika kila kituo na kujaza abiria kupita kiasi. Hii kampuni ya TAQWA inabidi imulikwe vinginevyo si muda tutashuhudia vifo vya watu 30, 40 au 50 katika ajali moja
 
madereva wetu ni wazembe ila hata sisi tunachangia wazee..! utakuta ukiwa kwenye daladala unaona kua dereva anaetanua ni mzuri na anajua kazi yake.. lakini ukiwa unaendesha gari yako private ukakutana na dereva anae tanua unamind kua huyu kajifunza chini ya mti auuu yani unakuta sisi wenyewe ni vigeu geu...!
 
Noma sana hii, kwenye kona kama hio ana overtake? Mchezo huu ndio unasababisha ajali karibia zote.

Naona labda kwenye sehemu kama hizi waweke ukuta mdogo katikati kwa umbali flani kutenganisha gari za kulia na kushoto mpaka sehemu ambayo ni. Salama ku-overtake.
 
Utaahira+bange+misifa isiyokuwa na maana=akili ya madereva wetu (walio wengi) wa mabasi hapa nchini!
Mi naona wangeweka dereva wa bus lazima elimu ya chini iwe form 4.nahisi elimu inachangia
 
Back
Top Bottom