Haya mabasi vipi?

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,782
2,406
Nimetoka Singida naelekea Arusha, nimepanda Mtei bus yaani linasimama kila sehemu limejaza sana na abiria wengi wamesimama.

Ninachoshangaa traffic wapo barabarabi na wanalisimamisha gari wanachungulia mlangoni ambapo kwa uwingi Wa abiria hawawezi ingia, mara wanachungulia madirishani ni kuturuhusu huku konda akitoka nje kumalizana nao, abiria wanapiga kelele hakuna hewa huku wengine wakitapika.

Jamani Hawa traffic kazi Yao nini Kama sio kusimamia usalama barabarani?
 
kuna namba huwa zinawekwa kwenye mabasi za wakuu wa polisi hebu piga mkuu, au huu utaratibu upo mabasi ya mbeya tuu!?
 
kuna namba huwa zinawekwa kwenye mabasi za wakuu wa polisi hebu piga mkuu, au huu utaratibu upo mabasi ya mbeya tuu!?

Mkuu sijaona namba yoyote hapa. Tumefika kwa mizani wamewaamsha abiria viti vya nyuma waje kusimama katikati uzito usizidi..... Ha ha ha!
 
Mabasi ya mafisadi au ya wenye uhusiano nao huwa hayakamatwi ndugu yangu! We omba Mungu tu muweze kufika salama! Bon Voyage!
 
Mabasi ya mafisadi au ya wenye uhusiano nao huwa hayakamatwi ndugu yangu! We omba Mungu tu muweze kufika salama! Bon Voyage!

Mkuu huwezi amini wameweka mafuta Babati tumefika Miserani Gari imezima mara hao sheli na dumu la lita 20 hapa limegoma kuwaka wanahangaika! Mungu tujalie tufike salama
 
Mkuu huwezi amini wameweka mafuta Babati tumefika Miserani Gari imezima mara hao sheli na dumu la lita 20 hapa limegoma kuwaka wanahangaika! Mungu tujalie tufike salama
Dah..! Poleni sana ndio usafiri wetu huo. Trafiki wao wanakusanya pesa tu barabarani
 
kama upo meserani tayari umeshafika.....shuka kamata kifodi njoo mjini....siku nyingine ukiona gari limejaa sana usipande.....azawais weka namba ya gari tukusaidie msaada wa kipolisi.....
 
kama upo meserani tayari umeshafika.....shuka kamata kifodi njoo mjini....siku nyingine ukiona gari limejaa sana usipande.....azawais weka namba ya gari tukusaidie msaada wa kipolisi.....

Naelekea Moshi Preta, na Nina mizigo, ndo tumeingia Arusha stand, duh! Usafiri huu kizunguzungu,
 
Last edited by a moderator:
mungu ni mwema sana, nimefika salama Moshi. Haya mabasi ni hatari kujaza abiria kiasi hicho, tumetoka singida vizuri, sanyasanya njiani duh!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom