Haya kama maajabu vile

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,832
2,790
Watanzania tumekuwa wepesi sana wa kuiga mambo mbali mbali toka sehemu nyingine aidha kwasababu tumeona katika picha au kusikia hebu soma hii taarifa huwezi kuamini kama imetokea Tanzania. Mbona mazuri ya huko tunakoiga mabaya hatuyaigi???

Aliyemchinja mdaawa wake kutinga Mahakama Kuu

http://www.freemedia.co.tz/daima/2007/12/17/habari33.php

na Anthony Komanya, Shinyanga

MTU mmoja anayedaiwa kumchinja kwa panga na kuondoka na kichwa cha mdaawa wake hadi mahakamani, atafikishwa mbele ya Mahakama Kuu kujibu tuhuma za mauaji, imefahamika.
Akisoma maelezo ya awali, wakili wa upande wa mashitaka, Robert Mkoba, aliiambia Mahakama Kuu mjini Shinyanga kuwa mtuhumiwa Ndito Sukumawiki, alimkatakata na kumchinja kwa panga, akitenganisha kichwa na kiwiliwili mdaawa wake, aliyemshinda kwenye kesi ya madai ya nyumba ya thamani ya sh 60,000, Yusuf Charles.
Wakili Mkoba alisema tukio hilo lilitokea nyumbani kwa marehemu Machi 5, mwaka 2002 majira ya saa 5:00 usiku katika Kijiji cha Kimali wilayani Meatu, Mkoa wa Shinyanga.
Mkoba aliendelea kudai kuwa, baada ya kumkata kichwa, Sukumawiki, aliondoka na kichwa cha marehemu hadi kwenye Mahakama ya Mwanzo ya Kimali, ambako aliendelea kufanya vitendo vya kinyama.
Akiwa mahakamani huko, alisema mshitakiwa alipaka milango, madirisha na sakafu kwa damu inayosadikiwa kuwa ya marehemu, kwa kuandika herufi 'n.d.s' hapa na pale mahakamani humo.
Ilidaiwa kuwa, akiwa anaendelea na vitendo hivyo vya kinyama, mshitakiwa alikurupushwa na mlinzi wa mahakama hiyo na kutoroka hadi alipokamatwa siku nyingi baadaye.
Ilidaiwa kuwa katika maelezo ya ungamo la awali mbele ya mlinzi wa amani wa Mahakama ya Mwanzo Kimali, mshitakiwa alikiri kufanya mauaji hayo ya kinyama.
Hata hivyo, wakati akisomewa maelezo ya awali, mtuhumiwa huyo alikana kutenda kosa hilo mbele ya Jaji Alice Chinguwile na hivyo kesi yake kupangwa kusikilizwa katika kikao kijacho.
 
Back
Top Bottom