Hawara amuua mwenye mume

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAMKE mkazi wa Ronsoti mjini Tarime mkoani Mara, Debora James (30), anatuhumiwa kumuua mwenzake, Teresia Nago, kwa kumchoma kisu katika mauaji yanayohusisha kugombea mwanamume.

Kwa mujibu wa Polisi, Teresia aliuawa jana saa 4.30 asubuhi Bomani mjini Tarime, baada ya kuchomwa visu viwili tumboni na kifuani na mgomvi wake huyo.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rorya/Tarime, Sebastian Zakaria, alisema Debora alikuwa akituhumiwa kuwa na uhusiano na mume wa Teresia, John Nago ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ujenzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Kaimu Kamanda alisema, wanawake hao wawili walikuwa na ugomvi wa muda mrefu na vurugu wakigombea mwanamume huyo.

Alisema, jana Teresia na Debora walikwenda kusuluhishwa na mzee wa Kanisa ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja eneo la Bomani.

Lakini wakiwa Bomani, kulitokea vurugu na Debora ambaye alikuwa na kisu alimshambulia Teresia kwa kumchoma kisu kifuani karibu na moyo na tumboni na kusababisha kifo chake papo hapo, baada ya kutokwa damu nyingi naye akajichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake kwa lengo la kujimaliza.

Kamanda Zakaria alisema Debora amelazwa katika hospitali ya wilaya mjini hapa chini ya ulinzi wa Polisi baada ya kujijeruhi.
 
nilidhani idadi ya wanaume wakware imeongezeka!ila na sie wanawake huwa tuna akili za kuku,why on earth wld u kill someone for lov,ama kujiua? kuna watu wamefiwa na wenzi wao ambao waliwaonesha upendo na kuwajali,seuze ambaye haoneshi hata kujali! he is nt worth even a blink of my eye,kha!
idadi ya wanawake wavuta bangi inaongezeka
 
Jamani nini kinachogombewa hasa, du ona sasa. Hii yote ni upungufu wa kufikiri.
 
nilidhani idadi ya wanaume wakware imeongezeka!ila na sie wanawake huwa tuna akili za kuku,why on earth wld u kill someone for lov,ama kujiua? kuna watu wamefiwa na wenzi wao ambao waliwaonesha upendo na kuwajali,seuze ambaye haoneshi hata kujali! he is nt worth even a blink of my eye,kha!
ase is true it seems hilo janadume lilishindwa kuchagua liache yupi?is not an issue to fight for someone as dishonest as this shem on him loool,af msibani atalia huyooo kama ndama
 
pole bwana harusi sasa umewakosa wote . mmoja jela mwingine kaburini!umefaidi nini hapo na nafsi itakusuta mpaka mwisho wako
 
maisha kweli yamebadilika, cku hizi unaenda kusuluhishwa na hawara wa mumeo, khaa...RIP mdada.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom