Hawa watu wako wapi? (waliosomea shule za Vipaji maalumu).

Nina mwanangu hakupitia hizo mnazoziita special schools. Yeye alisomea shule ya private ya hapa Tanzania ya kawaida tu. Habari zake zilidakwa na sasa hivi anamalizia Phd katika fani nyeti kwa gharama za vyuo vya marekani vilivyokuwa vinamgombania. Sijamlipia hata senti tano tangu amalize
O level na sasa anamalizia Phd.
 
Sidhani kama umefanya uchunguzi wako vizuri,,, mimi ni product ya ILBORU Kwa miaka sita yote ya sekondari na kuitwa kipaji maalum sio tu ni jina ni kweli tuna mshukuru MUNGU tuna vipaji maalumu. Hakika nakuambia ukimuweka form 1 wa kipaji maalum na wa shule za kawaida utagundua utofauti mkubwa hasa wa uelewa na wala usiulize tuko wapi tupo TZ hii hii na tuna nafasi nzuri tu ki maisha na ki elimu pia. Nenda UDSM uangalie zile shahada kali kali zote utawakuta wamejaa na wana ufaulu mzuri tu na si hilo tu ukipima uelewa wao utagundua utaofauti wao. Kama ni muungwana fanya uchunguzi zaidi ila kama ni mbishani baki na msimamo wako.Sisi ni vipaji kweli kweli.
 
hello, im new here, the thread is interesting. but still shule za vipaji maalum, ni maalum kweli.
 
vipaji maalumu inatokana na ufaulu wako, then usubili kuchaguliwa kuingia huko. Unapofika huko utawakuta vipaji binafsi, wale waliofaulu kwa spoon feeding na hata wale waliofaulu kwa kupata nondo!
 
Na waulize wale waliosoma shule za watakatifu kama nao ni watakatifu, kwa watanzania haya mambo hayazingatii maana wala dhima watu wanajianzishia tu na kupachika majina hata kama hayaendani na uhalisia
 
vipaji maalum ni kama baba alikuwa kiongozi serikalini basi mtoto wake naye kuwa kiongozi inaonyesha kipaji.
Shule za wenye vipaji husomesha watoto wa matajiri na viongozi. Wenye vipaji wengi tunao vijiweni.
 
Mimi kila mara huwa najiuliza walikuwa wanatumia vigezo gani kuamua yupi ana kipaji maalumu na yupi hana.

Ni kwamba walikuwa wana wa-observe kwa muda mrefu katika masomo yao au?

Au walikuwa wanaangalia maksi apatazo mtu kwenye mtihani wa taifa?

Manake kupata maksi za juu kwenye mtihani si kipaji maalumu. Na kufanya vizuri shuleni si kipaji maalumu.

Ningependa sana kujua walikuwa wanatumia vigezo gani! Na pia ningependa kujua fasili yao ya 'kipaji maalumu' ni nini!

Kaka watu wenye vipaji maalum wapo,na tuko nao kwenye jamii.Bahati nzuri mimi nimesoma nao na wana vitu vingi tu vya ziada,kimsingi ni UELEWA wao wa mambo ya Darasani na mengine yanayotuzunguka.Ila kwa bahati mbaya HAWAPEWI nafasi sana ndani ya nchi hii.Nchi hii haiwapi umuhimu wa kutosha sana ndani ya serikali na sehemu muhimu.Hivyo wengi wao wanaishia kwenda nje ya nchi kufanya nchi kufanya kazi na wachache sana wanabakia kama WALIMU vyuoni na kwenye taasisi binafsi.Kwenye taasisi binafsi wanatambuliwa na wanasaidia sana taasisi hizo.
 
Mimi mwenyewe ni product ya hizo shule.Nimepitia O-level pale kibaha lakini advance nilienda Tech sec school.Kusema ukweli hizi shule kigezo wanachotumia ni marks za juu.Tatizo kuu linaloibuka ni wanafunzi kubweteka kutokana na kupewa jina kipaji maalumu.Halafu pia hata walimu husika nao hawafanyi bidii kubwa kufundisha wakiamini hawa wanafunzi hawahitaji msaada mkubwa.That's why mimi mwenyewe nilitoka na div 1 ya kawaida tu then nikaenda advance shule ya kawaida i.e Tanga tech.Lakini pale mahali nilipikwa nikapikika na mwisho wa siku nikachana paper uzuri kabisa na nilipoingia chuo niliwaburuza watu mwanzo mwisho,mimi sikuijua SUP wala DISCO.Kitu kilichonifanya niamini nina kipaji ni kwamba nilikuwa napiga msuli sisimizi napata matokeo tembo.
Hi bro!
 
Nina mwanangu hakupitia hizo mnazoziita special schools. Yeye alisomea shule ya private ya hapa Tanzania ya kawaida tu. Habari zake zilidakwa na sasa hivi anamalizia Phd katika fani nyeti kwa gharama za vyuo vya marekani vilivyokuwa vinamgombania. Sijamlipia hata senti tano tangu amalize
O level na sasa anamalizia Phd.
Hongera yake
 
hatuna shule za vipaji maalumu tz, shule za vipaji zilikuwa ifunda, mazengo, tanga tech, etc ambapo mwanafunzi anakwenda kusomea masomo ya ufundi kivitendo akimaliza f4 anakuwa ni fundi kabisa. Sasa hao mzumbe, ilboru mwanafunzi wa PCM anamaliza f6 div 1.5 hata kuconnect socket hajui, hili ndio tatizo la mfumo wetu wa elimu nikijiuliza PCM niliyosoma ilinisaidia nini wala sipati majibu. Na mbaya zaidi hao tunaowaita vipaji wakimaliza chuo wanakimbilia mzumbe university BAF na si udaktari au engineering
Ujengewe sanamu mkuu

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Kaka watu wenye vipaji maalum wapo,na tuko nao kwenye jamii.Bahati nzuri mimi nimesoma nao na wana vitu vingi tu vya ziada,kimsingi ni UELEWA wao wa mambo ya Darasani na mengine yanayotuzunguka.Ila kwa bahati mbaya HAWAPEWI nafasi sana ndani ya nchi hii.Nchi hii haiwapi umuhimu wa kutosha sana ndani ya serikali na sehemu muhimu.Hivyo wengi wao wanaishia kwenda nje ya nchi kufanya nchi kufanya kazi na wachache sana wanabakia kama WALIMU vyuoni na kwenye taasisi binafsi.Kwenye taasisi binafsi wanatambuliwa na wanasaidia sana taasisi hizo.
Hii hoja nimeikubali 100%
 
Mimi mwenyewe ni product ya hizo shule.Nimepitia O-level pale kibaha lakini advance nilienda Tech sec school.Kusema ukweli hizi shule kigezo wanachotumia ni marks za juu.Tatizo kuu linaloibuka ni wanafunzi kubweteka kutokana na kupewa jina kipaji maalumu.Halafu pia hata walimu husika nao hawafanyi bidii kubwa kufundisha wakiamini hawa wanafunzi hawahitaji msaada mkubwa.That's why mimi mwenyewe nilitoka na div 1 ya kawaida tu then nikaenda advance shule ya kawaida i.e Tanga tech.Lakini pale mahali nilipikwa nikapikika na mwisho wa siku nikachana paper uzuri kabisa na nilipoingia chuo niliwaburuza watu mwanzo mwisho,mimi sikuijua SUP wala DISCO.Kitu kilichonifanya niamini nina kipaji ni kwamba nilikuwa napiga msuli sisimizi napata matokeo tembo.
Nimependa "msuli sisimizi, matokeo Tembo".... hahahaha
 
Miaka ya nyuma kulikuwa na thread critical sana.

Sasa hivi huwezi kuta thread kama hii definitely because kiwango cha ujinga kimeongezeka.
 
Habari wa JF nimatumaini yangu mnafurahia wikiendi nzuri.
Binafisi hoja yangu hapa nikutaka kujua hawa watu walio soma hizi shule za vipaji maalumu ziko nyingi pamoja na kwamba zinazidi kupungua umaarufu wake, je hao waliosomea kama watu wavipaji maalumu wako wapi? nawanafanya nini? nilitegemea hawa watu serikali iliwatengea shule maalumu kwa nia nzuri kwamba waandaliwe katika kuja kulikomboa taifa hili ambalo liko chini sana kimaendeleo, matokeo yake sioni hata maana ya hizo shule uwepo wake, matokeo yake naona viongozi wasiokuwa na huruma hata chembe ya uzalendo kwa taifa lao na hapo ndo nashindwa kuelewa kama hao viongozi iliowandaa kupitia shule za vipaji maalumu?

Binafisi ni sikioapo neno kipaji maalumu tafisiri yake inakuja haraka haraka kwamba ni mtu mwenye uwezo wa akili za ziada juu ya fani fulani kama uchoraji,mcheza mpira, nk, yaani ubunifu wa ziada bila kufundishwa na kama mtu huyu atafundishwa basi nikumuongezea skills fulani fulani ambazo zitamfanya afanye vizuri zaidi katika fani yake hiyo. Sijui serikali yetu wakati inazianzisha ilikuwa na maana hiyo au jina ndo lilipotoshwa tu? Na kama ndo lilipotoshwa basi hatuna shule ya vipaji maalumu na muda huu ndo wakati wa kuwa na shule za vipaji maalumu kulingana na nauhitaji wa dunia ya sasa, elimu yetu kwa sasa sioni hasa inalenga nini? inamwandaa mtanzania wa namna gani? aje alifanyie nini taifa lake? au ndo tuna andaa watu ambao wategemee kuajiriwa pekee?

Watanzania na wasomi walio wengi wakitanzania asomapo mara nyingi tuna fikiria baada ya masomo ni ajira serikalini au mashrika binafisi ndani ya nchi nasi nje ya nchi na hii ni kwa sababu hatukuaandaliwa vizuri tunaogopa kupambana na nchi zingine katika soko la ajira,hii ni kwamba hatuna vipaji maalumu? au inawekena tunavyo lakini havikuendelezwa? hizo shule zina fundisha vipaji maalumu au zina fundisha watu wenye vipaji mchanganyiko? ambao wanashindwa kujipambanua navipaji vyao na kuishia kuwayawaya tu, pengine tungeweza kuwa na shule inayo andaa watu wenye vipaji vya uongozi, na kupata watu ambao wangelipeleka taifa hili mahara pazuri na lenye mafanikio makubwa.

Swali langu je? hizi shule ni vya vipaji maalumu katika fani gani?
Wengi tupo nao kitaa na 95% ni Broke and Drunkard Intellectuals.
 
Back
Top Bottom