Hawa watu wako wapi? (waliosomea shule za Vipaji maalumu).

Mtanganyika1

Member
Sep 13, 2011
56
5
Habari wa JF nimatumaini yangu mnafurahia wikiendi nzuri.
Binafisi hoja yangu hapa nikutaka kujua hawa watu walio soma hizi shule za vipaji maalumu ziko nyingi pamoja na kwamba zinazidi kupungua umaarufu wake, je hao waliosomea kama watu wavipaji maalumu wako wapi? nawanafanya nini? nilitegemea hawa watu serikali iliwatengea shule maalumu kwa nia nzuri kwamba waandaliwe katika kuja kulikomboa taifa hili ambalo liko chini sana kimaendeleo, matokeo yake sioni hata maana ya hizo shule uwepo wake, matokeo yake naona viongozi wasiokuwa na huruma hata chembe ya uzalendo kwa taifa lao na hapo ndo nashindwa kuelewa kama hao viongozi iliowandaa kupitia shule za vipaji maalumu?

Binafisi ni sikioapo neno kipaji maalumu tafisiri yake inakuja haraka haraka kwamba ni mtu mwenye uwezo wa akili za ziada juu ya fani fulani kama uchoraji,mcheza mpira, nk, yaani ubunifu wa ziada bila kufundishwa na kama mtu huyu atafundishwa basi nikumuongezea skills fulani fulani ambazo zitamfanya afanye vizuri zaidi katika fani yake hiyo. Sijui serikali yetu wakati inazianzisha ilikuwa na maana hiyo au jina ndo lilipotoshwa tu? Na kama ndo lilipotoshwa basi hatuna shule ya vipaji maalumu na muda huu ndo wakati wa kuwa na shule za vipaji maalumu kulingana na nauhitaji wa dunia ya sasa, elimu yetu kwa sasa sioni hasa inalenga nini? inamwandaa mtanzania wa namna gani? aje alifanyie nini taifa lake? au ndo tuna andaa watu ambao wategemee kuajiriwa pekee?

Watanzania na wasomi walio wengi wakitanzania asomapo mara nyingi tuna fikiria baada ya masomo ni ajira serikalini au mashrika binafisi ndani ya nchi nasi nje ya nchi na hii ni kwa sababu hatukuaandaliwa vizuri tunaogopa kupambana na nchi zingine katika soko la ajira,hii ni kwamba hatuna vipaji maalumu? au inawekena tunavyo lakini havikuendelezwa? hizo shule zina fundisha vipaji maalumu au zina fundisha watu wenye vipaji mchanganyiko? ambao wanashindwa kujipambanua navipaji vyao na kuishia kuwayawaya tu, pengine tungeweza kuwa na shule inayo andaa watu wenye vipaji vya uongozi, na kupata watu ambao wangelipeleka taifa hili mahara pazuri na lenye mafanikio makubwa.

Swali langu je? hizi shule ni vya vipaji maalumu katika fani gani?
 
crap!!
 
Mimi nilisoma kayumba primary nilifeli nikaenda shule ya wazazi pale Iringa baadaye Tosamaganga boys nikakutana na hawa wanaotoka special school nikawakimbiza vibaya sana, nikaenda zangu Muhimbili kwa sasa ni Dr. Hizi special unafikri zinamaana basi watu wenyewe wanaiba mitihani mwisho wa siku wanapata 0 hakuna cha special wala nini. Aliyeandika crap hapo yawezekana ni mwathirika mmoja wao.
Wakati nipo o level nilikuwa naamini jina la shule halifaurishi ila inategemea umejiandaa vp. Ndicho nilichofanya nikaandika records ambazo mpaka sasa hazijavunjwa. Maisha ni popote
 
Nilikutana nao chuo udsm, kozi yangu walikuwa zaidi ya 80%, for sure walikuwa na vitu vya ziada. Sijui hawa wa sasa maana wengi watakuwa wanatoka st. lunatics maarufu kwa kununua mitihani !
 
Mimi kila mara huwa najiuliza walikuwa wanatumia vigezo gani kuamua yupi ana kipaji maalumu na yupi hana.

Ni kwamba walikuwa wana wa-observe kwa muda mrefu katika masomo yao au?

Au walikuwa wanaangalia maksi apatazo mtu kwenye mtihani wa taifa?

Manake kupata maksi za juu kwenye mtihani si kipaji maalumu. Na kufanya vizuri shuleni si kipaji maalumu.

Ningependa sana kujua walikuwa wanatumia vigezo gani! Na pia ningependa kujua fasili yao ya 'kipaji maalumu' ni nini!
 
Mbona wakifika vyuo wanakimbizwa kama kawa hasa wale waliotoka St St, wanaishia kuongoza kuongea Kingereza tu?!
 
nimesoma nao A-level na Udsm but wengine hawakufanya vizuri A-level na wengine Walidisco UDSM si unajua ni wazee wa kukesha so wakipata semehemu ambayo no control at all wanadata na kufeli hovyo hovyo coz hawajui maisha ya kitaa...But kuna wengine realy nakubali ni extra ordinary na wana uelewa wa ajabu its because serikali yetu haijali wasomi wenye uwezo wa ziada.
 
Siku hizi shule za vipaji zimeingiliwa coz asilimia kubwa wanao enda huko wanafauulu vizuri utokana na high spooon feeding kwenye private schools then waienda kwenye special za gvt ambazo ufundishaji haupo guaranteed na changamoto za gvt schools brding lyf advanc wanajikuta wanachemka,vpaji ce bhana primary gvt olevel gvt tena ya day yenye changamoto za ukwel na tukachomoaka wit flying colors,advnc special n flying colors as usual sasa iv tupo udsm twapigwa mabomu but katabia chetu ka ufaulu na kukimbiza class kama kawaida.......
 
Mimi mwenyewe ni product ya hizo shule.Nimepitia O-level pale kibaha lakini advance nilienda Tech sec school.Kusema ukweli hizi shule kigezo wanachotumia ni marks za juu.Tatizo kuu linaloibuka ni wanafunzi kubweteka kutokana na kupewa jina kipaji maalumu.Halafu pia hata walimu husika nao hawafanyi bidii kubwa kufundisha wakiamini hawa wanafunzi hawahitaji msaada mkubwa.That's why mimi mwenyewe nilitoka na div 1 ya kawaida tu then nikaenda advance shule ya kawaida i.e Tanga tech.Lakini pale mahali nilipikwa nikapikika na mwisho wa siku nikachana paper uzuri kabisa na nilipoingia chuo niliwaburuza watu mwanzo mwisho,mimi sikuijua SUP wala DISCO.Kitu kilichonifanya niamini nina kipaji ni kwamba nilikuwa napiga msuli sisimizi napata matokeo tembo.
 
Mimi kila mara huwa najiuliza walikuwa wanatumia vigezo gani kuamua yupi ana kipaji maalumu na yupi hana.

Ni kwamba walikuwa wana wa-observe kwa muda mrefu katika masomo yao au?

Au walikuwa wanaangalia maksi apatazo mtu kwenye mtihani wa taifa?

Manake kupata maksi za juu kwenye mtihani si kipaji maalumu. Na kufanya vizuri shuleni si kipaji maalumu.

Ningependa sana kujua walikuwa wanatumia vigezo gani! Na pia ningependa kujua fasili yao ya 'kipaji maalumu' ni nini!

kuna dogo ambaye enzi zile za mitihani mitatu ya fianal std VII alipata maksi 148/150..
Alipelekwa Ilboru.. Wanaangalia mtihani wa mwisho tu NN. Ni utaratibu mbovu though...
 
hatuna shule za vipaji maalumu tz, shule za vipaji zilikuwa ifunda, mazengo, tanga tech, etc ambapo mwanafunzi anakwenda kusomea masomo ya ufundi kivitendo akimaliza f4 anakuwa ni fundi kabisa. Sasa hao mzumbe, ilboru mwanafunzi wa PCM anamaliza f6 div 1.5 hata kuconnect socket hajui, hili ndio tatizo la mfumo wetu wa elimu nikijiuliza PCM niliyosoma ilinisaidia nini wala sipati majibu. Na mbaya zaidi hao tunaowaita vipaji wakimaliza chuo wanakimbilia mzumbe university BAF na si udaktari au engineering
 
mbona mimi waliniacha wakati nilifikisha marks hizo au kwakuwa nilisoma Rukomatwize?
 
hatuna shule za vipaji maalumu tz, shule za vipaji zilikuwa ifunda, mazengo, tanga tech, etc ambapo mwanafunzi anakwenda kusomea masomo ya ufundi kivitendo akimaliza f4 anakuwa ni fundi kabisa. Sasa hao mzumbe, ilboru mwanafunzi wa PCM anamaliza f6 div 1.5 hata kuconnect socket hajui, hili ndio tatizo la mfumo wetu wa elimu nikijiuliza PCM niliyosoma ilinisaidia nini wala sipati majibu. Na mbaya zaidi hao tunaowaita vipaji wakimaliza chuo wanakimbilia mzumbe university BAF na si udaktari au engineering
The best reply so far!
 
Back
Top Bottom