Mimi naona badala ya kujadili nani achukue bendera ya chdema kwenye urais wa 2015 wangejikita zaidi kuhakikisha kunakuwa na katiba mpya kabla ya uchaguzi ujao ili walau wawe na nafasi japo finyu ya kukishinda chama tawala. Vinginevyo hata ungewasimamisha hao wote uliowataja upande mmoja (kwa tiketi ya chadema) na mgombea wa CCM upande mwingine yumkini watashindwa tu kwani ATAKAYETANGAZWA kuwa mshindi kwa mujibu wa katiba hii na tume iliyopo ATAKUWA ni MGOMBEA WA CCM. Huu ndio ukweli wenyewe japo najua kuna watu huwa hawapendi kuusikia.