Hawa wako wapi sasa?

brazameni, hivi unamjua Pereila/Pelera ana kaka yake anaitwa George? Yuko wapi huyu jamaa hivi sasa..

Halafu nyie masela mwaongelea mashati ya ujiuji na suruali za mchelemchele...je, mnayakumbuka mashati ya 'mikorosho korosho' (paisley so to say..)
images
, miye nilikuwa na kama 4 hivi, mawili nilinunua kwa maduka ya wahindi barabara ya Uhuru na mawili toka mtaa wa Kongo pale Kariakoo kwa masela moja hivi jina anaitwa Zuberi, sijui yuko wapi naye huyu siku hizi... alikuwa mtu wa kutafuta safari sana enzi hizo, basi, kila burungutu la mitumba tu likija jamaa alikuwa ananichukulia kapello zile top range (offcourse mitumba yote) but yenye mvuto bomba zaidi ya yote na kuniwekea kando, kuanzia Ma LA-Raiders enzi hizo to Chicago Bull ofcourse...pia wakati huo LA Gear na NIKE air-pump zinatamba kichizi.... daah, kulikuwa na ka utamu fulani hivi wee acha tu, maana ukija check ma Yo Mtv na kuona umevaa chepello same,mtu weweeeeee!
 
.... Nani anakumbuka pale Amitabh Bachchan alipokuja Bongo, mid or late 80s, nakumbuka watu walikuwa wanasema alikuja ku shoot video ila ikashindikana kui release kutokana na editing kuzidi... maana kila alipoenda kushoot alikutana na watu wakiwa wameweka alama ya 'MAMBO?- DOLE TUPU HALINA UKUCHA'
thumbsup.gif
, duuh, huu msemo nao ulitoweka kinyemela... ndipo ikaja misemo kama UJANJA KUWAHI, na huu chimbuko lake mimi naona likikuwa pale station ya mabasi, maana watu walikuwa hawajali nani yuko mstarini wakati basi linasimama nao kudandia tu na kujipatia siti, basi na ile hali ya kujijitea wanakuja na majibu yao kama vile...nini wewe bana, ujanja kuwahi...
 
unajua humu ndani kumbe watu tunafahamiana sana tu..........duuuhh, ila wengi ni wadogo zangu kwa saaana tu
 
wako wapi mazee wa AZA BOY, pale stendi ya Fire. au kwenye mechi za umiseta football versus watoto wa shule za jeshi.

Nani anamkumbuka Mdudu?.
 
masela mko wapi leo ndio mkesha,basi watoto wa geti kali na wale december twaja ndio wamejaa mitaani.
leo na kesho ndio siku ya mimba kutingamaana kila mkiumbe ndio siku ya kusherekea kuzaliwa,
tukutane viwanja ngani leo,naomba kutoa hoja
 
Machizi mpo eeh?

... tupo tu tumeuchuna, si unajua tena siku zenye ma breaking news kama leo... noma tupu..

...sasa nyie masela, nani anamkumbuka jamaa mmoja hivi pale Tambaza alikuwa anaitwa Meja, jamaa alikuwa mnoko huyoo usiombee, alikuwa prefect wa maswala ya misosi....mbona tulikuwa tunakoma siye mafreshers pale, jamaa kwa vile alivyo lazima tu alienda kupapa kazi jeshini, niaminini mimi... mdude ule ulikuwa nuksi, fullstop!

...lakini pia wakati wa mgao wa misosi pale Tambaza, kuna jamaa mmoja alijitokeza, tulikuwa tunamwita Chua (chuwa), jamaa naye alikuwa nuksi kichizi kwenye maswala ya misosi, yeye wala hakuwa prefect, lakini connection zake kule jikoni na ukiwa kundi moja naye lazima muibuke na sinia kama 3 hivi za wali na nyama, hali wengine wakiangulia vibakuli tuu... jamaa alikuwa hana mchezo, siku nyingine kukiwa msosi hautoshi wanafunzi halafu unamkuta amefanikiwa kupata walau plate moja, jamaaa alikuwa anatemea mpunga wote na mate, ili mtu asimsogelee... lakini kuna machizi vile vile nakumbuka hilo halikuwa sooo kwao, walikuwa bado wanautwanga wali ule pamoja na kutemewa mate...nomaaaaaa... halafu chizi yule siku amekuruhusu kula msosi wake, ukishiba na kutaka kuondoka anakuambia 'lete mikono hiyo', kama hujaelewa unaweza anza shangaa shangaa, kumbe jamaa walikuwa wanamaanisha kuleta mikono hiyo 'na kulambwa', ili mradi tu usiondoke na punje hata moja... daaaah, kweli siku hizo nazimiss kichizi masela wangu..
 
haya mambo ya siasa yameanza kunibore sasa...

hivi masela mtaleta mambo tofauti hapa...hebu fanyeni kweli basi..
 
...eeebana, vipi mbona mmesusa hivoo? mnaumwa nini? mimi ngoja niwachore tuu sasa....mnaboa bana.... aaaaaah!

6yk4un4.gif
85zufiu.gif
6krsb42.gif


anywei, hamna noma wala nini...
 
Nani anamkumbuka Rabia yule bibi wa kihindi pale Upanga? Bibi alikuwa anatema mate kaa nyoka halafu ukimwuzi zaidi anakufunulia uchi wake....
 
Nani anamkumbuka Rabia yule bibi wa kihindi pale Upanga? Bibi alikuwa anatema mate kaa nyoka halafu ukimwuzi zaidi anakufunulia uchi wake....

ha ha ha ha ha ha ha ha!!!!

eeeeebwana weeee,,, noma.. halafu saa nyingine alikuwa anatembea mpaka kule train station akiwa anaomba omba shilingi 5!!
duuh, weee chizi umenikumbusha mbali kichizi.... ukimwona tu mtu lazima ukatishe barabara..
 
Nani anamkumbuka Rabia yule bibi wa kihindi pale Upanga? Bibi alikuwa anatema mate kaa nyoka halafu ukimwuzi zaidi anakufunulia uchi wake....

Nyani, hivi ni kweli kuwa kuna baadhi ya macheck bob wa ShaabanRoberts walikuwa wanamtokea na kumhonga fegi?!!!!!!!! kufuru tupu!
 
Nyani, hivi ni kweli kuwa kuna baadhi ya macheck bob wa ShaabanRoberts walikuwa wanamtokea na kumhonga fegi?!!!!!!!! kufuru tupu!

Aaah yaani totoz zote zile pale Shebby Robby waziache wamtokee Rabia...labda Erick Mwenda na mwenzake Jesse....Lol
 
SteveD ulikuwa group One or two? Nakumbuka ubwabwa wa Mwinyi mijiwe kibaaaaaoooo.
 
SteveD ulikuwa group One or two? Nakumbuka ubwabwa wa Mwinyi mijiwe kibaaaaaoooo.

Group II mshirika, nakumbuka sana ule ubwabwa...maana haukuwa na mchanga, bali ulikuwa na kokoto... lakini masela wenye dhiki walaaaa.... hamna noma wala nini, tuliutwanga hivo hivyo... lol
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom