Hawa wakereketwa wa magamba waliomvua ubunge kamanda wetu Arusha wataishije A-city

Liverpool2005

Member
Jul 20, 2011
43
39
Hawa wafuasi wa magamba walishauriwa vibaya kisa chenji chache kutoka huko juu, wakaingia kichwa kichwa,mabwana zao wakamwaga hela wakashinda.sasa wao wanarudi kwenye nyumba zao za vibatari mabwana zao wapo kwenye viyoyozi wanapanga kurudi tena kuwapa kofia kwenye uchaguzi ujao.swali langu kwao ni sasa wataishije huku uswailini coz najua hata salamu kupata itakuwa ngumu kupata...WALAANIWE
 
vizee badala ya kupumziak bado vinaikumbatia siasa ..vitakufa kw apresha we viache tu
 
Hakuna kitu kibaya kama kuishi kwa dhulma! Hawa watu wanaweza kucheka mchana lakini usiku ndani ya mioyo yao watakuwa wanyonge sana. And they can not change what happened. Kitabu cha historia ya nchi hii kitakuwa na ukarasa uliojaa majina yao.
 
Ninawaonea huruma kuisaliti jamii ambayo wewe ni mwanajamii humo humo sijui hata sura wataziweka wapi.
 
Kwani wanaishi kwenye vibanda gani hapo arusha? mwasameheni tu kwani hawajui watendalo.
 
Hakimu alietoa hukumu alikua kama PILATO, hakutenda haki kwa kuiogopa CCM kama PILATO alivyowaogopa WAYAHUDI na kuamuru YESU asulibiwe!
 
nadhani kufungua kwao kesi ni mtaji tosha wa kuipaisha chadema na kuifukia CCM
kwa ushindi waliopata jana kicheko chao kitaisha karibu watalia na kusaga meno
chadema watakaposhinda kwa kishindo kiti cha ubunge marudio na urais 2015
wao watajifia wenyewe kwa msongo wa mawazo na heart attck
 
tusiwe na shaka, kwani ukiangalia matukio yanayokikumba chama cha demokrasia na maendeleo yamekaa kama matukio ya ukombozi wa yesu kristo kwa wanadamu! Jaribu kukaa chini then fananisha matukio! CHADEMA NDIO ITAKAYOIKOMBOA TANZANIA BILA KIPINGAMIZI CHOCHOTE! WATAKUMBANA NA MENGI LAKINI MWISHO WAKE WATASHINDA NA KUIKOMBOA TANZANIA YETU TUKUFU!
 
Sipati picha juu ya uchaguzi ujao.Kile kilicho na kinachotegemewa na CCM hakitatokea.
Kuja kwa hukumu ya kesi siku 5 baada ya ushindi wa CDM huko Arumeru ni kama inasomeka hivi;
"TUKISHINDA ARUMERU WAACHIENI ARUSHA,TUKIPOTEZA KULE BASI TUWAPORE ARUSHA MJINI".
Kama mtazamo ulikuwa hivyo,wananchi watatoa hukumu yao pia baada ya siku 90.
 
Ili chama kiimarike ni lazima kipate misukosuko mingi na mingine lazima iwe migumu saana na kwa kufanikiwa kushinda misukosuko hiyo, kwanza kinaimarika na pili kinaaminiwa na wananchi kwamba kinaweza kujisimamia. Kwa hiyo hii ni njia katika kukipeleka CHADEMa katika level inayostahili.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom